Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Friday, 26 February 2021
JUMAMOSI HII WEST BROM WANAWAKARIBISHA BRIGHTON. TAZAMA MECHI HII LIVE NDANI YA DStv
Soka Jingi Hela Kiduchuuuu....
Jumamosi hii West Brom wanawakaribisha Brighton!..
Je nani kutoka na ushindi wa pointi tatu?
Piga *150*53# kulipia kifurushi cha Bomba TShs 19,900 tu ili usikose mechi mechi hii.
@abouliongo
#SokaLisiloPimika
WOMEN IN MANAGEMENT AFRICA AWARDS 2021 ARE BACK FOR THE SECOND EDITION!
Speaking at the launch, The Country Director for CV People of Tanzania, Naike Moshi said that, “It’s been a long wait, but we are pleased to finally announce that the second edition of the WIMA Awards is here and set to once again celebrate the senior women leaders across Africa who have excelled in their professional careers in different ways. The WIMA Awards were created to promote and increase visibility for Senior-Level Women in Management. The idea came to feature 50 Senior Women in Management to our Social Media Pages "Career Women Wednesday" This idea created a lot of buzz and traction by inspiring emerging leaders showing them it's possible for them to reach the career ladder specifically for female professionals.
Every year the corporate industry continues to grow in leaps and bounds and we are proud to be a part of its success story through this initiative. For this year, we have extended our awards and we have new categories such as SDG female champion, WIMA Stem Awards, Next Gem WIMA Awards, “He for She” Leadership Award, WIMA abilities Award, WIMA Lifetime Award and Exemplary Female Leadership during Covid-19 crisis.
Thursday, 25 February 2021
BENKI YA CRDB YAZINDUA HUDUMA YA ‘BENKI NI SIMBANKING’ JIJINI MWANZA
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Februari 25, 2021 katika tawi la Rock City Mall jijini Mwanza, Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Lusingi Sitta alisema huduma hiyo inawarahisishia wateja kutoa pesa, kuhamisha pesa, kufanya malipo ya Serikali huku pia usalama wa akaunti ya mteja ukiimarishwa zaidi.
Aidha Sitta aliongeza kuwa huduma nyingine zilizoboreshwa ni urahisi wa kupata mikopo mbalimbali, taarifa za mihamala ya fedha, kutoa pesa kwa mawakala na mashine za ATM bila kuwa na kadi ya benki na hivyo kuwahimiza wananchi kuchangamkia huduma hiyo kwani sasa hakuna sababu ya kwenda ndani ya benki kufuata huduma za kifedha kwa kuwa zote zinapatikana kiganjani.
GRAND FINALE YA NMB MASTABATA WIKI IJAYO
Kuelekea droo kuu 'Grand Finale' ya Kampeni ya NMB MastaBATA, Benki ya NMB imewataka wateja wake kuongeza kasi ya matumizi na manunuzi kwa njia ya Kadi za Mastercard na MastercardQR, ili kujiongezea nafasi ya kushinda safari ya utalii wa ndani ama zawadi mbadala.
NMB MastaBATA inayolenga kuhamasisha matumizi na manunuzi kwa njia ya kadi, ilizinduliwa Novemba 24 mwaka jana, ambako katika kipindi cha miezi mitatu sasa, imewazawadia washindi 400 wa kila wiki, pamoja na washindi 24 wa kila mwezi na sasa wanasakwa washindi wa fainali kuu.
Wito huo umetolewa na Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa NMB, Manfred Kayala, wakati wa droo ya wiki ya 10 ya NMB MastaBATA, iliyofanyika chini ya uangalizi wa Joram Mtafya, Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ambako washindi 40 walipatikana.
Kayala alibainisha kuwa, tayari washindi 400 wa kila wiki wameshazawadiwa pesa zao (Sh. 100,000 kila mmoja), kwa nyakati tofauti (jumla kuu ikiwa ni Sh. Mil.40), huku washindi wa kila mwezi 24, wakizoa zawadi mbalimbali zenye thamani ya Sh. Mil. 57.6.
DEPUTY MINISTER OF COMMUNICATIONS, ENGINEER ANDREA MATHEW VISITS AIRTEL TANZANIA OFFICES
PRESIDENT JOHN MAGUFULI DISSOLVES DAR CITY COUNCIL
President John Magufuli has dissolved Dar es Salaam City Council, while promoting Ilala Municipal to a City Council effective yesterday.
President Magufuli had earlier in in the day expressed the Government's intention to dissolve the Dar es Salaam City Council to ensure god expenditure of the taxpayers' money.
