Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 30 November 2022

HAKUNA MGAO UKIWA NA DStv APP. MECHI ZOTE 64 LIVE KIGANJANI MWAKO


Usichaguliwe mechi ya kutazama kwenye michuano ya World Cup! @dstvtanzania ndio suluhisho

Lipia kifurushi cha Compact kwa kupiga *150*53# ufurahie mtanange wa Poland dhidi ya Argentina Jumatano hii!

Mgao unasumbua?

Pakua DStv App ufurahie mechi zote popote ulipo!

#HiiNiKwaKilaShabiki

Tuesday, 29 November 2022

WASHINDI WA SHINDANO LA KAMPENI YA TISHA NA TEMBOACARD WATINGA QATAR KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA


Benki ya CRDB baada ya kuhitimisha awamu ya kwanza ya kampeni yake ya “Tisha na TemboCard” na kuwakabidhi tiketi za kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia wateja wake watatu walioibuka washindi wa jumla wa kampeni hiyo hatimae yawapeleka Qatar.

Wateja hao waliondoka tarehe 25 kupitia uwanja wa Julius Nyerere International Airport na kusindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo.

 

Akizungumza kwa niaba ya washindi wenzake katika safari hiyo, Rajabu Dossa Mfinanga aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwapa kipaumbele wateja wake kwani wanajihisi ni sehemu ya familia ya Benki hiyo, pia alitoa rai kwa watanzania kujijengea utamaduni wa kutumia kadi zao za benki hiyo kwa kuafanya manunuzi na malipo mbalimbali kama bili, usafiri na kadhalika si kwasababu ya kushinda zawadi;

“Niwape wito wateja wenzangu wa Benki ya CRDB na watanzania kwa ujumla tujenge utamaduni wa kutumia kadi kupata huduma mbalimbali badala ya kutumia fedha taslimu. Matumizi ya kadi ni rahisi na inakupa kujiamini zaidi kuliko ukibeba fedha taslimu, unakosa kujiamini kila uendapo unakuwa na wasiwasi kwa kuhofia kuibiwa, lakini ukiwa na Tembocard yako mambo ni burdani”. Aliongeza Mfinanga.
 

Kwa kufahamu namna ambavyo Watanzania wanapenda michezo na hasa msimu huu wa Kombe la Dunia imeona ni vyema ikawa sehemu ya kutimiza shauku ya wateja wao ya kushiriki katika mashindano hayo makubwa duniani.

Katika safari hiyo Benki ya CRDB imewagharamia tiketi za ndege kuelekea Doha Qatar, malazi, pamoja na fedha za matumizi wakiwa huko.

 

Washindi walioibuka kidedea kwenye safari hiyo ya kushuhudia kombe la dunia ni pamoja na; Haji Athumani Msangi, Erick Boniface Kashangaki, Kelvin Jackson Twissa na Rajabu Dossa Mfinanga wote wakazi wa Dar es Salaam.

Benki ya CRDB inatarajia kuendesha awamu ya pili ya kampeni hii na kuahidi kuleta mambo mazuri zaidi, hivyo imetoa rai kwa wateja wake kuendelea kutumia kadi zao za TemboCard kulipia manunuzi ili kupata punguzo la bei (discount) au kurudishiwa sehemu ya kiasi walichotumia (cashback) katika maduka mbalimbali.

NMB YAZIPIGA JEKI SHULE ZA KILOSA NA MVOMERO

Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (kulia) akimkabidhi moja ya madawati 50, Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Mvomero, Bruno Sangwe wakati benki hiyo ilipotoa msaada wa vifaa vya elimu kwa shule za msingi na sekondari nne zenye thamani ya Shilingi Milioni 25 katika hafla iliyofanyika shule ya msingi Madizini Turiani, Mkoani Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Madizini, Darini Nassoro.

Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya elimu katika shule tano za halmashauri ya wilaya ya Kilosa na Mvomero vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 35 ikiwa sehemu ya kupunguza changamoto za elimu mkoani Morogoro.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mabati, mbao, misumari na madawati kwa shule za sekondari Murrad Sadiq Sekondari, Mziha Sekondari huku kwa shule za msingi ni Madizini, Mlali, Matongolo na Mkwatani.

Wakizungumza wakati wa hafla iliyofanyika katika shule hizo kwa nyakati tofauti, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Matongolo wilaya ya Kilosa, Sifa Jonas alisema shule hiyo imepokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya Sh.Mil 5 ambayo yatasaidia tatizo la wanafunzi kukaa chini wakati wa masomo yao ya kila siku.

Sifa alisema shule ya msingi Matongolo ina jumla ya wanafunzi 2379 wavulana wakiwa 1155 na wasichana 1224 huku kukiwa na madawati 236 huku kukiwa kukihitajika madawati 557.

BENKI YA CRDB YATWAA TUZO TATU ZA TOP 100 EXECUTIVE

 
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Omar Shaaban (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendanji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela tuzo ya Mkurugenzi Mtendaji (CEO/MD) Bora wa Mwaka 2022 Tanzania katika tuzo za Top 100 Executive zilizofanyika tarehe 27 Novemba 2022 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam. Wengine katika picha ni kutoka Tanzania Instute of Managers ambao ni Mwanzilishi mwenza (Co–founder) Deo John (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji, Alex Shayo (kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Frederick Nshekanabo (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa Benki hiyo, Jesca Njau wakiwa na tuzo zao walizoshinda katika usiku wa tuzo za Top 100 Executive zilizofanyika tarehe 27 Novemba 2022 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Frederick Nshekanabo (wa nne kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa Benki hiyo, Jesca Njau (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wengine wa benki hiyo usiku wa tuzo za Top 100 Executive zilizofanyika tarehe 27 Novemba 2022 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam.
Furaha baada ya ushindi.
Wadau.

UZA, INALIPA! E-COMMERCE COMPANY LAUNCHES PRODUCT TO BOOST YOUTH ENTREPRENEURSHIP

Product Manager Bertha Shao and Host Millard Ayo speaking to the press.
CEO Hafiz Juma speaking to invited guests.
Product Manager Bertha Shao clarifies how uza works.

inalipa (https://www.inalipainc.com) has launched a new innovative product that promises to be a much needed tool to reduce youth unemployment.

inalipa is a prominent e-commerce company based in Tanzania that has gained accolades across Africa for its mission to build a new route to market for consumer FMCG goods in Africa. inalipa is one of the few Tanzanian companies to attract international investment from renowned venture capital firms backing the most promising technology businesses.

Host Frederick Bundala speaking with the press.

The core vision of inalipa is to see an Africa where large consumer goods brands can easily access and supply the market, get valuable data and insight and have better visibility of their customers.



inalipa believes that MSMEs, small retailers and Dukas are critical stakeholders in the development of the retail sector.

Today, inalipa launched uza, a novel sales app that allows anyone to register and be their own boss by selling consumer goods in wholesale. uza is an exciting product which provides instant rewards to its users, has a competitive leaderboard for sellers to earn prizes and more.

TANZANIA INSTITUTE OF MANAGERS LAUNCHES TOP 100 EXECUTIVE LIST, SECOND EDITION

Abdulmajid Nsekela, the Managing Director of CRDB Bank, was ultimately named this year's CEO of the Year during the Top 100 Executive List held in Dar es Salaam over the weekend. The award was handed over by the Minister of Trade, Zanzibar - Hon. Omar Shabaan, (second left). Extreme left is Deo Kilawe, the Founder and CEO of Tanzania Institute of Managers. Extreme right is Alex Shayo, Director of the Tanzania Institute of Managers.
Abdulmajid Nsekela, the Managing Director of CRDB Bank speaks after having been awarded his best CEO of year trophy.
Deo Kilawe, CEO and Founder of Tanzania Institute of Managers makes his opening speech during the Top 100 Executive list event held over the weekend in Dar es Salaam.
Jesca Njau, Head of Procurement at CRDB Bank at the Top 100 Executive List event held over the weekend.
Abdulmajid Nsekela, the Managing Director of CRDB stands with all of the winners at the Top 100 Executive List that was held at Mlimani City over the weekend.

