Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakiifurahia bia mpya ya Guiness smooth muda mfupi baada ya kuzinduliwa hivi karibuni jijini Arusha. |
Katika uzinduzi wa bia hiyo mpya, wateja wa kampuni ya SBL, wauzaji wake wa bia pamoja na wenye mabaa walipata nafasi ya kuonja na kufurahia ladha ya kipekee ya bia ya Guinness smooth
Akiongea wakati wa uzinduzi huo jijini Arusha, Meneja Uvumbuzi wa SBL Bertha Vedastus alisema “Bia hii mpya kwenye familia ya Guinness ina ladha ya kipekee ambayo inamfanya kila mnywaji afurahie kila mara anapoitumia na wakati akiwa na marafiki,” alisema
Bertha aliongeza “Ikiwa imetengenezwa kwa kumjali mnywaji wa Kitanzania, bia hii ina hadhi ya kimataifa na imetengenezwa katika kiwanda chetu cha moshi huku ikitumia malighafi za Kitanzania ikiwa ni Pamoja na shayiri inayolimwa katika mikoa ya Moshi, Arusha na mingineyo,”
Meneja uvumbuzi huyo aliongeza kuwa familia ya Guinnness Tanzania inayo furaha kuwaletea bia hiyo wakazi wa mikoa ya Kaskazini ambao siku zote wamekuwa waaminifu kwa bidhaa za SBL na kuongeza kuwa bia ya Guinness smooth itakuwa ikipatikana kwa shilingi 1,500 tu.
“Guinness inahistoria ndefu na kongwe ya kutengeneza bia bidhaa ambazo zimefanikiwa kuteka soko la dunia na kuendelea kuwa kinara. Bia hii ni muendelezo wa Guinness kuwaleta wateja wake bidhaa ambazo zinakidhi mahitaji yao na kuenda na wakati,” alisema
Baadhi ya wateja waliohudhuria uzinduzi na kuonja bia hiyo mpya walielezea kuvutiwa na ladha ya kipekee ya bia hiyo mpya na kusema kuwa watakuwa mabalozi wazuri.
“Bia ni nzuri na huu ni ujumbe kuwa ika kila sababu ya kufanya vizuri sokoni. Kwangu mimi kama msambazi wa bia naona ni fursa ambayo nitaitumia vyema kwa ajili ya kuweza kuongeza wigo wa wateja wangu Pamoja na kukuza biashara yangu pia,” aliongeza

No comments:
Post a Comment