Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda - amesema tawi hilo limekuwa likisubiriwa kwa hamu sana kwani NMB ndio taasisi ya kwanza kufungua tawi maeneo hayo na chuoni hapo ambapo anaamini, litachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo katika eneo hilo.
Chibunda alisema kuwa Benki hiyo licha ya kukuza uchumi pia itawapunguzia gharama, wateja wake hususani wafanyakazi wa SUA, wanafunzi na wakazi wa Magadu, Mzinga, Kididimo,Misufini, Vibandani, Kasanga, Lugala na Mafiga waliolazimika kusafiri hadi Tawi la Wami zaidi ya kilometa 6 kupata huduma za kibenki- kwani sasa watapata huduma hizo kwa ukaribu zaidi.
Naye Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi, alisema kufungua tawi hilo litawanufaisha wateja wao ambao ni wanafunzi na wana Morogoro kuweza hufurahia huduma bora za benki hiyo ikiwemo, akaunti ya Mwanachuo, NMB Mkononi, Akaunti ya Fanikiwa, Huduma za bima ikiwemo Dunduliza, akaunti za kilimo na nyingine nyingi.
Ufunguzi wa tawi hili, unafanya Morogoro kuwa na matawi ya NMB 14 na Kanda ya Mashariki matawi 22 na jumal ya matawi 227 nchi nzima!
Sambamba na uzinduzi huo, NMB imetoa msaada wa vifaa vya hosipitali ya SUA na madawati kwa Shule ya Sekondari SUA vyote vikiwa na thamani ya Sh. 13.7 milioni ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.

No comments:
Post a Comment