Key Highlights;
  • Top 100 Executive List audited by recognized auditing firm, KPMG 
  • TIM recognizes excellence and leadership
  • The VISA USD Debit Card allows customers to make purchases in USD without incurring extra charges 
  • The event has attracted over 400 guests this year
DAR ES SALAAM, 27th Dec 2022 - Tanzania Institute of Managers, a training institute launched Top 100 Executive List 2022 over the weekend. Top 100 Executive List this year celebrates excellence and leadership in Tanzania. The Tanzania Top 100 Executive List 2022 is organized by the Tanzanian Institute of Managers. The institute recognizes that good management is the single most influential factor in the success of any enterprise.

The Top 100 Executive List was established last year and is now a yearly celebration of the individual and collective successes of Tanzania's trailblazing business leaders.

The Founder and Chairman of Eastern Star Consulting Group, Deogratius Kalawe said “We decided to recognize excellence this year after last year's celebration of corporate executives' performances. As a country, we think it's important to set an example for other managers and executives in terms of what excellence looks like. Integrity and excellence need to be encouraged in our businesses. We think we are laying the groundwork for the development of managers and executives who operate with integrity and value their reputations and careers through the programs we provide at the Tanzania Institute of Managers (TIM).”

NETHERLANDS VS QATAR LEO NDANI YA DStv PEKEE


Hapa Netherlands hapa Qatar Jumanne hii kwenye michuano ya World Cup! Furahia mechi Zoooooote na sio za kuchaguliwa kuona!

Matokeo yatakuaje?

Lipia mapema kifurushi chako cha Compact usipitwe na mechi hii Live ndani ya @dstvtanzania pekee.

Mgao usikustress, DStv App ipo kwa ajili yako!

#HiiNiKwaKilaShabiki

SHINDA SAFARI YA DUBAI UKITUMIA NMB MASTERCARD AU LIPA MKONONI (MASTERCARD QR) KUFANYA MALIPO

 

Ni msimu wa kukwea pipa✈️! Matumizi yako ya NMB mastercard au Lipa Mkononi (mastercard QR), ndio yatakayokuhakikishia nafasi ya kushinda safari ya kwenda Dubai kwa siku nne pamoja na mwenza wako.

#NMBKaribuYako 
#MastaBataKoteKote

Monday, 28 November 2022

SERENGETI BREWERIES - GUINNESS BRAND INSPIRES ARTS AND CREATIVITY AMONG TANZANIANS

Serengeti Breweries Limited (SBL) Sales Director Chris Gitao (left), congrats painters Alfred Onyango and Sharlene Gapare for winning the Guinness Brews and Brushes painting competition held at Fuego Lounge in Dar es Salaam on Saturday. Extreme left is competition judge Arafa Hamadi.
A group of painters engaged in the painting competition organized by Guinness to spark interest in arts and creativity during the event last Saturday.
Serengeti Breweries Limited (SBL) Sales Director Chris Gitao (left), congratulates painter, Tracy Humplick (centre) for her excellent painting skills. On the right is competition judge, Arafa Hamadi. The competition took place on Saturday 26 November 2022.
Serengeti Breweries Limited (SBL) Sales Director, Chris Gitao, congratulates painter, Rispa Hatibu who is also SBL’s Communication Manager, engaged in the competition to show support for other painters attending the event last Saturday.

Dar es Salaam, 26 November 2022 - Tanzania's second leading brewer, Serengeti Breweries Limited (SBL) and Dar es Salaam residents jointly ushered a bespoke arts and creativity event dubbed “Guinness Brews and Brushes” inspiring local painting talents via executing a freestyle painting competition. The event occurred at Fuego Lounge in Dar es Salaam on Saturday evening.

