Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema sekta ya fedha ina mchango mkubwa katika ukuaji na maendeleo ya uchumi, kujenga uchumi jumuishi na kupunguza umasikini ndio maana Serikali nyingi duniani kote zinatilia mkazo suala la ujumuishi wa kifedha (financial inclusion).
Pamoja na juhudi hizo, Waziri Nnauye alisema bado idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za benki ni ndogo akikumbusha utafiti wa kwanza wa Finscope wa mwaka 2006 ulioonyesha kuwa ni asilimia 46 tu ya watu wazima walijumuishwa kifedha, ambapo asilimia 11 tu walikuwa wakitumia huduma rasmi za kifedha.
Sababu kuu za watu wengi kuwa nje ya mfumo wa fedha, alisema ni ufikiwaji mdogo wa huduma za benki kupitia matawi katika maeneo ya vijijini na gharama kubwa za ufikiaji wa huduma za kifedha ikiwemo hitaji la kusafiri umbali mrefu katika maeneo yenye matawi ya benki kwani nyingi zilikuwa maeneo ya mkoani au wilayani.
Kwa kutambua mchango wa teknolojia kutatua changamoto hiyo, alisema Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Februari 2013 ilitoa Mwongozo wa Huduma za benki kupitia wakala na leo hii Benki ya CRDB ina zaidi ya mawakala 25,000 ambao ni sawa na asilimia 46 ya mawakala wote 55,000 wa benki waliopo nchini wanaofanikisha zaidi ya miamala milioni 100 yenye thamani ya shilingi trilioni 50 zikiwamo shilingi trilioni 1.3 za mapato ya Serikali.

"Mfumo wa CRDB Wakala umekua na mchango mkubwa katika ufikishaji wa huduma za fedha kwa wananchi, taarifa zetu za utendaji zinaonyesha zaidi ya miamala milioni 100 yenye thamani ya shilingi Trilioni 50 imekua ikifanyika kupitia CRDB Wakala kwa Mwaka, mfumo huu pia umekua ukisaidia katika ukusanyaji wa mapato ya serikali ambapo takribani Trilioni 1.3 hukusanywa kwa mwaka," alisema Nsekela.
Aidha, Nsekela alifafanua kwamba mfumo huo wa CRDB Wakala unatoa huduma za fedha kwa watanzania milioni 3 kwa mwezi ambapo asilimia 40 ni wateja wa Benki na asilimia 60 ni wananchi wengine.
Mfumo wa CRDB Wakala, alisema umetoa zaidi ya ajira 35,000 kwa vijana wanaopokea kamisheni kwa miamala wanayoifanya.
CRDB Wakala App ni mfumo mpya wa kisasa, salama na wa kidijitali unaotumika kwenye simu janja kutoa huduma za kibenki kwa ufanisi wa hali ya juu hivyo kuongeza ufanisi, kasi ya utoaji huduma na kupunguza gharama za uendeshaji kwa watoa huduma hasa kwa mawakala wa Benki.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akibonyeza sehemu yenye ujumbe wa Ubora wakati wa uzinduzi rasmi wa mfumo mpya na wakisasa utakaowawezeza mawakala wa benki ya CRDB kutoa huduma kwa urahisi zaidi kupitia simu janja zao, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam, Novemba 15, 2022. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo (watatu kushoto), Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda.
No comments:
Post a Comment