Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 31 March 2023

NEWCASTLE VS MAN UNITED JUMAPILI HII NDANI YA DStv



Jumapili hii NewCastle United anakipiga na Manchester United. Je mashabiki wa Man U watapata ushindi wikiendi hii?

Mtonyo wa #PandaTukupandishe unaisha leo wewe mteja wa Bomba lipia sasa kifurushi cha Shangwe upandishwe cha Compact ufurahie mechi hii Live ndani ya @dstvtanzania pekee.

Piga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema!

#MsimuwaSokalaKibabe

NMB BONGE LA MPANGO - 'MOTO ULEULE' YAZINDULIWA, WATEJA KUZOA MILIONI 180

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Paul Chacha pamoja na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB - Filbert Mponzi wakipeperusha bendera kama ishara ya kuzindua rasmi kampeni ya Bonge la Mpango – Moto Uleule, katika uzinduzi uliofanyika katika soko la Buhongwa jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa Benki ya NMB, Wogofya Mfalamagoha, wa pili kulia ni Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi, Aikansia Muro na kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa - Ladislaus Baraka.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB - Filbert Mponzi (wa pili kushoto) akimfungulia akaunti ya NMB dereva bodaboda katika soko la Buhongwa jijini Mwanza wakati wa kuzindua rasmi kampeni ya Bonge la Mpango – Moto Uleule. Akishuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi – Mhe. Paul Chacha (pili kulia).

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi - Paul Chacha akimkabidhi kadi ya benki dereva bodaboda katika soko la Buhongwa jijini Mwanza, baada ya kumfungulia akaunti ya NMB wakati wa uzinduzi rasmi wa Bonge la Mpango – Moto Uleule. Wakishuhudia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB - Filbert Mponzi, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa - Ladislaus Baraka (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi - Aikansia Muro.

Msimu wa Tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa kuweka pesa Benki ya NMB 'NMB Bonge la Mpango - Moto ni Ule Ule', umezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza- Paulo Chacha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima, ambako zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 180 - zikiwemo pesa taslimu, bodaboda, pikipiki za mizigo za matairi matatu na vifaa vya nyumbani vya kieleltroniki, zitatolewa katika kipindi cha miezi mitatu.

Bonge la Mpango inalenga sio tu kuhamasisha uwekaji akiba, bali pia kurejesha kwa jamii sehemu ya faida yake, huku pia ukiwa ni mkakati wa NMB kuendelea kuwa chaguo la kwanza la wateja kwa usalama wa fedha zao pamoja na uhakika wa huduma bora na rafiki za kibenki nchini.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa NMB Bonge la Mpango katika soko la Buhongwa, madereva 10 wa bodaboda, bajaji na matoroli wanaoendesha shughuli katika soko hilo, walifunguliwa akaunti na Mkuu wa Wilaya Chacha pamoja na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Filbert Mponzi na kuwakewa kiasi cha Sh. 100,000 kwa kila mmoja ili kukidhi kigezo kikuu cha kuingia kwenye droo ya promosheni hiyo na kushinda zawadi.

