Milu alijiunga na Bolt mwaka wa 2018 kama Meneja Mkazi nchini Tanzania, ambapo amekuwa na umuhimu katika kuhakikisha ukuaji wa biashara wa kampuni na mafanikio. Mtazamo wake wa kibunifu katika kutatua changamoto za kiutendaji na kujitolea katika kuridhisha wateja wetu wa Biashara/makampuni kwa kuhakikisha Bolt Business kama chaguo namba moja na linalopendelewa zaidi kwa huduma za usafiri katika eneo hili.
Juliano Fatio, ambaye ni Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika & Masoko ya Kimataifa ya Bolt Business barani alisema: "Tuna furaha kubwa kumpandisha cheo Milu kwa kutambua uongozi wake bora. Uzoefu wake mkubwa na mafanikio yaliyothibitishwa yatakuwa muhimu tunapopanua shughuli zetu na kuboresha bidhaa yetu nchini Tunisia na Ghana. Katika jukumu lake jipya, Milu atatekeleza mbinu bora katika nchi zote tatu, kuhimiza ushirikiano kati ya timu za wenyeji, na kuboresha utoaji wa huduma za Bolt ili kuwahudumia vyema wateja na washirika wetu. Zaidi ya hayo, ataongoza mipango inayolenga kuendesha ufanisi wa uendeshaji na kuimarisha uhusiano na wadau wa ndani.
Milu Kipimo, Meneja Mwandamizi wa Bolt Business alisema: “Ninayo furaha kubwa ya kupata nafasi hii ya kukabiliana na changamoto hii mpya na ninashukuru kwa fursa ya kuongoza mipango yetu katika masoko haya yanayokuwa. Kwa kujitolea kwa timu zetu zenye uwezo nchini Tanzania, Tunisia na Ghana, nina imani kwamba tutatoa suluhisho ya kibunifu ya usafiri ambayo Itawezesha jamii na kuboresha maisha katika eneo zima.
Ukuaji huu wa kimkakati unalingana na maono ya Bolt Business ya kupanua wigo wake kote barani Afrika, na kuimarisha dhamira yake ya kutoa chaguzi za usafiri zinazotegemewa, nafuu na salama kwa mamilioni ya watumiaji.
No comments:
Post a Comment