Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 29 November 2024

NMB YAZINDUA WORLDWIDE PESA, HAKUNA MIPAKA KUTUMA FEDHA EAC, SADC


Benki ya NMB imezindua Huduma ya Kimkakati kwa Ustawi wa Sekta ya Fedha na Uchumi wa Taifa 'NMB Worldwide Pesa', inayowapa fursa Watanzania ya kutuma na kupokea pesa kutoka nchi 22 za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia simu za mkononi.


Uzinduzi wa NMB Worldwide Pesa ‘Dhumuni Halina Mipaka,’ umefanyika jijini Dar es Salaam Alhamisi Novemba 28, 2024 ikizinduliwa na Mkurugenzi wa Biashara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi John Ulanga.


NMB Worldwide Pesa inayoletwa kwa ushirikiano wa NMB, Mastercard, Thunes, TerraPay na Nala, ni zao la maboresho maalum ya huduma ya Worldwide Pesa iliyozinduliwa mwaka jana, ikilenga kuwawezesha Watanzania waishio nje ya nchi ‘Diaspora,’ kutuma fedha nchini kutokea kote duniani.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Alfred Shao, dhamira ya huduma hiyo ni kusapoti lengo la Serikali la kuongeza kiwango cha fedha kinachopokelewa kutoka kwa Diaspora wa Tanzania hadi kufikia kiasi cha Shilingi Trilioni 3.75 kwa mwaka ifikapo mwaka 2028.


Kwa kulitambua lengo hilo, nasi kuunga mkono, NMB tuko hapa kuleta masuluhisho muhimu ya kuendana na adhma hiyo ya Serikali na taifa letu kwa ujumla, na Worldwide Pesa itakuwa na mchango mkubwa sio tu wa kufanikisha lengo hilo, bali pia kutanua wigo wa huduma zetu na kuzifanya kuwa za kisasa zaidi."


Kwetu sisi NMB, ni heshima kubwa kwetu kupata imani kutoka kwa washirika wetu ambao ni taasisi za fedha kama Mastercard, Thunes, TerraPay na Nala, ambazo zina mtandao mpana na mahusiano na mabenki makubwa ya nchi nyingi za ndani na nje ya Afrika,” alibainisha Shao.


Aliongeza ya kuwa, ushirikiano wa taasisi hizo utaiwezesha NMB kuongeza tija ya huduma za kifedha (kutuma na kupokea), huku akitambia uwekezaji mkubwa ambao wameufanya kwenye Teknolojia ya Kidijitali hasa kwenye Kulinda Usalama wa Mifumo na Taarifa za Benki na Wateja ‘Cybersecurity Technologies.’


Aidha, Shao aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia kwa kujenga misingi imara inayoharakisha ukuaji wa sekta ya fedha, huku akiahidi benki yake kuendeleza mashirikiano mema na Benki Kuu ya Tanzania katika kuhakikisha taifa linapiga hatua za haraka za kimaendeleo

NMB UPGRADES WORLDWIDE PESA TO STREAMLINE INTERNATIONAL REMITTANCES



NMB Bank has taken the local payments industry to new heights by adding more value to its WorldWide Pesa remittance service, further enhancing and simplifying international money transfers.


The bank announced in Dar es Salaam that the new solution, which was originally designed for customers in the diaspora, now also enables outbound global payments through the NMB Mkononi service.


At the official launch of the new WorldWide Pesa, NMB's Chief of Wholesale Banking, Mr Alfred Shao, highlighted that the innovative solution, which allows customers to send funds abroad directly from their NMB accounts via smartphones, will initially be available in 22 countries in the EAC and SADC blocs.


The development, he added, aligns well with the government's efforts to boost diaspora remittances to USD 1.5 billion (about TZS 3.75 trillion) by 2028.


"With innovative solutions like the upgraded WorldWide Pesa service, NMB Bank is well-positioned and fully equipped to support the government's goal of increasing remittances from Tanzanians abroad who wish to send money and invest back home," Mr Shao stated.


