Kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohamed Thabit Kombo, Balozi Ulanga aliipongeza NMB kwa mapinduzi chanya na uwekezaji mkubwa wa kiteknolojia katika kufanikisha huduma rahisi, rafiki, nafuu na salama kwa ukuaji wa haraka wa uchumi wa wateja na Watanzania.
“Siri namba moja ya mafanikio yenu ni pamoja na kujali wateja na namna ya kutatua changamoto zao, pili matumizi ya teknolojia kwa sababu kampuni zote zilizofanikiwa duniani, zimefaanya uwekezaji katika eneo hilo na siri ya tatu ni wafanyakazi weledi, wabunifu na mkiendelea ‘ku-focus’ katika hayo, mtafanikiwa zaidi.”
“Sisi kama Serikali tuna furaha kuona huduma yenu hii mpya imeanza na nchi 22 wanachama wa Jumuiya mbili kubwa Afrika yaani Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Afrika (SADC), kwani itakuwa chachu ya mzunguko wa fedha katika ukanda huu, ambao sisi ni wanachama wa jumuiya zote mbili,” alisisitiza.
Balozi Ulanga aliitaka NMB kuunda mfumo utakaowezesha matumizi ya huduma hiyo kutoka benki zote na kwamba hilo litaharakisha na kuongeza kasi ya ukuaji wa taasisi hiyo, ambayo kwa ilipofikia inapaswa kuvuka mipaka ya nchi na bara la Afrika kutokana na ukubwa na ubora wake kihuduma
“Kwa sasa wacha tuendelee na mataifa 22, lakini dhamira iwe kuvuka mipaka ya kujitanua kama ndio kweli benki bora ya kimapinduzi, napowapongeza kwa ‘innovation’ hii, nitumie nafasi hii kuwaahidi kuwa Wizara tuko tayari kuwasaidia kufikia malengo yenu, ambayo yanasaapoti uchumi wa taifa.”
“Kwa ‘innovation’ hizi, haitoshi kusema NMB tupo tu Tanzania, tunapaswa kuvuka mipaka ya nchi na bara zima la Afrika. Tuna wafanyabiashara hapa kutoka mataifa ya Comoro, DRC, ambao kitovu cha ukuaji wao kibiashara ni Tanzania, kwahiyo tunapaswa kuiona NMB Bank nchini Comoro, ambako itakuwa kubwa kule,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Akaunti – Afrika Mashariki wa Thunes, Jack Ngari, aliishukuru NMB kwa kujenga msingi imara wa ushirikiano kihuduma na kwamba imani waliyopata kutoka kwa NMB inawapa nguvu ya kushiriki ukuzaji uchumi wa Tanzania, jambo ambalo ni fahari kwao.
Naye Doreen Ngallo, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TerraPay, alisema wanajivunia miaka mitano ya ushirikiano wa kibiashara na NMB, wenye wastani wa miamala ya kimataifa yenye thamani ya zaidi ya Dola Mil. 1.2 na kwamba uzinduzi wa NMB Worldwide Pesa unawapa uhakika wa kuongezeka kwa miamala hiyo.
No comments:
Post a Comment