Pia washiriki wa bahati nasibu ya taifa wataweza kununua tiketi na kupokea malipo ya ushindi kupitia majukwaa ya fedha kwa njia ya simu, USSD, hamisho kutoka benki, vituo vya malipo ya Selcom, na miamala ya kidijitali. Aidha, upatikanaji wa Selcom katika taasisi mbalimbali za kifedha utahakikisha kuwa hata wale wanaoishi maeneo yasiyofikika kiurahisi wanaweza kushiriki kikamilifu katika michezo ya bahati nasibu ya taifa.
Bahati nasibu ya Taifa si michezo ya kubahatisha tu bali pia ni chombo cha maendeleo ya taifa. Sehemu ya mapato yatokanayo na mauzo ya tiketi za bahati nasibu yatatengwa kwa ajili ya miradi muhimu kama vile kuendeleza michezo ya vijana chipukizi, na sekta nyingine zinazo igusa jamii. Ushirikiano huu na Selcom utakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ushiriki wa umma, hatimaye kuongeza mchango wa pato la Taifa kupitia miradi hii.
Usalama ni nguzo kuu ya ushirikiano huu, ambapo kupitia teknolojia bora ya Selcom washiriki wataweza kununua tiketi, kupokea malipo kidigitali kwa usalama ambao utazuia udanganyifu wa aina yoyote.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa ushirikiano huu, Shumbana Walwa, Mkuu wa idara ya Masoko wa Selcom Tanzania amesema, "Ushirikiano wetu na Bahati nasibu ya Taifa ya Tanzania unalenga kurahisisha ushiriki katika michezo ya kubahatisha kwa kila Mtanzania. Kupitia miundombinu yetu imara ya malipo, tutahakikisha kuwa mara tu Bahati nasibu ya Taifa itakapozinduliwa, wachezaji wataweza kushiriki kwa urahisi kupitia njia ambazo tayari wanaziamini na kuzitegemea. Tumejidhatiti kutoa huduma ya malipo salama, bora, na ya kuaminika ili kuongeza urahisi wa upatikanaji wa michezo ya bahati nasibu na ushiriki."
Kwanzia sasa, Bahati nasibu ya Taifa ya Tanzania na Selcom wataendelea kushirikiana kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata uzoefu wa kusisimua wa michezo ya bahati nasibu itakayopatikana katika jukwaa la Bahati nasibu ya Taifa, kwa usalama na uwazi wenye manufaa kwa watu binafsi na taifa kwa ujumla.
Kwa Mawasiliano zaidi:
📩 Mpange Chapeshamano
📧 mpangec@ithubatanzania.co.tz
📱 WhatsApp Channel
No comments:
Post a Comment