Guinness is yet another thrilling SBL brand that inspires the best out of consumers. Thus the Brews and Brushes bespoke event was a direct call to realizing the latter. The freestyle painting competition called for any participant, special guest and all invitees to engage in painting tasks and showcase their inner talents, with no rules applied.

The event drew several interesting figures in the arts and creativity arena, such as Hamis Mandi “BDOZEN”, a radio/Tv personality and young aspiring talents in the painting arena.

Irene Jeremiah, an aspiring young painter, commended SBL’s commitment to supporting artistic expressions with a creative event.

WOMEN IN MINING: HOW GEITA GOLD MINING LTD. ELEVATES WOMEN IN THE MINING INDUSTRY AND CONTINUES TO SUPPORT THEM

Josephine Kimambo and Shadya Jamal in their daily work routines.
Josephine Kimambo Senior Officer in the Health, Safety, Environment and Training (HSE&T) Department.
Engineer Ruth Mugurusi from the Drilling and Blasting Department at the 5th National Mining Technology Exhibition.
Engineer Ruth Mugurusi from the Drilling and Blasting Department briefs the guest of honour at the opening ceremony of the 5th National Mining Technology Exhibition, Minister of Minerals Dr. Dotto Biteko (right), who visited the GGML exhibition stand. Extreme left is AngloGold Ashanti’s Vice President of Sustainability for Tanzania and Ghana, Simon Shayo.

The struggle for gender equality is ongoing, although in recent years there has been a closer parity in the opportunities that are afforded to women compared to their male counterparts. There is still some way to go, however. Young girls today begin life’s journey with lofty dreams, but most often, culture extinguishes these flames of optimism, compelling women to stick to the traditional roles of homemaker and mother. Consequently, this chips away at a young woman's self-belief, with most not knowing their true worth.

Today, attitudes and practices are changing, and gender is not seen as the obstacle it once was, preventing women from pursuing their dreams. The key drivers of success today are aptitude, commitment, hard work, dedication, and a “can do” attitude.

Josephine Kimambo and Shadya Jamali are among the few women in the mining industry, forming part of Geita Gold Mining Limited’s Health, Safety, Environment, and Training (HSE&T) Department. They both live by the mantra that “an ordinary life in an extraordinary world is boring and unfulfilled.” Believing that everyone is unique and can leave a legacy has proved from their perspective that gender is not a barrier as long as they know the purpose of their existence.

RAIS WA BURUNDI AIPONGEZA BENKI YA CRDB

Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye akiwa kwenye mazungumzo na ujumbe wa Benki ya CRDB, ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Dkt. Ally Laay na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati walipomtembelea kwenye makazi rasmi yaliyopo eneo la Kiriri, Bujumbura, Novemba 25, 2022. Mkutano huo ilikuwa ni sehemu ya muendelezo wa maadhimisho ya miaka 10 ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi, ambayo kilele chake kilifanyika mwishoni mwa wiki.

Bujumbura, Burundi - Ikitarajia kufungua tawi la tano mapema mwakani itakapofikisha miaka 11 ya kutoa huduma za fedha nchini Burundi, Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye ameipongeza Benki ya CRDB kwa huduma bora ilizozitoa kwa muongo mmoja sasa.

Benki hiyo iliyoingia nchini Burundi mwaka 2012 ina matawi manne kwa sasa yanayotoa huduma pamoja na mawakala zaidi ya 600 wanaohakikisha wananchi na wafanyabiashara wanahudumiwa kwa wakati na mapato ya Serikali kukusanywa kwa utaratibu rahisi nchini humo.


Rais Ndayishimiye ametoa pongeza hizo alipozungumza na menejimenti ya Benki ya CRDB iliyoongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wake, Abdulmajid Nsekela aliyeambatana na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi kusherehekea miaka 10 ya kutoa huduma nchini humo.