According to him, the new solution that allows Tanzanians to securely and cost-effectively send and receive money globally via NMB Mkononi is the result of strategic partnerships with leading global and regional money transfer providers, namely Mastercard, Thunes, TerraPay, and Nala.


He explained that this collaboration was made possible by the significant investments NMB Bank has made over the years in building robust digital platforms and developing a strong team of ICT experts.


Highlighting that the new solution puts an end to the days of delays and complex paperwork often involved in global money transfers, Mr Shao described WorldWide Pesa as a technological transformation that streamlines international transactions, making them quick and convenient to complete anytime, and anywhere.

"The service we are launching today to simplify sending and receiving money internationally also plays a critical role in advancing the national financial inclusion agenda, while also contributing fully to national building efforts,” he noted.

STANBIC YASAIDIA KUTOA ELIMU NA KUHIFADHI MAZINGIRA KIGAMBONI

Meneja wa Kanda kitengo cha Huduma kwa Wateja katika Benki ya Stanbic, Bi Edditrice Marco, pamoja na Meneja wa Tawi la Industrial, Emma Medda (kulia) na Meneja wa Tawi la Kariakoo, Saleh Said (kushoto), wakiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ufukoni, Kigamboni, wakiwa wamekaa kwenye moja ya madawati 150 yaliyochangwa na benki hiyo kuboresha miundombinu ya kujifunzia.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mheshimiwa Halima Bulembo, akipokea moja ya mche kati ya miche 150,kutoka kwa Meneja wa Kanda, kitengo cha Huduma kwa Wateja Benki ya Stanbic, Bi Edditrice Marco, kama sehemu ya mpango wa kusaidia uhifadhi wa mazingira. Tukio hili lilifanyika Kigamboni - Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mheshimiwa Halima Bulembo, pamoja na Meneja wa Kanda kitengo cha Huduma kwa Wateja, Benki ya Stanbic Edditrice Marco, wakipanda mti kati ya miche ya miti 150, kuonesha dhamira ya benki hiyo ya kurejesha miti iliyotumika kutengeneza madawati yaliyotolewa. Jumla ya miche 150 ilitolewa kwa ajili ya mpango huo.
  • Stanbic Yatoa Msaada wa madawati 150 na miche ya miti 150 katika Shule ya Msingi Ufukoni.
  • Mradi unaonyesha dhamira ya Stanbic katika kuboresha elimu kote nchini.
  • Mpango huu ni sehemu ya dhamira ya Stanbic inayoendelea kwa maendeleo ya jamii.
Benki ya STANBIC Tanzania, mnamo tarehe 20 Novemba 2024, imedhihirisha dhamira yake ya kuongeza maendeleo ya jamii kwa kutoa msaada wa madawati 150 yenye gharama ya shilingi milioni 18.

Pamoja na msaada huo, vilevile STANBIC imetoa miche 150 ya miti kwa Shule ya Msingi ya Ufukoni iliyoko Wilayani Kigamboni jijini Dar es salaam.

Juhudi hizi zinalenga kuboresha miundombiu ya shule na kusaidia uhifadhi wa mazingira katika eneo hilo.

Hafla ya utoaji wa misada hiyo, ilihudhuriwa na Mgeni Rasimi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mhe Halima Bulembo, viongozi wa Chama na Serikali ya wanafunzi pamoja na wadau wengine wa maendeleo. Tangu Januari mwaka huu hadi sasa benki ya STANBIC imetoa jumla ya madawati 1,850 na imepanda jumla ya miti 50,450 ambayo ni ya kivuli na matunda kwenye shule mbali mbali nchini .

Akikabidhi madawati hayo,Meneja wa Benki ya STANBIC Tawi la Industrial Branch, Ndugu Emma Medda alisisitiza umuhimu wa msaada huo kwa kusema. “Madawati haya yatasaidia kuweka mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi na kuchangia katika lengo la kutoa elimu bora kwa wote".