BENKI YA NMB YAFUNGUA TAWI SUA - MOROGORO
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda - amesema tawi hilo limekuwa likisubiriwa kwa hamu sana kwani NMB ndio taasisi ya kwanza kufungua tawi maeneo hayo na chuoni hapo ambapo anaamini, litachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo katika eneo hilo.
Naye Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi, alisema kufungua tawi hilo litawanufaisha wateja wao ambao ni wanafunzi na wana Morogoro kuweza hufurahia huduma bora za benki hiyo ikiwemo, akaunti ya Mwanachuo, NMB Mkononi, Akaunti ya Fanikiwa, Huduma za bima ikiwemo Dunduliza, akaunti za kilimo na nyingine nyingi.
KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAWAPELEKEA WAKAZI WA MIKOA YA KASKAZINI BIA MPYA YA GUINNESS SMOOTH
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakiifurahia bia mpya ya Guiness smooth muda mfupi baada ya kuzinduliwa hivi karibuni jijini Arusha. |
Katika uzinduzi wa bia hiyo mpya, wateja wa kampuni ya SBL, wauzaji wake wa bia pamoja na wenye mabaa walipata nafasi ya kuonja na kufurahia ladha ya kipekee ya bia ya Guinness smooth
Akiongea wakati wa uzinduzi huo jijini Arusha, Meneja Uvumbuzi wa SBL Bertha Vedastus alisema “Bia hii mpya kwenye familia ya Guinness ina ladha ya kipekee ambayo inamfanya kila mnywaji afurahie kila mara anapoitumia na wakati akiwa na marafiki,” alisema
Bertha aliongeza “Ikiwa imetengenezwa kwa kumjali mnywaji wa Kitanzania, bia hii ina hadhi ya kimataifa na imetengenezwa katika kiwanda chetu cha moshi huku ikitumia malighafi za Kitanzania ikiwa ni Pamoja na shayiri inayolimwa katika mikoa ya Moshi, Arusha na mingineyo,”
UBUNGO INTERCHANGE RENAMED AFTER ENG. JOHN KIJAZI
President John Magufuli yesterday inaugurated the Ubungo Interchange, renaming the one of its kind road junction after the fallen Chief Secretary, Engineer John Kijazi in honour of his contribution to the country's road sub-sector.
PRESIDENT JOHN MAGUFULI SAYS PROJECTS MUST BENEFIT ALL CITIZENS
President John Magufuli has warned authorities against overlooking and mistreating petty traders at the newly launched ultra-modern bus terminal in Dar es Salaam.
Dr. Magufuli made the remarks yesterday while inaugurating the 50.9 billion new bus terminal at Mbezi in the city.
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI ATEMBELEA KAMPUNI YA SIMU YA VODACOM
Wednesday, 24 February 2021
JUMAPILI HII SHEFFIELD UNITED WATAKUWA NA MECHI YA NYUMBANI DHIDI YA LIVERPOOL NDANI YA DStv
Jumapili hii Sheffield United watakuwa na mechi ya nyumbani dhidi ya Liverpool.... Je karata yako unaitupia wapi?
Piga sasa *150*53# kulipia kifurushi cha Bomba TShs 19,900 tu ili usikose mechi hii.
#SokaLisilopimika
Tuesday, 23 February 2021
BENKI YA NMB YAZINDUA KAMPENI YA "BONGE LA MPANGO" - ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 550 KUTUMIKA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI
Aina tatu ya zawadi zinazoshindaniwa ndani ya kampeni ya "Bonge la Mpango" - Pikipiki za miguu mitatu, gari ya mizigo alimarufu Kirikuu na Toyota Fortuner mpya. |
Katika kampeni hiyo, zaidi ya shilingi 550 milioni zitatumika kutoa zawadi kwa washindi, huu ukiwa ni mkakati wa Benki ya NMB kwa mwaka 2021 unaokusudia kuendelea kuifanya Benki ya NMB kuwa chaguo la kwanza kwa wateja kwa usalama wa fedha zao pamoja na uhakika wa huduma nyingine za kibenki.
Wateja wote wa NMB wanaofika zaidi ya Milioni Tatu nchini wana nafasi ya kushinda zawadi wakati mshindi wa mwisho atajinyakulia Toyota Fortuner mpya kabisa (kilomita sifuri) yenye thamani ya shilingi milioni 169.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi alisema ni hii ni moja ya njia za kurudisha faida kwa wateja wao waaminifu wanaotunza fedha ndani ya benki hiyo huku ikikusudia kuhamasisha utamaduni wa kutunza akiba kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
Monday, 22 February 2021
BAADA YA AMSHAAMSHA ZA MICHUANO YA #EPL, TUNAIANZA WIKI NA SAKATA LA LIGI YA #UEFA NDANI YA DStv
Ni mwendo wa bandika Bandua!
