Mkuu wa Idara ya wa M-pesa Tanzania, Jacqueline Ikwabe, amebainisha umuhimu wa ushirikiano huu kwa kusema, "M-Pesa imejikita katika kuwezesha uvumbuzi wa kidijitali unaowanufaisha wafanyabiashara na wateja. Kwa kuiunganisha Bahati Nasibu ya Taifa kwenye jukwaa letu, tutahakikisha ushiriki salama, wa haraka na rahisi huku tukifungua fursa zaidi za ushirikiano katika sekta mbalimbali."
Bahati Nasibu ya Taifa inalenga kutumia ushirikiano huu kuongeza uelewa wa huduma zake na kuimarisha uaminifu kabla ya uzinduzi rasmi wa Bahati nasibu ya Taifa. Hatua hii inatarajiwa kuweka msingi wa ushirikiano katika sekta ya michezo ya kubahatisha na fedha nchini Tanzania.
Ujumuishwaji wa jukwaa la Bahati nasibu ya Taifa kwenye majukwaa ya Vodacom Tanzania utarahisisha ununuzi wa tiketi na upatikanaji wa maudhui ya michezo ya kubahatisha kwa Watanzania wengi zaidi hapa nchini. Hatua hii ya kimkakati inatarajiwa kuongeza ushiriki wa umma, kupanua wigo wa huduma na kuhakikisha ushiriki mpana kutoka kwa makundi mbalimbali ya watu.
Kuhusu ITHUBA
ITHUBA ni muendeshaji rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania, aliyeteuliwa kwa kipindi cha miaka nane kuanzia mwaka 2025. Kama sehemu ya kampuni inayoongoza katika uendeshaji wa bahati nasibu barani Afrika, ITHUBA inaleta utaalamu na ubunifu wa hali ya juu hapa Tanzania, kwa kuhakikisha uzoefu wa michezo ya kubahatisha wa viwango vya kimataifa. Kampuni imejizatiti kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kuimarisha ajira, na kusaidia miradi ya michezo na jamii kwa ujumla.
Kuhusu Vodacom M-Pesa
Vodacom M-Pesa ni mtoa huduma mkubwa zaidi wa kifedha kwa njia ya simu nchini Tanzania, iliyoanzishwa na Vodacom Tanzania PLC mwaka 2008. Ikiwa na cheti cha GSMA na zaidi ya wateja milioni 11, M-Pesa imechangia kwa kiasi kikubwa ujumuishaji wa kifedha na ukuaji wa uchumi nchini. Wateja kuweza kuweka na kutoa fedha kupitia mawakala zaidi ya 160,000 kote nchini.
Mfumo wa M-Pesa unawaunganisha wafanyabiashara, benki na taasisi za serikali, kuwezesha malipo ya kidijitali. Mpaka sasa, M-Pesa inaendelea kuwa kinara wa huduma za kifedha kwa njia ya simu, ikitoa huduma bunifu kama Akiba & Mikopo, Kadi za Kielektroniki, Mikopo ya Dharura, Akiba za Vikundi, Malipo ya Kidijitali, na nyingine nyingi zinazokidhi mahitaji halisi ya Watanzania, hivyo kusaidia kuimarisha ujumuishaji wa kifedha nchini.
Kwa Maswali ya Vyombo vya Habari:
📩 Mpange Chapeshamano
📧 mpangec@ithubatanzania.co.tz
📱 WhatsApp Channel
No comments:
Post a Comment