ABSA BANK TANZANIA DRIVES CASHLESS ECONOMY WITH DIGITAL INITIATIVES

The first winner of Absa Bank Tanzania’s Spend & Win campaign, Mr. Rashidi Saidi (right) holds the ignition key to a brand-new 2024 Subaru Forester, shortly after it was presented to him by the bank’s Managing Director, Mr. Obedi Laiser (center), at an event in Dar es Salaam. The campaign aims to encourage more Tanzanians to adopt digital banking solutions, such as debit and credit cards, which offer safety, convenience, and access to a range of banking services.
Absa Bank Tanzania Managing Director, Mr. Obedi Laiser (third left), addresses participants during the handover ceremony of a brand-new 2024 Subaru Forester to the first winner of the bank’s ongoing Spend & Win campaign, Mr. Rashidi Saidi (third right), at an event in Dar es Salaam. The campaign aims to encourage more Tanzanians to adopt digital banking solutions, such as debit and credit cards, which offer safety, convenience, and access to a range of banking services.

Absa Bank Tanzania is intensifying its efforts to promote a cashless economy by encouraging the use of digital transactions.

The bank’s Managing Director, Mr. Obedi Laiser, highlighted that digital adoption not only enhances convenience but also reduces reliance on cash-based transactions, aligning with the government’s financial inclusion agenda.

“The use of banking services remains low in our country. As financial stakeholders, we must innovate to encourage citizens to embrace formal financial systems,” said Mr. Laiser during the second draw and handover ceremony for the bank’s ongoing three-month Spend & Win campaign. The first winner of the campaign received a brand-new 2024 Subaru Forester.

Mr. Laiser added, “The campaign’s theme, ‘Winning a car can change your story,’ aligns with our brand promise, ‘Your story matters.’ At Absa, we strive to be part of our customers’ journeys, helping them achieve their goals and dreams step by step.”

The push towards a cashless economy is gaining momentum, supported by initiatives such as the growing use of mobile money services, career-oriented financial programs, and digital banking solutions that enhance access to financial services.

Thursday, 28 November 2024

NMB YATOA MSAADA WA VIFAA VYA SH. MIL. 23 KATIKA SHULE 3 MUFINDI


Benki ya NMB imetoa msaada wa mabati 150 na madawati 150 kwa shule za msingi KASANGA, KISASA na SAWALA zilizopo wilayani Mufindi mkoani Iringa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni 23.


Msaada huo kutoka benki hiyo ni sehemu ya kuunga mkono jithada za serikali katika sekta ya elimu pamoja na kurejesha kwa jamii kama ilivyo utaratibu wa benki hiyo.


Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Ndg. Benedicto Baragomwa alisema lengo kubwa la Benki ya NMB ni kuhakikisha inawafikia wateja wake kote nchini kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu.


“Nilikutana na Mbunge wenu wa Mufindi Kusini, Mhe. David Kihenzile akanieleza kuhusu changamoto ya madawati katika shule hii ya Kasanga, Sawala na Kisasa nami nikamuahidi nitafanyia kazi kilio chake na leo kupitia sera yetu ya kurejesha kwa jamii tumewafikia”, alisema Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Ndg. Benedicto Baragomwa.


Baragomwa pia ameziagiza kanda za nyanda za juu kusini za benki hiyo kufanya tathmini ya kina kuhusu uchakavu wa shule mbalimbali na mahitaji ili kusaidia wanafunzi kusoma kwenye mazingira bora.


Aliongeza kuwa Benki ya NMB imepokea ombi la uhitaji wa mabati 110 kutoka Shule ya Msingi Kasanga na wanakwenda kulifanyia kazi ili kuona uwezekano wa kuwapunguzia mzigo wa michango wazazi na walezi.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile ameishukuru na kuipongeza Benki ya NMB kwa msaada huo mkubwa ambao unakwenda kuondoa kabisa kadhia ya wanafunzi kuketi chini na hata nyakati zingine kunyeshewa na mvua kwa madarasa kuvuja.


Kihenzile aliwataka wananchi kutumia Benki ya NMB kwa kufungua akaunti mbalimbali ili waweze kujiweka akiba na kuwapa nguvu ya kuendelea kurejesha kwa jamii huku akiipigia chapua benki hiyo kwa kutoa mikopo ya papo hapo kupitia simu ya mkononi.