SHULE 20 TABORA ZAKABIDHIWA VIFAA VYA TEHAMA VYENYE THAMANI YA TSHS 150 MILIONI NA VODACOM TANZANIA FOUNDATION



Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mh. Balozi Dk. Batilda Buriani (kulia) akipokea msaada wa mojawapo ya kompyuta na vifaa vingine vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi milioni 150 kwa shule za sekondari 20 kutoka kwa Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania Plc Kanda ya Ziwa, Bw. Ahmed Akbarali (katikati) ikiwa ni sehemu ya mradi wa uunganishwaji wa shule za sekondari unaolenga kuziunganisha shule 300 Tanzania, (school connectivity project), kwa kushirikiana na African Child Projects na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). Akishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika katika shule ya sekondari Kariakoo mkoani humo, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Bi. Neema Kapesa.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mh. Balozi Dkt. Batilda Buriani (katikati) akishuhudia makabidhiano ya msaada wa mojawapo ya kompyuta na vifaa vingine vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi milioni 150 kwa shule za sekondari 20 kutoka kwa Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania Plc Kanda ya Ziwa, Bw. Ahmed Akbarali (kushoto) kwenda kwa Mkurugenzi wa Shirika la Youth Relief Foundation, Bw. Joachim William (kulia), ikiwa ni sehemu ya mradi wa uunganishwaji wa shule za sekondari unaolenga kuziunganisha shule 300 Tanzania (school connectivity project), kwa kushirikiana na African Child Projects na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Afisa Elimu Taluma Sekondari Mkoa wa Tabora, Bi. Rosemary Massawe (kushoto) akikabidhi mojawapo ya kompyuta kwa mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Kariakoo, Bw. Leonard Nyasebwa (kulia) huku Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Manispaa ya Tabora, Bi. Neema Kapesa akishuhudia. Vodacom Tanzania Foundation imesaidia vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi milioni 150 kwa shule za sekondari 20 mkoani humo ikiwa ni sehemu ya mradi wa uunganishwaji wa shule za sekondari unaolenga kuziunganisha shule 300 Tanzania (school connectivity project), kwa kushirikiana na African Child Projects na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kariakoo ya Tabora, wakijisomea kwenye chumba cha kompyuta baada ya kupokea msaada wa vifaa tofauti vya TEHAMA kutoka Vodacom Tanzania Foundation. Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 150 ulitolewa kwa shule za sekondari 20 mkoani humo ikiwa ni sehemu ya mradi wa uunganishwaji wa shule za sekondari unaolenga kuziunganisha shule 300 Tanzania (school connectivity project), kwa kushirikiana na African Child Projects na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Tabora – Machi 30, 2023: Vodacom Tanzania Foundation imekabidhi msaada wa vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 150 milioni kwa shule za sekondari 20 mkoani Tabora ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uunganishwaji wa shule kwa kushirikiana na taasisi ya African Child Projects na Mfuko wa Mawasiliono Sawa kwa Wote (UCSAF) ambao unalenga kuzifikia shule 300 nchini kote.



Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Kariakoo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani alipongeza jitihada za mpango wa uunganishwaji wa shule katika kuboresha mfumo tulionao sasa wa ufundishaji na kujifunzia kuhamia kwenye mfumo wa kidigitali.

Thursday, 30 March 2023

BENKI YA NMB YADHAMINI MKUTANO WA WAHARIRI MOROGORO

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (katikati) akiteta Jambo na Kaimu Meneja Tawi la NMB Wami, Paul Nyoni baada ya kupokea Cheti cha shukrani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa mwaka wa kitaaluma wa wahariri wenye kauli mbiu ya "Sheria ya habari na maendeleo ya vyombo vya habari" unaofanyika mkoani Morogoro. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deudatus Balile na Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Bakari Machumu (kulia kabisa). Benki ya NMB ilishiriki kama mdhamini kwenye mkutano huo unaoendelea Hoteli ya Morena, Morogoro.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akimkabithi Kaimu Meneja Tawi la NMB, Wami Paul Nyoni (kulia) Cheti cha shukrani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa mwaka wa kitaaluma wa wahariri wenye kauli mbiu ya "Sheria ya habari na maendeleo ya vyombo vya habari" unaofanyika mkoani Morogoro. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deudatus Balile (kushoto) na Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Bakari Machumu (wa pili kulia). Benki ya NMB ilishiriki kama mdhamini kwenye mkutano huo unaoendelea Hoteli ya Morena, Morogoro.

