Aliongeza kuwa sekta ya utalii ya Tanzania inakua kwa kasi na hivyo kuongeza mahitaji ya nguvu kazi yenye ujuzi wa sekta hiyo, pengo ambalo alisema ushirikiano kati ya SBL na NCT utasaidia kulijaza kwa kutengeneza nguvu kazi inayokidhi viwango vya kimataifa vya ukarimu.
“Zaidi ya athari yake ya moja kwa moja kwa wanafunzi, programu hii pia inaashiria dhamira pana kwa maendeleo endelevu. Kwa kukuza talanta na kuongeza ajira, SBL na NCT wanachangia katika ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa taifa la Tanzania,” aliongeza Mkuu huyo wa Taaluma.
No comments:
Post a Comment