SBL YAPAISHA VIWANGO VYA SEKTA YA UKARIMU KUFIKIA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Meneja wa Taaluma kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Mary Maduhu akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo ya Utalii na Ukarimu ambayo yanatolewa kwa wanafunzi kwa chuo hicho kwa kushirikiana na Kampuni ya SBL kupitia programu yake ya 'Learning for Life'. Kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Ukarimu NCT, Jafari Mwemtsi, Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu (watatu kushoto), Mariam Mambosasa, Meneja wa Huduma Saidizi za Kitaaluma, na Claudia Nshekanabo - Mkuu wa Idara ya Uratibu wa Matukio NCT.

Dar es Salaam, Novemba 27, 2024: Wanafunzi wanaosomea fani ya ukarimu katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) sasa watapata mafunzo ya ziada ya miezi mitatu kutoka kwa watalaamu wa Serengeti Breweries Limited (SBL) huku kampuni hii ikilenga kusaidia kujenga kizazi kipya cha wataalamu wa sekta ya utalii na ukarimu inayokua kwa kasi nchini Tanzania.


Kupitia makubaliano yaliyosainiwa mwezi Septemba kati ya chuo hicho na SBL, kundi la kwanza la wanafunzi zaidi ya 100 tayari wamejiunga na mpango huu kama sehemu ya mpango wa mafunzo ya ujuzi wa maisha uitwao "Skills for Life".


Wanafunzi hawa watajifunza miongoni mwa mambo mengine, viwango vya kimataifa vya utoaji wa vinywaji vya pombe ikiwa ni pamoja na ustadi wa kutengeneza mchanganyiko wa vinywaji vilivyo (cocktails) na visivyo na kilevi (mocktails), pamoja na kuboresha viwango vya huduma za baa na vinywaji.


“Haya ni mafunzo ya kipekee yanayoenda mbali na ujuzi wa kiufundi na kutoa mafunzo ya ujuzi wa maisha kama vile kutengeneza chapa binafsi, usimamizi wa muda, uongozi, na ufanisi katika mawasiliano,” alisema Rispa Hatibu wakati wa hafla ya ufunguzi wa kundi hilo la kwanza la wanafunzi.


Hatibu, ambaye ni Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, alisisitiza dhamira ya kampuni katika maendeleo ya vijana akisema, “Mpango huu ni zaidi ya ujuzi tu—ni kuhusu kuwawezesha vijana na zana za kubadilisha maisha yao na kusaidia ukuaji wa sekta ya utalii na ukarimu nchini.”


Kwa upande wake, Mary Maduhu ambaye ni Meneja wa Taaluma kutoka NCT alielezea programu hii kama ishara ya maono ya ushirikiano kati ya SBL na NCT. “Mafunzo haya siyo tu yanahusu ujuzi wa kiufundi; ni kuhusu kufungua uwezo na kuhamasisha vipaji kwa wanafunzi. Pia ni mwanzo wa safari kuelekea ukuaji wa kitaaluma na kibinafsi,” alisema Maduhu.

MULTICHOICE, VODACOM WAZINDUA SHOWMAX TANZANIA



Dar es Salaam, Tanzania, 25 Novemba 2024 – MultiChoice Tanzania imetangaza ushirikiano na Vodacom Tanzania PLC, kampuni inayoongoza katika mawasiliano ya simu nchini, kwa ajili ya kuzindua Showmax – jukwaa maarufu la burudani kupitia video barani Afrika. Ushirikiano huu muhimu unaashiria zama mpya za burudani bora na rahisi kufikiwa Tanzania, huku ukiunga mkono matumizi ya kidijitali nchini na kuinua vipaji vya ndani.


Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Jacqueline Woiso, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, alisema, “hili ni tukio kubwa nchini kwetu ambapo makampuni makubwa mawili katika sekta za mawasiliano na burudani wameungana kwa maslahi ya wateja wetu. Ushirikiano huu unasisitiza dhamira yetu ya kutoa maudhui ya kimataifa ya kiwango cha juu huku tukitumia teknolojia ya kisasa ya Vodacom Tanzania.”