Kupitia Ofa ya Panda Tukupandishe, mteja wa Family lipia sasa Compact TShs 49,000 kwa kupiga *150*53# na DStv ikupandishe hadi Compact Plus uweze kutazama michuano hii Live.
#SokaLisilopimika
#PandaTukupandishe
DStv TANZANIA JUST GETS BETTER WITH SHOWMAX
- DStv Premium customers in Tanzania now get Showmax at no extra cost.
- DStv Bomba, Family, Compact and Compact Plus receive 50% off on Showmax subscription.
Jacqueline Woiso, Managing Director at MultiChoice Tanzania said, “We are introducing Showmax Add to Bill in response to our subscribers’ changing consumption patterns as a result of video entertainment services increasingly moving online”.
“As a Technology anchor within Tanzania, it’s only fitting that we maintain pace with these trends and provide greater access to our existing online entrainment offering. Showmax Add to Bill now makes it easier for DStv subscribers to access these services.
BENKI YA CRDB KUWAPA WATEJA WAKE MKONO WA POLE HADI SHILINGI MILIONI 15
Dar es Salaam - Benki ya CRDB imeendelea kutoa mafao ya gharama za mazishi na mkono wa pole kwa wateja wake wa ndani na nje ya nchi kati ya Shilingi milioni 2 hadi 15 kwa matatizo ya misiba au ajali.
Mafao hayo yanatolewa kupitia huduma ya bima ambatanishi ya maisha iliyozinduliwa na benki hiyo mwishoni mwa mwaka jana ijulikanayo kama 'KAVA Assurance'.
Akizungumza leo Februari 21, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Bima ya CRDB, Wilson Mzava, amesema waliangalia soko na kubaini kuna uhitaji ndipo walipoamua kutengeneza huduma hiyo ya KAVA Assurance.
"Tuliona wateja wetu walikuwa wanahitaji kitu cha ziada zaidi, tuliona pia wateja wetu wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) walikuwa na changamoto nyingi hasa pale mwenzao mmoja anapokuwa amefariki. Pia tukaangalia mtu akifungua akaunti katika Benki ya CRDB tunampa nini cha tofauti ili kumtofautisha na benki nyingine.
"Timu ya kitengo cha bima katika Benki ya CRDB ilikaa chini na kuamua kutengeneza bidhaa ambayo tutaiongezea thamani katika akaunti ya mteja wetu," amesema Mzava.
Akifafanua amesema mteja mwenye akaunti katika benki hiyo ikitokea akafariki benki itatoa mkono wa pole wa Shilingi milioni 2 na kwa wateja maalumu (Premier) benki itatoa Shilingi milioni 5 wakati wale wenye akaunti ya Tanzanite wanaoishi nje ya nchi watapewa Shilingi milioni 5.
STANBIC BANK DONATES TO THE OCEAN ROAD CANCER INSTITUTE IN DAR ES SALAAM AND LEMARA PRIMARY SCHOOL IN ARUSHA
Dar es Salaam - Stanbic Bank Tanzania has donated equipment worth TZS 9.1 million to Lemara primary school in Arusha and Ocean Road Cancer Institute in Dar es Salaam. TZS 4.4 million worth of equipment has gone to support the renovation of key facilities at Lemara Primary School, while TZS 4.7 million was for equipment and supplies to Ocean Road Cancer Institute. The donations are part of the bank's programmes to support the dispensation of quality health services to cancer patients and support the government in its efforts to continue providing quality education to Tanzanians.
The donations made by the bank are a reflection of Stanbic’s commitment to being one of the drivers towards economic development by investing in improving the livelihood of Tanzanians through various social investments.
BENKI YA NMB YATOA VIFAA VYA MILIONI 50 MOROGORO, DODOMA NA SINGIDA
Vifaa hivyo ni pamoja na Meza, viti, madawati, pamoja na vitanda kwa ajili ya vituo vya afya mbalimbali, vikiwemo vutanda kwa ajili ya kujifungulia akina mama wajawazito.
Katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Benki hiyo imetoa madawati 50, vito 50 pamoja na meza 50 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 15.
