Benki ya CRDB kwa kushirikiana na kampuni ya Visa international leo imezindua kampeni ya “Tisha na TemboCard Visa” inayolenga kuhamasisha wateja kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao za TemboCardVisa huku wakijiwekea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwamo kushuhudia kombe la mataifa ya afrika AFCON litakalofanyika nchini Cameroon mwakani 2022.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Rabala alisema zawadi zitatolewa kwa wateja ambao watafanya miamala mingi zaidi kupitia TemboCardVisa zao katika kipindi chote cha kampeni ambayo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Machi 2022.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Rabala alisema zawadi zitatolewa kwa wateja ambao watafanya miamala mingi zaidi kupitia TemboCardVisa zao katika kipindi chote cha kampeni ambayo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Machi 2022.
Akielezea kuhusu zawadi zitakazotolewa katika kampeni hiyo, Raballa alisema wateja watapata zawadi mbalimbali ikiwamo kurudishiwa asilimia 5 ya kiasi walichotumia, kulipiwa bili ya malipo ya manunuzi, simu janja, tablet, televisheni, sofa set, home theatre, pamoja na safari ya kitalii kwenda Zanzibar au Serengeti. “Kubwa zaidi ni zawadi ya safari ya kwenda Cameroon kushuhudia michuano ya AFCON kwa wateja 4 ambao watakuwa na miamala mingi zaidi katika kipindi cha Desemba na Januari. Washindi wataruhusiswa kwenda na wenza au rafiki zao” alisema Rabala.
“Kwa wale ambao hawana akaunti niwashauri wafungue akaunti ili waweze kuunganishwa na TemboCardVisa na kuanza kufurahia huduma huku wakijiwekea nafasi ya kujishindia zawadi kemkem. Kama mnavyojua sasa hivi zoezi la kufungua akaunti tumelirahisisha sana…”
“…kama una simu janja unachotakiwa kufanya ni kupakua SimBanking App na kufuata hatua za kufungua akaunti kwa kutumia namba ya NIDA na kisha utaomba kupata TemboCard yako, kwa wale wa sio na simu janja wanaweza kutembelea kwa CRDB Wakala wakiwa na kitambulisho cha NIDA kufunguliwa akaunti na kupata TemboCardVisa kwa urahisi. Tunatamani kuona watu wengi zaidi wakishiriki ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo,” aliongezea.
Uzinduzi huo wa kampeni hiyo ya “Tisha na TemboCardVisa” ulienda sambamba na uzinduzi na muonekano mpya wa kadi za Benki ya CRDB ‘TemboCard’ ambazo zimeboreshwa zaidi ili kuwapa wateja uzoefu bora zaidi pindi watumiapo kadi zao. Akielezea kuhusu ujio wa kadi hizo mpya za TemboCardVisa, Mkuu wa kitengo cha Masoko, Joseline Kamuhanda alisema kadi hizo zimetengenzwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayowawezesha wateja kutumia kadi zao kwa urahisi kufanya malipo popote pale.
No comments:
Post a Comment