“Burundi tumeipokea Benki ya CRDB kwa mikono miwili na tunajivunia uwepo wake. Tanzania na Burundi ni ndugu wa karibu, hata mipaka iliyopo ni matokeo ya ukoloni lakini haiwezi kuwa kikwazo cha mahusiano mazuri yenye historia kubwa ya ushirikiano. Tunashukuru kuwa Tanzania ilishiriki kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa amani Burundi na sasa mnakuja tufanye maendeleo kwa pamoja kwa manufaa ya nchi zetu,” alisema Rais Ndayishimiye.

Katika kipindi hicho cha kutoa huduma nchini Burundi, Benki ya CRDB imefanya vyema sokoni hadi kushika nafasi ya tatu kwa kupata faida kubwa kati ya benki 13 zilizopo. Mpaka Septemba mwaka huu, benki hiyo ilikuwa imetoa mikopo kiasi cha faranga 300 bilioni (Sh338 bilioni).

Mwaka 2019 Serikali ya Burundi iliyahamisha makao makuu yake kutoka Bujumbura kwenda jiji la Gitega hivyo Benki ya CRDB inatarajia kufungua tawi jipya huko ili kuihudumia pamoja na wafanyakazi wake, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida. Tawi hilo litafunguliwa mapema mwakani.

 

“Tunawashuru sana kwa jitihada zenu za kutoa elimu ya fedha kwa Warundi ili wajifunze namna nzuri ya usimamizi wa fedha na kuwekeza. Tungependa kushirikiana nanyi zaidi katika programu za vijana na wanawake ambao ni kipaumbele chetu kikubwa kwa sasa,” alisema Rais Ndayishimiye.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa CRDB, Nsekela alisema Serikali ya Burundi inawapa ushirikiano mkubwa unaowasaidia kupata mafanikio ndani ya miaka 10. Serikali imeipa benki hiyo eneo la kujenga ofisi katika Jiji la Gitega.

“Benki ya CRDB itaendelea kuunga mkono jitihada za kukuza uchumi wa Burundi kwa manufaa ya Warundi, Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla. Tunatarajia kuingia DRC (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) hivi karibuni na tutafungua matawi katika mikoa iliyo karibu na mpaka wa Burundi na DRC ili kuchochea biashara kati ya nchi hizo mbili,” alisema Nsekela.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB, Dk. Ally Laay alisema haikuwa rahisi kuridhia uamuzi wa kufungua biashara nchini Burundi kwa kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kutoa huduma nje ya nchi.

“Maswali yalikuwa mengi juu ya kuichagua Burundi lakini leo hii sote tunajivunia na kuona nchi zote mbili zinanufaika. Hapa Burundi tunalipa kodi na kutoa ajira huku faida inayopatikana ikiwanufaisha wanahisa wetu hadi Tanzania,” alisema Dk. Laay.

Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye (katikati) akimpongeza Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kulia) wakati walipomtembelea kwenye makazi rasmi yaliyopo eneo la Kiriri, Bujumbura, Novemba 25, 2022. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Kahumbya Bashige.

Rais wa Jamhuri ya Burundi, Évariste Ndayishimiye akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, baada ya kumaliza mazungumzo yao walipomtembelea kwenye makazi yake rasmi yaliyopo eneo la Kiriri, Bujumbura, Novemba 25, 2022. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Hosea Kashimba (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Fredrick Siwale (wa pili kushoto), Afisa Mkuu wa Uwendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwille (kulia), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Kahumbya Bashige pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Menard Bucumi. Mkutano huo ulikuwa ni sehemu ya muendelezo wa maadhimisho ya miaka 10 ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi, ambayo kilele chake kilifanyika mwishoni mwa wiki.

