- Stanbic Yatoa Msaada wa madawati 150 na miche ya miti 150 katika Shule ya Msingi Ufukoni.
- Mradi unaonyesha dhamira ya Stanbic katika kuboresha elimu kote nchini.
- Mpango huu ni sehemu ya dhamira ya Stanbic inayoendelea kwa maendeleo ya jamii.
Pamoja na msaada huo, vilevile STANBIC imetoa miche 150 ya miti kwa Shule ya Msingi ya Ufukoni iliyoko Wilayani Kigamboni jijini Dar es salaam.
Juhudi hizi zinalenga kuboresha miundombiu ya shule na kusaidia uhifadhi wa mazingira katika eneo hilo.
Hafla ya utoaji wa misada hiyo, ilihudhuriwa na Mgeni Rasimi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mhe Halima Bulembo, viongozi wa Chama na Serikali ya wanafunzi pamoja na wadau wengine wa maendeleo. Tangu Januari mwaka huu hadi sasa benki ya STANBIC imetoa jumla ya madawati 1,850 na imepanda jumla ya miti 50,450 ambayo ni ya kivuli na matunda kwenye shule mbali mbali nchini .
Akikabidhi madawati hayo,Meneja wa Benki ya STANBIC Tawi la Industrial Branch, Ndugu Emma Medda alisisitiza umuhimu wa msaada huo kwa kusema. “Madawati haya yatasaidia kuweka mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi na kuchangia katika lengo la kutoa elimu bora kwa wote".
Naye Meneja wa Tawi la Benki ya STANBIC Kariakoo, Bw. Saleh Said Awadh ambaye alitoa miti hiyo, alitoa maelezo kuhusu umuhimu wa upandaji miti kwa kusema, Miche hiyo inaonesha dhamira ya STANBIC ya kulinda mazingira na kuhakikisha kwamba vizazi vijavyo vitafurahia dunia ya kijani na yenye afya.
Wakati akitoa nasaha kwenye hafla hiyo Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo alisema, “Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Benki ya STANBIC kwa Uzalendo wa kujitolea katika kuboresha elimu na kuhimiza utunzaji wa mazingira. Huu ni mfano mzuri wa Kuigwa ambapo imeonyesha ni jinsi gani sekta binafsi inavyoweza kushiriki katika kutatua changamoto zinazoikumba jamii yetu”
Aliwataka washiriki wa hafla hiyo hususan walimu, wanafunzi na jamii yote ya eneo hilo kwa ujumla kuendelea kutunza na kutumia vyema rasilimali hizo zilizotolewa na STANBIC "Yatumieni madawati haya vizuri, na mtunze miche hii ya miti ili iwe alama ya uelewa wa mazingira." Alisisitiza Mhe Bulembo. Aliendelea kusisitiza kuwa Kutoa madawati 150 ni hatua kubwa inayotegemea kubadilisha maisha ya wanafunzi shuleni hapo. "Tunafahamu changamoto za ukosefu wa vifaa vya kutosha mashuleni. Msaada huu hakika utakuwa suluhisho litakaloboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wetu na kuwawezesha kufikia malengo yao ya kielimu na ndoto zao za Maisha,' alisema.
Akielezea kuhusu miche ya miti 150 iliyotolewa na Benki hiyo Mhe Bulembo aliongeza kwa kusema kuwa huo si mchango wa siku hiyo pekee, bali ni uwekezaji wa muda mrefu kwa ajili ya mazingira yetu, kwakuwa Miti hiyo sio tuu itatoa kivuli bali itaboresha mazingira ya shule na pia kuonyesha umuhimu wa kutunza mazingira. Hii ikiwa ni pamoja na kuwafundisha wanafunzi na jamii nzima kuhusu uendelevu na uwajibikaji wa utunzaji mazingira.
Msaada huo ulitokana na ushirikiano wa wafanyakazi kutoka matawi ya STANBIC Industrial na Kariakoo ambao nisehemu ya jitihada za mpango unaoendelea wa benki hiyo uitwao Stanbic Madawati Initiative, unaolenga kuchangia madawati zaidi kwenye shule mbalimbali nchini Tanzania.
Tangu kuzinduliwa kwa mpango huo, umekwisha nufaisha shule mbalimbali nchini na kupitia ushirikiano huu, Benki ya STANBIC inaendelea kuoanisha juhudi zake na malengo ya maendeleo ya Tanzania chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayo ongozwa na Mhe Dr Suluhu Hasan kwa kusaidia mipango ya elimu endelevu. Benki inaendelea kujitolea kujenga mustakabali mwema kwa jamii za Kitanzania kwa kuwekeza katika miradi ambayo inaacha athari chanya na za kudumu.
Ushirikiano wa muda mrefu kati ya Serikali na Benki ya STANBIC kwenye sekta ya Elimu na uhifadhi wa mazingira unasaidia kuimarisha benki hiyo kuwa taasisi inayoongoza ajenda ya maendeleo ya Tanzania. Kwa kuwa Benki inajenga msingi wa uchumi endelevu zaidi kwa kuwekeza katika elimu na mipango endelevu ya maendeleo.
Kwa habari zaidi, tafadhali wasiliana na:
Jina: Azda Nkullo
Title: Meneja Masoko wa Biashara katika Benki ya Stanbic Tanzania
Barua Pepe: azda.nkullo@stanbic.co.tz
Kuhusu Benki ya Stanbic Tanzania ni mtoa huduma bora za kifedha nchini Tanzania, inayotoa bidhaa na huduma mbalimbali kwa wateja binafsi, biashara na makampuni. Kama kampuni tanzu ya Standard Bank Group, Benki ya Stanbic Tanzania inatumia ujuzi na utaalamu wake wa ndani kwa kufikia kimataifa na uwezo wa Benki ya Standard kusaidia ukuaji na maendeleo ya wateja wake.
No comments:
Post a Comment