Woiso aliongeza, “Ushirikiano huu utawezesha wateja wa Vodacom kote Tanzania kupata maudhui bora ya vipindi vya TV, filamu, michezo, na makala kupitia Showmax, hivyo kufanya burudani ya kiwango cha juu iwe rahisi kufikiwa katika vifaa mbalimbali vya kidijitali. Showmax ina maktaba kubwa ya maudhui inayojumuisha uzalishaji wa ndani na nje ya Tanzania, pamoja na michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza, ikienda sambamba na ladha mbalimbali za burudani. Ushirikiano huu ni mfano dhahiri wa jinsi ushirikiano unavyoweza kuleta thamani kubwa kwa wateja, kuweka maslahi yao mbele ya ushindani.”


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Phillip Besiimire, alisema “Ushirikiano huu unaendana kikamilifu na dhamira yetu ya kusaidia Tanzania kuelekea zama za kidijitali huku tukiboresha maisha kupitia teknolojia. Kadri upatikanaji wa simu janja unavyoongezeka nchini, tumejikita katika kuboresha huduma zetu za kidijitali kwenye burudani, elimu, kilimo, afya, na usafiri. Leo, tunajivunia kuongeza Showmax katika orodha yetu ya burudani, tukiwawezesha wateja wetu kufurahia maudhui ya kiwango cha juu yanayowagusa moja kwa moja.”


Uzinduzi wa Showmax pia unaangazia umuhimu wa kuunga mkono vipaji na uzalishaji wa maudhui ya ndani. Kupitia maudhui ya ndani yanayoonyeshwa kwenye jukwaa hili, lengo ni kuinua sauti za wasanii wa Kitanzania na kuhakikisha kazi zao zinafikia hadhira kubwa zaidi. Hatua hii si tu inaimarisha sekta ya burudani bali pia inachangia ukuaji wa uchumi wa ubunifu wa ndani.


Ili kunufaika na ushirikiano huu, Vodacom na MultiChoice wanatoa vifurushi vya kipekee vya data vinavyowezesha wateja wa Vodacom kufurahia maudhui ya burudani kwa gharama nafuu. Watumiaji wanaweza kupakua programu ya Showmax, kununua kifurushi, na kufurahia ulimwengu wa burudani ya kuvutia.






VODACOM YAWAPA SHANGWE WATEJA WAKE MSIMU HUU WA SIKUKUU NA KAMPENI YA ‘SHANGWE POPOTE UKITUMIA M-PESA’

RUDISHIWA NAULI YAKO! Mteja wa Vodacom Tanzania Plc, Regina Mbalamwezi akirudishiwa nauli yake baada ya kukata tiketi ya basi kupitia M-Pesa kutoka Dar es Salaam Kwenda Morogoro wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa’ katika kituo cha mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam.
SHANGWE POPOTE! Mkurugenzi wa Biashara kutoka Vodacom Tanzania, Brigita Shirima akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo ya ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa!’ lenye lengo la kuhamasisha wateja wake kufanya miamala yao kutumia M-Pesa wakati wa msimu huu wa sikukuu. Kushoto ni Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni.
FURAHIA POPOTE ULIPO! Timu kutoka Vodacom Tanzania Plc wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa!’ tarehe 26 Novemba 2024 jijini Dar es Salaam kuhamasisha wateja wa Vodacom kutumia kufanya malipo kutumia M-Pesa ambapo wanajiweka kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwamo wateja 1,500 kurudishiwa nauli za mabasi, tiketi 100 za bure za SGR pamoja na punguzo za aina mbalimbali katika miamala yao.
SHANGWE LA SIKUKUU! Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Biashara kutoka Vodacom Tanzania, Brigita Shirima (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa’ uliofanyika kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Uzinduzi wa kampeni kabambe ya 'Shangwe Popote Ukilipa Kwa M-Pesa' ambayo inahamasisha wateja wa Vodacom kufanya miamala kupitia M-Pesa'.