BENKI YA NBC YAKABIDHI ZAWADI KWA KOCHA NA MCHEZAJI BORA MWEZI OKTOBA, YAAHIDI MAKUBWA ZAIDI

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya pesa yenye thamani ya Tsh milioni 1 pamoja na tuzo kwa kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alietangazwa kocha bora wa ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League kwa mwezi Oktoba wakati wa mechi kati ya Yanga SC na Mbeya City FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Mchezo huo ulikamilika kwa timu ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa sifuri.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya pesa yenye thamani ya Tsh milioni 1 pamoja na tuzo kwa mchezaji Sixtus Sabilo kutoka Mbeya City SC alietangazwa mchezaji bora wa ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League kwa mwezi Oktoba wakati wa mechi kati ya Yanga SC na Mbeya City FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Mchezo huo ulikamilika kwa timu ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa sifuri.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akikabidhi zawadi ya king’amuzi cha Azam kwa mchezaji Sixtus Sabilo kutoka Mbeya City SC alietangazwa mchezaji bora wa ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League kwa mwezi Oktoba wakati wa mechi kati ya Yanga SC na Mbeya City FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki hiyo, Elvis Ndunguru (katikati) wakiwa wameshikilia baadhi ya zawadi kwa ajili ya mchezaji bora pamoja na kocha bora wa Ligi ya NBC Premiere League kwa mwezi Octoba. Benki hiyo ndio mdhamini wa ligi hiyo ambayo hadi sasa imetoa ajira na kipato kwa watu zaidi ya 12,000.

Dar es Salaam: Novemba 26, 2022 - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League jana ilikabidhi zawadi ya pesa na tuzo kwa mchezaji bora wa ligi hiyo wa mwezi Oktoba, Sixtus Sabilo kutoka Mbeya City SC pamoja na kocha bora wa mwezi huo, Nasreddine Nabi kutoka klabu ya Yanga.

Makabidhiano ya zawadi hizo yalifanyika muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya Yanga SC dhidi ya Mbeya City FC uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, mchezo ambao ulikamilika kwa timu ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa sifuri. Magoli ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Fiston Mayele.

Katika tukio la makabidhiano ya zawadi hizo, ilishuhudiwa Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru akikabidhi mfano wa hundi ya pesa yenye thamani ya Tsh milioni 1 kwa kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi pamoja na tuzo sambamba na king’amuzi cha Azam huku pia mchezaji Sixtus Sabilo kutoka Mbeya City SC akipatiwa mfano wa hundi yenye kiasi kama hicho cha pesa, tuzo na kingamuzi cha Azam.

Friday, 25 November 2022

HAKUNA MGAO UKIWA NA DStv APP - MECHI ZOTE 64 LIVE KIGANJANI MWAKO

Katika mechi yao ya kwanza waliwakalisha Qatar, lakini je wanawez kuwa na nguvu ya kuwatikisa Netherlands?

Usiwaze kuhusu mgao, DStv App ipo hapa kwa ajili yako, pakua App ya DStv na ufurahie mechi hizi popote utakapokua.

#HiiNiKwaKilaShabiki

NMB YATOA ELIMU YA HUDUMA ZAO KWA WANANCHI WIKI YA HUDUMA YA KIFEDHA JIJINI MWANZA

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa NMB, Vicky Bishubo (kushoto), alipotembelea banda lao na kuelezwa kuhusu jitihada zao walizofanya kutoa Hati Fungani ya ‘Jasiri Bond’ ambapo jumla ya Shilingi bilioni 74.3 zilipatikana kwa ajili ya kuwawezesha akina mama wanaofanya shughuli za kiuchumi kwenye sekta ndogo na za kati hapa chini.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa NMB, Vicky Bishubo katika viwanja vya Rock City jijini Mwanza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Sophia Mjema (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa NMB, Vicky Bishubo, katika viwanja vya Rock City jijini Mwanza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wiki ya Huduma za Fedha kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), Tuse Joune (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa NMB, Vicky Bishubo jijini Mwanza wakati wa maonesho ya wiki ya Huduma za Fedha kitaifa.