LETSHEGO BANK AND AIRTEL MONEY LAUNCH A SAVE AND WIN PROMOTION


Dar es Salaam, Tanzania: Letshego Bank Tanzania, a subsidiary of Letshego Holdings Limited (Letshego Group), has, in partnership with Airtel Money, announced the launch of Vimba na Timiza Akiba, an eight weeks promotion that aims at encouraging Tanzanians to save digitally by offering them an opportunity to win Bajaji, Motorcycles, Television Sets and Cash prizes.


Speaking during the launch of the promotion, Letshego Bank Tanzania Head of Sales, Leah Phil, said, "We are excited to partner with Airtel Money to launch the Vimba naTimiza Akiba promotion. We believe that digital savings are the future of financial services, and we are committed to providing innovative products that meet the needs of our customers. For this promotion, we want to assure all Airtel Money customers that they will get their prizes through Airtel Money accounts immediately after they are declared the winners."


Timiza Akiba is a digital saving product, offered by Letshego Bank in partnership with Airtel Money, that enables individuals to save money directly from their Airtel Money account. The product is designed to provide a safe, convenient, and reliable way for Tanzanian’s to save money and achieve their financial goals while earning 4.5% per annum on interest.

BENKI YA NMB YAKABIDHI VIFAA VYA ELIMU MOROGORO

Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa (kushoto) akipokea moja ya viti 100 na meza 100 kutoka kwa Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi wakati wa ugawaji wa vifaa vya elimu kwa shule ya msingi Sinyaulime iliyopo kata ya Ngerengere na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa Manispaa ya Morogoro ambapo taasisi hizo zimepokea msaada msaada wa vifaa vya sekta ya elimu vyenye jumla ya Sh. 12.5 milioni.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa (katikati waliokaa) na Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (wa kwanza kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shule ya msingi Sinyaulime iliyopo kata ya Ngerengere na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa Manispaa ya Morogoro baada ya benki hiyo kutoa viti 100 na meza 100 na vifaa vya ujenzi wakati wa ugawaji wa vifaa vya elimu kwa ambapo taasisi hizo zimepokea msaada wa vifaa vya sekta ya elimu vyenye jumla ya Sh. 12.5 milioni.
 
Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa (wa kwanza kushoto) na Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (wa kwanza kulia) wakikabidhi sehemu ya vifaa vya ujenzi kwa viongozi wa shule ya msingi Sinyaulime iliyopo kata ya Ngerengere wakati wa hafla ya kupokea msaada iliyofanyika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Manispaa ya Morogoro ambapo taasisi hizo zimepokea msaada ya jumla ya Sh. 12.5 milioni.

Morogoro - Benki ya NMB imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya msingi Sinyaulime na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa (FDC) ikikabidhiwa meza na viti vikiwa na vyenye thamani ya sh12.5 milioni wakati wa hafla iliyofanyika Bigwa, ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha sehemu ya faida kwa jamii ikiwemo sekta ya elimu hapa nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo mjini hapa, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi amesema benki hiyo imekabidhi meza 100 na viti 100 kwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Manispaa ya Morogoro wakati shule ya msingi Sinyaulime iliyopo kata ya Ngerengere ikikabidhiwa vifaa vya ujenzi.

Mlozi amesema benki ya imekuwa na utamaduni wa kutoa misaada kunatokana na faida wanayopata kila Mwaka na asilimia moja ya faida hiyo kuipeleka kwenye huduma za kijamii.

Wednesday, 29 March 2023

MAN CITY VS LIVERPOOL LIVE NDANI YA DStv JUMAMOSI HII


Manchester City kukipiga na Liverpool LIVE Jumamosi hii ndani ya @dstvtanzania pekee!

Nani kupata alama 3?

Zimebaki siku 2 mtonyo wa #PandaTukupandishe uishe sasa basi mteja wa Bomba changamkia mtonyo huu mapema kwa kulipia kifurushi cha Shangwe upandishwe cha Compact ufurahie mechi hii bila kukosa!

Piga *150*53# kulipia mapema kifurushi chako!

#MsimuwaSokaLaKibabe

BENKI YA CRDB YAANDAA FUTARI KWA WATEJA WAKE

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (katikati) akiwa ameambatana na Kaimu Sheikh wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, wakiongozana na Mwenyeji wako, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakati walipowasili kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 1,000.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (wa tano kulia) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kulia) wakikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa watoto wawakilishi wa moja ya kituo cha kuwalea watoto yatima, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Kaimu Sheikh wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Baraq, Rashid Rashid akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.


DR. MPANGO KICK-STARTS NMB SUSTAINABILITY PROJECT TO PLANT 1 MILLION TREES

In the spirit of sustainable development and in support of the global cause to conserve the environment, NMB Bank has embarked on a grand afforestation project to boost the decreasing stock of trees in the country.


The nationwide green crusade, which was launched in Dodoma by Dr. Philip Mpango, targets to plant one million trees this year as part of advancing the bank’s sustainability agenda.


Vice President Mpango kick-started the ambitious venture by gracing planting of 3,000 tree seedlings in the Mtumba Government City suburb, where he said afforestation and reforestation undertakings have now become inevitable and indispensable.


According to him, the NMB environment conservation initiative adds significant value to national and worldwide efforts to preserve the natural world and reverse climate change.

BENKI YA DUNIA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUTEKELEZA PPP

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru akiongoza kikao kati ya Serikali na ujumbe wa Benki ya Dunia (WB), cha kujadili namna bora ya utekelezaji wa PPP sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru akizungumza katika kikao kati ya Serikali na Benki ya Dunia (WB), cha kujadili namna bora ya utekelezaji wa sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) pamoja na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete, akizungumza katika kikao kati ya Serikali na Benki ya Dunia (WB), cha kujadili namna bora ya utekelezaji wa mpango wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), pamoja na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete baada ya kikao kati ya Serikali na Benki ya Dunia (WB), kilichojadili namna bora ya utekelezaji wa mpango wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), pamoja na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, jijini Dodoma.

Kikao kati ya Serikali na Benki ya Dunia (WB), cha kujadili namna bora ya utekelezaji wa PPP pamoja na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, kilichofanyika jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru akimsikiliza Bi. Atal Agarwal kutoka Benki ya Dunia wakati wa kikao kati ya Serikali na Benki ya Dunia (WB), kilichojadili namna bora ya utekelezaji wa Mpango wa Ubia kati ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), pamoja na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, jijini Dodoma.

Na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru amesema kuwa Serikali inafanya majadiliano ya kimkakati na Benki ya Dunia (WB) namna ya kuiwezesha sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia mpango wa ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, yaani PPP.

Alieleza hayo jijini Dodoma baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo, Bw. Nathan Belete, ambapo walijadili namna bora ya utekelezaji wa sheria ya PPP pamoja na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini.

Alisema majadiliano hayo ni utekelezaji wa msisitizo na maelekezo yanayotolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa sasa ni wakati wa Sekta Binafsi kushirikiana na Serikali kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kiuchumi.

ANNUAL MEETINGS OF THE BOARDS OF GOVERNORS OF THE AFRICAN DEVELOPMENT BANK GROUP, 22-26 MAY 2023


What: African Development Bank Group Annual Meetings

Who: The African Development Bank Group

When: 22 to 26 May 2023

Where: Sharm El Sheikh International Conference Center, Sharm El Sheikh, Egypt

The 58th Annual Meetings of the Board of Governors of the African Development Bank and the 49th Meetings of the Board of Governors of the African Development Fund will take place in Sharm El Sheikh, Egypt, from 22 to 26 May 2023. The African Development Fund is the concessional arm of the Bank Group,

The theme of the 2023 Annual Meetings is Mobilizing Private Sector Financing for Climate and Green Growth in Africa. It provides a framework for Bank Group Governors to share their experiences with galvanizing private financing domestically and internationally and harnessing natural capital to bridge the climate financing gap and promote the transition to green growth in Africa.

