Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 19 June 2023

NMB YATOA GAWIO LA BILIONI 45.5, RAIS SAMIA APONGEZA

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Gawio la Serikali la TShs. Bilioni 45.5 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 25 ya mafanikio ya benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba na kushoto ni Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu.

Benki ya NMB imeandika historia!

Benki ya NMB imetoa gawio la TShs. Bilioni 45.5, ikiwa ni gawio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na Taasisi ya kifedha kwa Serikali. Gawio hili kwa serikali ni kiashiria tosha cha Azma yetu ya kuhakikisha tunaleta tija na faida kubwa kwa wawekezaji wetu wote, ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NMB - Dkt. Edwin Mhede pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu - Ruth Zaipuna, wamemkabidhi Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Dkt. Samia Suluhu Hassan mfano wa hundi ya gawio hilo katika sherehe ya maadhimisho ya mikaa 25 ya mafanikio ya Benki ya NMB katika ukumbi wa Mlimani City – Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango - Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Msajili Wa Hazina - Nehemiah Mchechu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania - Emmanuel Tutuba pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

No comments:

Post a Comment