Thursday, 24 November 2022

BENKI YA NBC YAUNGANA NA JUBILEE KUTUMIA MTANDAO WA MAWAKALA WA NBC KUUZA BIDHAA ZA BIMA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akizungumza na mawakala waliojitokeza kwenye uzinduzi wa mafunzo ya bima kwa mawakala, yanayotolewa na Benki ya NBC pamoja na Jubilee Alience Insurance kupitia Chuo cha Bima na Hifadhi ya Taifa(ACSID). Jumatatu 21 Novemba,2022, Posta-Dar-es-Salaam.  
  • Benki ya Jubilee Allianz zafanya semina ya siku nne kwa mawakala wa NBC kuwapa elimu ya bidhaa mbalimbali za bima 
  • Lengo ni kuunga mkono ajenda ya serikali ya huduma za kifedha jumuishi na kuweka huduma za kibenki karibu na wananchi
  • Benki ya NBC ina zaidi ya mawakala 8000 nchi nzima   
Dar es Salaam; Novemba 22, 2022 - Ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha utoaji wa huduma za bima nchini, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeshirikiana na Jubilee Allianz kutoa mafunzo kwa mawakala wa Benki hiyo (NBC Wakala) na kuwapatia vitendea kazi na maarifa ya huduma za bima katika lengo la kukuza mauzo. 

Mapema wiki hii, Benki kwa ushirikiano na washirika wa bima ya Jubilee Alliance General Insurance, ilianza mafunzo ya wiki tano kwa Wakala wa Benki hiyo ili kuwaelimisha na kuwapa taarifa za bidhaa. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, alisema benki hiyo inaunga mkono ajenda ya Serikali ya huduma za kifedha jumuishi kwa kuweka huduma za kibenki na bima karibu na wateja kupitia mtandao wa NBC Wakala. 

“Tanzania ina kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma za bima katika Afrika Mashariki, chini ya asilimia 1. Kwa mtandao mpana zaidi wa NBC Wakala zaidi ya elfu nane kote nchini, tuna uhakika wa kuwafikia watu wengi na kuwapa huduma hizi muhimu za bima. Tunatoa huduma mbalimbali za bima kwa magari, mali, na ustawi kupitia bima ya maisha na afya,” alisema Sabi.

 

Sabi pia alieleza kuwa mawakala hao sasa watatumia mfumo maalum uliotengenezwa na benki na washirika wake ili kurahisisha utoaji wa huduma za bima. "Mauzo yetu ya bima kupitia mawakala yatafanywa kupitia mfumo maalum uliotengenezwa na benki na washirika ili kufanya huduma hiyo iwe ya kipekee, na ya kirafiki na jumuishi," alibainisha.


Kwa upande wake, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, aliipongeza Benki ya NBC na Jubilee Allianz kwa kutekeleza wito wa Serikali wa kupanua wigo wa huduma na bidhaa za bima nchini. Dk Saqware alikumbusha kuwa Mei 2022, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango, ilitoa mwongozo unaoelekeza makampuni na watoa huduma za bima kusajili maafisa mauzo wa bidhaa za bima nchini. 

“Nimefurahi kuona kwamba Benki ya NBC imekuwa ya kwanza kuitikia azma hii, na kwa kushuhudia mafunzo haya, hakuna shaka kwamba kutakuwa na upatikanaji mzuri wa huduma ya bima nchini kote. Ninaipongeza NBC na Jubilee Allianz kwa kuongoza katika mpango huu, na ninatumai kuwa taasisi nyingi zaidi pia zitashiriki. Baada ya muda mfupi, Watanzania wengi watakuwa na upatikanaji rahisi wa huduma za bima,” alisema Dk. Saqware.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Jubilee Allianz, Bw. Dipankar Acharya, alisema, “Hii ni fursa ya kusisimua kwa mawakala na umma kupata bima ya afya kwa urahisi. Nimefurahishwa na ushiriki na maswali yanayoulizwa. Hii inaonyesha tumejipanga katika kutoa huduma bora za bima kote Tanzania.” 

Mawakala watafanya mafunzo na uhamasishaji wa kujiunga na bima zaidi kwa kufuata michakato inayoratibiwa na TIRA na mamlaka nyinginezo ili kuhakikisha kuwa huduma za haraka, zinazopatikana kwa urahisi na zinazofaa zinatolewa.