Saturday, 20 February 2021
BENKI YA NMB YAKABIDHI MABATI 200 KWA AJILI YA UKARABATI WA SHULE YA SEKONDARI YA JAMBIANI, KUSINI UNGUJA
“Benki ya NMB tumeamua kushirikiana pamoja na Jamii yote inayozunguka eneo la Jambiani kuchangia mabati 200 kwa ajili ya kutatua changamoto ya kuvuja kwa madarasa wakati wa mvua” alisema Donartus.
Aliongeza kuwa elimu ni kichocheo cha maendeleo hivyo kuna kila sababu kwa watoto kupata mazingira mazuri ya kupata elimu na kusisitiza ndio maana benki ya NMB imeamua kuisaidia shule hiyo.
Friday, 19 February 2021
JOB VACANCY AT NMB BANK PLC - RISK DATA ANALYST
Manager, Transaction Monitoring
Location:
Head Office
Application deadline:
2nd March 2021
Job Purpose:
- The Analyst is responsible for executing investigations to identify relationships that pose money laundering, terrorist financing, fraud, and sanctions risks.
- The Analyst compiles evidence and documentation in compliance with Anti Money Laundering (AML) procedures and regulatory requirements prior to escalations of potential Suspicious Transaction Reports (STRs) to Money Laundering Reporting Officer (MLRO).
- Ensure efficient identification and monitoring of suspicious activities and transactions.
- Support the implementation of an effective AML Transaction Monitoring alert analysis and suspicious activity investigations program to ensure compliance to relevant AML/Sanctions laws and regulations.
- Implement Transaction Monitoring (TM) techniques to support identification of risks around Money laundering, Terrorism Financing, Economic Sanctions, Fraud, and Operational risks consistent with the bank’s Financial Crime Compliance Risk Governance Framework.
- Monitor potentially suspicious patterns of activities and recommend changes to rules, parameters, and thresholds maintained within the transaction monitoring systems to ensure its continued effectiveness.
M-PESA CUSTOMERS TO REAP TZS 4.1 BILLION IN INTEREST PAYMENT FROM MOBILE MONEY TRANSACTIONS
Vodacom Tanzania Director of M-Pesa Ltd, Epimack Mbeteni. |
Director of M-Pesa Ltd Epimack Mbeteni said that the interest will be paid to M-Pesa customers, agents, super agents and M-Pesa business partners as well as retail agents who will all receive payments based on transactions made via their mobile wallets.
“In compliance with regulations of the Central Bank of Tanzania, interest earned from the deposit is periodically shared with the customers. Today we are happy to share a dividend of TZS 4.1 billion with our over 11 million customers across the Nation. M-Pesa service continues to give significant social and financial value to millions of Tanzanians with customers, agents, merchants and institutions currently transacting around TZS 100 Billion each day,” highlighted Mbeteni.
Vodacom Tanzania PLC has so far paid a total of TZS 147.6 billion as interest pay out to its M-Pesa Customers since July 2015 when Bank of Tanzania enacted the regulation.
BENKI YA NMB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 50 HANANG
Ringo alizitaka shule zilizopokea msaada kutoka NMB kuhakikisha wanafanya vizuri katika masomo na mitihani yao ili kuonyesha thamani ya mchango huo.
BENKI YA EQUITY TANZANIA YAZINDUA NJIA MPYA ZA UTUMAJI NA UPOKEAJI WA PESA KIMATAIFA
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, Robert Kiboti akizungumza na Waandishi wa Habari katika hafla fupi ya kutambulisha huduma mpya za kupokea pesa na kutuma kimataifa. Benki ya Equity imeungana na makampuni ya Kimataifa ya WorldRemit, Western Union, Terrapay na mengineyo katika kuhakikisha inapanua wigo wa huduma hizo duniani kote.
Tanzania inakisiwa kuwa na takriban wananchi milioni nne wanaoishi ughaibuni. Kwa mwaka, wananchi hao hutuma nyumbani Zaidi ya dola za milioni 437.
Akizungumza katika ghafla ya uzunduzi wa huduma hizo jijini Dar es Salaam hifi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity, Robert Kiboti kuwa alisema huduma hizi zipo katika vipengele viwili; Kwanza ni huduma za upokeaji na utumaji Pesa nje yaani (Remittance services) ambapo Benki ya Equity inashirkiana na makampuni makubwa ya World Remmit, Western Union, Money Gram, Small World, SimbaPay, Transact, Terrapy and Thunes ili kuweza kutuma na kupokea pesa kwa nchi zaidi ya 250 duniani.