Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 28 March 2023

NALA KUWEKEZA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 2 BAADA YA KUPATA LESENI YA BOT

Mwanzilishi Na Mkurugenzi Wa Kampuni Ya NALA, Benjamin Fernandes (katikati) akionyesha leseni ya mtoa huduma kwa malipo kutoka Benki Kuu ya Tanzania mara baada ya kukabidhiwa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Hoteli ya Hyatt Jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Meneja Bidhaa Thomas Robinson na kushoto ni Mtaalamu wa Progamu Bertha Sanga.

Mtaalamu wa Progamu, Bertha Sanga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa leseni ya mtoa huduma kwa malipo kutoka Benki Kuu ya Tanzania. 

 

Dar es Salaam Machi 27, 2023: NALA, kampuni ya Kitanzania inayowezesha huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya kidigitali sehemu mbali mbali duniani, imepata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na kuahidi kuwekeza Dola za Kimarekani milinio moja, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2. Leseni ya BOT inaifanya NALA kuwa mtoa huduma ya malipo na kuwezesha muunganiko wa moja kwa moja na benki pamoja na waendeshaji wa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu za mkononi, kama vile Mpesa, Tigopesa, Airtel Money na nyinginezo. 

Akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NALA Benjamin Fernandes alisema uwekezaji huo utaifanya NALA kuboreha huduma na kuongeza wigo wa huduma zake huku wateja wengi zaidi wakinufaika. Fernandes alisema hiyo itaiwezesha NALA kuanza kutengeneza bidhaa za ziada za kidijitali ambazo zitaongeza ujumuishaji wa malipo, kufanya huduma za malipo ziwe nafuu zaidi na za kuaminika kwa biashara na matumizi ya kawaida. 

“Kwa kutumia NALA wateja wanaweza kutuma na kupokea fedha kwa nia ya kijigitali kutoka nchi mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na Marekani, Uingereza, nchi za Jumuiya ya Ulaya na nginginezo,” alifafanua.


Mkurugenzi huyo aliafafanua kuwa mara baada ya NALA kuzinduliwa katika Umoja wa Ulaya, kampuni hiyo imepokea leseni yake ya mtoa huduma za malipo nchini Tanzania na kuongeza kuwa hiyo ni hatua kubwa kwa kuwa inatoa nafasi ya kuboresha huduma na kuongeza huduma mpya, kama vile; malipo ya kibiashara, huduma za wafanyabiashara na malipo ya nje kutoka Tanzania, pamoja na ushirikiano wa moja kwa moja na benki za ndani na kampuni za mawasiliano. 

Leseni hii imetolewa, ikiwa ni muendelezo wa juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwainua vijana, lakini pia kuweka mazingira rafiki ya kiuwekezaji kwa ujumla, ili makampuni mengi kama NALA yaweze kuwekeza nchini. Fernandes alisema “Malengo mawili makubwa ya NALA kutokea mwaka jana yamekuwa kuwezesha ushirikiano wa moja kwa moja kwa benki na kampuni za mawasiliano ya simu, kukabiliana na changamoto ambazo wafanyabiashara wanakabiliana nazo katika kuhamisha fedha kuvuka mipaka ya nchi. 

Tumefanya kazi kwa karibu pamoja na Benki Kuu ya Tanzania ili kukamilisha hatua zinazofaa za kupokea leseni yetu kama mtoa huduma wa malipo. Kwa leseni hii mpya mkononi, NALA inapata nafasi na uwezo wa kuendelea na malengo yetu, kubwa likiwa kufanya uwekezaji wenye thamani ya zaidi ya Bilion 2 za kitanzania ili kujenga miradi yetu mikubwa zaidi kuwahi kutokea katika soko letu la hapa nyumbani Tanzania” NALA inapatikana nchi nyingi za Ukanda wa Afrika na Ulaya, unaweza kuipakua kwenye simu yako kupitia App Store au Play Store. 

Licha ya chaguzi nyingi za kutuma pesa Afrika kutoka ng'ambo, bara hili bado limeendelea kuwa mahali pa gharama kubwa zaidi kutuma pesa. Benki ya Dunia inakadiria wastani wa ada za kutuma fedha Afrika kuwa 9%. Zaidi ya hayo, chaguo nyingi zilizopo ni pamoja na ada zilizofichwa ambazo hufanya iwe vigumu kutambua gharama halisi ya kutuma pesa. NALA inajitahidi kubadilisha dhana ya zana za kifedha kwa Waafrika kwa kutoa huduma za haki na uwazi ili kuwawezesha watu kudhibiti fedha zao. Kuhusu NALA: NALA ni kampuni ya malipo ya Kiafrika na programu ya kutuma pesa ambayo hukuwezesha kufanya malipo salama na ya kuaminika kutoka Ulaya, Uingereza na Marekani hadi Afrika kwa sekunde chache. 

Kampuni hiyo ina dhamira ya kuongeza fursa za kiuchumi katika bara la Afrika na miongoni mwa wanadiaspora duniani kote. Kuunda masuluhisho ya kifedha yanayoendeshwa na jumuiya, hurahisisha kufanya malipo ya kila siku na kuongeza fursa za biashara katika Afrika inayokua duniani. 

Malipo barani Afrika yamejengwa kwa 1%. NALA inatamani kuleta teknolojia ya malipo ya karne ya 21 barani Afrika ili kuunda njia za malipo za gharama ya chini na zinazotegemeka sana ambazo marafiki, familia na wafanyabiashara wanaweza kutumia. Ikiwa malipo ni rahisi, ya kuaminika, na yanapatikana kwa kugusa kitufe, chochote kinawezekana. 


Kwa kujenga njia za malipo na miundombinu, NALA itawezesha malipo ya haraka kwa bara la Afrika. Teknolojia yao imeundwa na wahandisi wa kiwango cha kimataifa kutoka duniani kote na tunajivunia kuhudumia jumuiya zote, kuanzia miji yenye shughuli nyingi hadi vijiji vyenye amani. Tumebahatika kushirikiana na jumuiya hizi katika safari hii pamoja.

     

No comments:

Post a Comment