Akizungumza katika hafla hiyo mjini hapa, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi amesema benki hiyo imekabidhi meza 100 na viti 100 kwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Manispaa ya Morogoro wakati shule ya msingi Sinyaulime iliyopo kata ya Ngerengere ikikabidhiwa vifaa vya ujenzi.
Mlozi amesema benki ya imekuwa na utamaduni wa kutoa misaada kunatokana na faida wanayopata kila Mwaka na asilimia moja ya faida hiyo kuipeleka kwenye huduma za kijamii.
Mlozi amesema kuwa benki ya NMB imekuwa ikisapoti serikali katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii ikiwemo sekta ya elimu, afya kwa kutoa vifaa na majanga yanapojitokeza ikiwemo kimbunga, matetemeko ya ardhi na mafuriko yanayowakumba wananchi.
Mkuu wa chuo hicho, Dismas Mguba alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto za uhaba wa vitanda kwa wanafunzi wa bweni na kuomba wadau wengine kuiga mfano wa benki ya NMB kusapoti kusaidia vitanda.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Sinyaulime, Rahabu Kisunga amtoa shukrani kwa uongozi wa NMB kutokana na msaada wa vifaa vya ujenzi, bati, kenchi na misumari kwa ajili ya kupaua ambavyo vitasaidia kumalizia ujenzi wa chumba kimoja cha darasa la pili na la tatu ambavyo wayoyo husongamana kwenye chumba kimoja wakati wa masomo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebeka Nsemwa ametoa wito kwa jamii kutunza vifaa na misaada iliyotolewa na na benki hoyo ili viweze kudumu kwa kipindi kirefu kwa masilahi ya vizazi vya sasa na vya baadae.
No comments:
Post a Comment