Particularly, the theme offers an opportunity for the Governors to discuss Africa's challenges in attracting private sector financing in low-carbon investments and practical policies that governments can deploy to address these bottlenecks.

The Annual Meetings of the African Development Bank Group comprise statutory meetings of its Governors (finance ministers or central bank governors representing the 81 member countries - and knowledge events. Attendees will include representatives of bilateral and multilateral development agencies, leading academics and non-governmental organizations, civil society, and the private sector.

The meetings are the Bank Group’s most important event annually, attracting around 3,000 participants. They allow the organization to take stock of progress with its shareholders.

Interested journalists are invited to send a press card and an appointment letter from their media organization to media@afdb.org(link sends e-mail) to get the reference code for online registration.

Deadline for registration: 10 April 2023 at 00:00 GMT.

Please visit the Annual Meetings website for more information: https://am.afdb.org/en

Tuesday, 28 March 2023

DKT. MWIGULU NCHEMBA ANA KWA ANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU WA AUSTRIA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa 10 wa Austria, Dkt. Alfred Gusenbauer, aliyeongoza ujumbe wa wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya ujenzi wa makazi ya kisasa ya gharama nafuu, kilimo na miundombinu ya bandari, Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wa nne kulia, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa wawekezaji kutoa Austria na Ujerumani, ukiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kumi wa Austria, Dkt. Alfred Gusenbauer, wa tatu kulia, wanataka kuwekeza kwenye sekta ya ujenzi wa nyumba/majengo kwa gharama nafuu kwa kutumia teknolojia ya kisasa, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu wa 10 wa Austria, Dkt. Alfred Gusenbauer, akisisitiza jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na wawekezaji kutoka Austria na Ujerumani, wanaotaka kuwekeza katika sekta ya ujenzi wa makazi ya kisasa ya gharama nafuu, kilimo, misitu na miundombinu ya bandari, Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewahimiza wawekezaji kutoka Austria na Ujerumani, kuharakisha mchakato wa kuwekeza katika sekta ya ujenzi wa makazi ya kisasa na ya gharama nafuu ili kutatua changamoto ya makazi hususan kwenye taasisi za umma hapa nchini.

Dkt. Nchemba ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji kutoka Austria na ujerumani, ukiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa 10 wa Austria, Dkt. Alfred Gusenbauer, jijini Dar es Salaam.

Wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba zenye gharama nafuu zinazotumia teknolojia ya kisasa na rafiki kwa mazingira, sekta ya misitu, kilimo na kuwezesha upatikanaji wa mitambo inayotumika kupakia na kupakua mizigo bandarini.

Dkt. Nchemba, alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa makazi katika sekta za afya, elimu na makazi binafsi hivyo aliwahimiza wawekezaji hao kukamilisha majadiliano na wataalam wa sekta husika ili kama kutakuwa na maridhiano ya gharama nafuu kwa kuzingatia ubora wa makazi hayo, basi mradi huo uanze kutekelezwa.

NALA TO INVEST TSHS 2.3 BILLION AFTER GETTING BOT LICENSE

NALA's Founder and CEO, Benjamin Fernandes (centre) displays the payment service provider (PSP) license from the Bank of Tanzania.

NALA, a Tanzanian money transfer fintech startup, said on Monday it plans to invest 1.0 million US dollars (2.3bn/-) after getting a payment service provider (PSP) license from the central bank.

The license approval will enable the fintech startup to make a direct integration with banks and local mobile money operators such Vodacom, Airtel, Tigo and the like.



NALA's Founder and CEO, Benjamin Fernandes, said the fintech biggest goal is enabling direct integration to banks and telcos and tackling the challenges that businesses face in money transfer across borders at affordable rates.

“The PSP license is a major milestone to us and we are making a major commitment to investing 1.0 million US dollars to build our most ambitious projects ever in our home market Tanzania,” Mr Fernandes said in a press conference.



NALA is an African payments company and money transfer app that enables users to make secure and reliable payments from Europe, the UK and US to Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda and Ghana in seconds.

NALA KUWEKEZA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 2 BAADA YA KUPATA LESENI YA BOT

Mwanzilishi Na Mkurugenzi Wa Kampuni Ya NALA, Benjamin Fernandes (katikati) akionyesha leseni ya mtoa huduma kwa malipo kutoka Benki Kuu ya Tanzania mara baada ya kukabidhiwa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Hoteli ya Hyatt Jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Meneja Bidhaa Thomas Robinson na kushoto ni Mtaalamu wa Progamu Bertha Sanga.

Mtaalamu wa Progamu, Bertha Sanga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa leseni ya mtoa huduma kwa malipo kutoka Benki Kuu ya Tanzania. 

 

Dar es Salaam Machi 27, 2023: NALA, kampuni ya Kitanzania inayowezesha huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya kidigitali sehemu mbali mbali duniani, imepata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na kuahidi kuwekeza Dola za Kimarekani milinio moja, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2. Leseni ya BOT inaifanya NALA kuwa mtoa huduma ya malipo na kuwezesha muunganiko wa moja kwa moja na benki pamoja na waendeshaji wa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu za mkononi, kama vile Mpesa, Tigopesa, Airtel Money na nyinginezo. 

Akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NALA Benjamin Fernandes alisema uwekezaji huo utaifanya NALA kuboreha huduma na kuongeza wigo wa huduma zake huku wateja wengi zaidi wakinufaika. Fernandes alisema hiyo itaiwezesha NALA kuanza kutengeneza bidhaa za ziada za kidijitali ambazo zitaongeza ujumuishaji wa malipo, kufanya huduma za malipo ziwe nafuu zaidi na za kuaminika kwa biashara na matumizi ya kawaida. 

ABSA BANK BIDS FAREWELL TO ITS MANAGING DIRECTOR DURING A SPECIAL IFTAR GALA

Outgoing Managing Director of Absa Bank Tanzania, Abdi Mohamed (centre) receives a prize from the bank’s Finance Director (CFO), Obedi Laiser, during a special Iftar party organized by the bank for its employees to spice the Holy Month of Ramadhan in Dar es Salam over the weekend. Left is the Director of Human Resources of Absa Bank Tanzania, Patrick Foya.

Outgoing Managing Director of Absa Bank Tanzania, Abdi Mohamed (left), serves Iftar dish to the Director of the Human Resources of the bank, Parick Foya, during a special iftar gala organized by the bank for its employees during the Holy Month of Ramadhan, an event that doubled as farewell platform for Abdi. The event took place in Dar es Salaam over the weekend. Third left is Absa’s Chief Internal Auditor, George Binde, and the Head of Business Banking, Melvin Saprapasen.

The outgoing Managing Director of Absa bank Tanzania, Abdi Mohamed (second left), enjoys the company of the Head of the Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga (left), during a special Iftar dinner organized by the bank for its workers, in Dar es Salam over the weekend.

Head of the Business Banking of Absa Bank Tanzania (Melvin Saprapasen (left), Chief Operating Officer of the bank, Oscar Mwamfwagasi, and the Director of Corporate and Investment Banking, Hugo Chilufya, serve food during a special Iftar organised by the bank for its employees and also to bid farewell to out-going Managing Director, Abdi Mohamed in Dar es Salaam over the weekend.

A cross- section of Absa Bank Tanzania employees enjoy their meal during an Iftar gala organized by the bank, in Dar es Salaam over the weekend. The function doubled as farewell for out-going Managing Director, Abdi Mohamed.

Some Absa Bank Tanzania workers enjoy their meal during a special Iftar party organized by the bank in Dar es Salaam over the weekend. The function doubled as farewell for out-going Managing Director, Abdi Mohamed.