Dar es Salaam – Benki ya Exim Tanzania imechukua hatua madhubuti katika kuunda mustakabali wa malipo ya kidijitali kwa kuzindua ‘Lipa ChapChap’, suluhisho la malipo yasiyotumia fedha taslimu linalorahisisha miamala kwa wafanyabiashara na wateja binafsi. Zaidi ya kuwa huduma mpya, Lipa ChapChap ni hatua muhimu katika dhamira ya benki ya kuendeleza ujumuishi wa kifedha, ubunifu, na uchumi wa kidijitali nchini Tanzania.
Kuelekea katika uchumi usiotegemea fedha taslimu ni moja ya vipaumbele vikuu vya BoT, ikiwa na malengo ya kuongeza uwazi wa kifedha, kuimarisha ukusanyaji wa kodi, na kuongeza usalama katika miamala. Kupitia mifumo ya malipo ya kidijitali kama Lipa ChapChap, utegemezi wa fedha taslimu unapunguzwa, hivyo kupunguza hatari za wizi na udanganyifu.
Kwa mjibu wa BoT, miamala ya kidijitali nchini Tanzania imekua kwa kasi, ikichochewa na huduma za fedha za simu na ubunifu katika teknolojia ya kifedha. Huduma hii mpya ya Benki ya Exim inachochea mwenendo huu kwa kuhakikisha mifumo ya kifedha inafanya kazi kwa pamoja, na hivyo kuongeza matumizi ya malipo ya kidijitali kwa wigo mpana zaidi.
Naye Mkuu wa Idara ya Njia Mbadala za Kidijitali, Silas Matoi alisisitiza umuhimu wa usalama na ufanisi katika kuhamasisha matumizi, "Usalama ni nguzo kuu ya miamala ya kidijitali, na Lipa ChapChap inatoa uthibitisho wa papo hapo wa miamala, hivyo kuhakikisha wateja na wafanyabiashara wanapata huduma isiyo na wasiwasi. Kwa kuskani tu kupitia simu yako, malipo yanakamilika mara moja—hakuna haja ya kushika fedha taslimu au kadi. Ni salama, rahisi, na imeundwa kwa ajili ya kila mtu."
Dhamira ya Benki ya Exim ya kuleta mageuzi ya kidijitali haijaishia tu kwa Lipa ChapChap. Benki imeendelea kuzindua bidhaa bunifu zinazolenga kuongeza urahisi wa huduma za kibenki, kuongeza uelewa wa kifedha, na kuwezesha jamii kwa njia za kidijitali. Kwa kutumia teknolojia kutatua changamoto halisi, benki hii inachangia kuunda mustakabali wa sekta ya kifedha nchini Tanzania.
"Kama taasisi ya kifedha inayoangalia mbele, tumejidhatiti kutumia teknolojia kuleta suluhisho bunifu linalojali mahitaji ya wateja," alisema Stanley Kafu, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano kutoka benki ya Exim. "Lipa ChapChap ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuendesha mabadiliko ya kidijitali na uwezeshaji wa kifedha. Kwa kuondoa vikwazo vya malipo ya kidijitali, hatuleti tu bidhaa mpya—tunaunda mustakabali wa huduma za kifedha."
Kwa maono yanayolingana na sera za kitaifa na mwenendo wa kidijitali wa kimataifa, Benki ya Exim inajiimarisha kama mshirika muhimu katika mapinduzi ya fedha za kidijitali nchini Tanzania. Hili si tu suluhisho la malipo, bali ni nyenzo yenye nguvu ya kuendeleza ujumuishi wa kifedha, kuongeza ufanisi wa biashara, na kuharakisha safari ya nchi kuelekea uchumi wa kidijitali kamili.
Kadri Tanzania inavyoendelea kuukumbatia ulimwengu wa kidijitali, dhamira ya Benki ya Exim ya kuleta uvumbuzi wa kiteknolojia inahakikisha kwamba watu binafsi na wafanyabiashara wanapata huduma za kifedha kwa urahisi, usalama, na uhakika. Uzinduzi wa Lipa ChapChap ni mwanzo wa sura mpya ya kusisimua katika sekta ya kifedha nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment