Akizungumza wakati wa droo hiyo mbele ya Msimamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Ladislaus Baraka alisema ushindi wa Abdallah umekamilisha orodha ya washindi 148 waliojishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh550 milioni tangu droo hiyo ilipozinduliwa mwezi Februari mwaka huu.
Kupitia kampeni hii, benki ya NMB imetoa zawadi ya fedha taslimu kwa washindi 120, pikipiki ya mizigo ya miguu mitatu aina ya LIFAN 24, magari matatu ya mizigo aina ya Tata ACE maarufu kama kirikuu na gari la kifahari aina ya Toyota Fortuner.
Akizungumza kwa njia ya simu baada ya kujishindia gari, Abdallah aliishukuru benki ya NMB kwa zawadi hiyo huku akiwahimiza watanzania kujenga utamaduni wa kuhifadhi fedha zao katika benki ya NMB. Alikiri kwani tangu aanze kuweka fedha NMB - ambayo ina matawi zaidi ya 225 nchini na machine za ATM zaidi ya 700 bila kusahau mawakala walitapakaa kila mahali, hajawahi kujuta kwani amekuwa mnufaika mkubwa wa huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo, na sasa amejishindia zawadi kubwa ya gari ambayo hakuitarajia.
"Bado sijaamini kama kweli nimeshinda zawadi ya gari kwa sababu hata sikujua kama kuna droo inachezeshwa leo; sina mengi zaidi ya kuishukuru NMB kwa zawadi hii," alisema Abdallah.
No comments:
Post a Comment