Ubora wa Benki ya NMB kiutendaji miaka ya hivikaribuni na mafanikio yake makubwa kifedha mwakajana ni miongoni mwa matokea ya ubunifu na uwekezajikatika mifumo ya kisasa hasa ile ya kidijitali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bi Ruth Zaipuna, amesema.
Akizungumza jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, kiongozihuyo alimwambia Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango, kuwa mifumo hiyo imekuwa na tija kubwa si tu kwataasisi hiyo kinara wa faida bali pia kwa serikali, wananchi na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2018, serikali imeweza kukusanya mapato yenye thamani ya takribani TZS trilioni 6 kupitia mifumo hii ambayo pia inamchango mkubwa kwenye ufanisi wa NMB kifedha.
Bi Ruth aliyasema hayo kabla ya kumkabidhi Dkt. Mpango hundi ya TZS 21.8 bilioni ambazo NMB imezitoa kwa serikali kama gawio la mwaka 2020 ikiwani ongezeko la asilimia 43 ya kiasi ilichokitoa mwaka2019.
Aidha, pamoja na kuwa mwanahisa mkubwa kwenyebenki hiyo, pia serikali ni mteja mzuri na mdau wakimkakati wa NMB kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali.
“Pamoja na miradi hii, uwekezaji ambao Benki ya NMB imeufanya kwenye teknolojia, unaendelea kuiwezeshabenki kuunganisha mifumo yake na taasisi mbalimbaliza serikali na zisizo za kiserikali na hivyo kurahisishaukusanyaji wa mapato,” Bi Zaipuna alisema.
“Serikali, zaidi ya kuwa mbia, ni mteja mzuri na mkubwawa Benki ya NMB. Sisi tunalitambua hilo natumeendelea kuwekeza katika teknolojia inayotoasuluhisho kwa serikali,” alifafanua.
“Pamoja na kuunganisha mfumo wa malipo ya serikalikatika mifumo ya Benki ya NMB, tunaendelea kuwekezakuhakikisha miamala mingine mbalimbali inafanyika kwanjia ya kielekroniki,” kiongozi huyo aliongeza.
“Juhudi hizi zote zinachangia kuleta ufanisi na pia kupunguza gharama za uendeshaji katika ukusanyaji wamapato. Kwa miaka mitatu, 2018/20, jumla ya TZS trilioni 5.9 zimekusanywa kupitia mifumo ya Benki yaNMB ambayo imeunganishwa na taasisi mbalimbalizilizopo nchini.”
Mbali na malipo ya gawio, ambalo katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 yamefikia TZS bilioni 155.8, Dkt Mpangoalisema NMB kuiwezesha serikali kukusanya mapatokupitia mifumo yake ni mchango mwingine mkubwakutoka benki hiyo mahili.
Alisema serikali inajivunia mafanikio makubwa ya NMB na kuwa mbia kwenye taasisi hiyo kitu ambachokinaifanya kupata faida nyinji zenye tija kutokana nauwekezaji wake wa asilimia 31.8. Dr Mpangoaliwachagiza Watanzania kuhakikisha benki hiyo inazidikuwa imara kwani faida zake ni kubwa kwao na taifa kwa ujumla.
Katika kipindi cha miaka mitano, benki hiyo imewezakuukuza mtaji wa wanahisa wake kwa ongezeko la zaidi ya TZS bilioni 463, hivyo kuufanya mtaji wake kufikiaTZS trilioni 1.1 ukilinganisha na TZS bilioni 666 mnamomwaka 2015.
Pia NMB imekuwa mstari wa mbele kusaidia ajenda yakitaifa ya kufikisha huduma za kifedha kwa Watanzania. Bi. Zaipuna alisema wigo mpana wa bidhaa na hudumazake umeongeza upatikanaji wa suluhisho za kifedhakupitia njia za kawaida na njia mbadala za kibenki.
Mpaka Desemba ya mwaka 2020, Benki ya NMB ilikuwana akaunti za wateja zaidi ya milioni nne na mawakalazaidi ya 8,400 waliotapakaa nchi nzima.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede, alisema zaidi ya ubunifu wa kidijitali, siri kubwa ya mafanikio ni wafanyakazi ambao ndiyo silaha kubwa ya benki hiyo. Aidha, mchango mwingineunatokana na ushirikiano kutoka kwa wateja pamoja na mazingira wezesha ya biashara.
No comments:
Post a Comment