Shule zilizopokea Misaada inayotolewa na benki ya NMB zimetakiwa kufanya vizuri katika masomo yao ili kuonyesha thamani ya misaada hiyo. Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Hanang,Ghibu Ringo wakati alipokuwa akizungumza baada ya kupokea msaada wa viti na meza 50 kwa ajili Shule ya Sekondari ya Getwanasi iliyopo wilayani hapa .
Ringo alizitaka shule zilizopokea msaada kutoka NMB kuhakikisha wanafanya vizuri katika masomo na mitihani yao ili kuonyesha thamani ya mchango huo.
“Unajua hata kama una mtoto wako unamilipia ada vizuri na kumnunulia mahitaji muhimu unategemea kuona matokeo yake mazuri,sasa hata ninyi shule hii na wengine ambao wameshapokea misaada mbalimbali kutoka NMB nataka kuona mnaonyesha mafanikio zaidi katika masomo yenu”alisema.
Alisema lazima wanaopata misaada hiyo kutoka Nmb na wadau wengine wa elimu na maendeleo kuonyesha thamani ya fedha zinazotolewa ili kuwatia moyo wa kuendelea kuwapa wengine.
“Haiwezekani mdau unakupa vifaa vizuri kama hivyo lakini matokeo anasiki shule hiyo imekuwa ya mwisho anajisikia vibaya kwa sababu lengo lake ni kukusaidia ufanye vizuri katika masomo yako”alisema
Aidha aliwataka aliwataka wakuu wa shule na kamati za shule kuweka mikakati ya kuvitunza vifaa vinavyotolewa na wadau wa maendeleo
Alisema misaada inapotoka inarekodiwa vizuri na uongozi wa halmashauri hivyo haiwezekani shuel hiyo hiyo kuendelea kuomba msaada wa vifaa hivyo kila.
Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hanang,Solomon Shati alisema halmashauri hiyo inazo shule sekondari 36 na kati ya shule hizo, ya binafsi ni moja tu,
Shati alisema kuwa kati ya shule hizo za serikali benki ya Nmb imetoa misaada kwa shule mbili kwa mwaka jana na mwaka huu ambapo msaada huo umesaidia kuleta mabadiliko kwa kuongezeka kwa kiwango ufaulu huko.
Kadhalika aliwashukuru NMB kwa misaada hiyo kwani imekuwa ikisaidia kupunguza mzigo kwa wanachi kwa wazazi kwani walitakiwa kununua mahitaji hayo
Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Rose Kamili alisema misaada ya Nmb imekuwa ikilenga maeneo ya wananchi wa uchumi wa chini jambo ambalo limekuwa likiigusa jamii.
Aliitaja misaada ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati pamoja na viti imekuwa chachu ya maendeleo ya elimu na jamii nchini.
Kwa upande wake Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alisema msaada huo wa viti na meza 50 uliotolewa na NMB unathamani ya milioni tano na unatokana gawio la faida iliyopata benki na kuirushia jamaii kutokan ana kuwaunga mkono
Mlozi alisema benki hiyo inatenga asilimia moja ya mapato yake kila mwaka na kuirudisha kwenye jamii kwa kutoa misaada katika sekta ya afya,elimu na majanga mbalimbali.
Alibanisha kuwa kutokana na serikali kuwa hisa za asilimia 38 wameona kuunga mkono juhudi za zake katika kutoa elimu kwa kuchangia vifaa vya elimu na ujenzi wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi waliochaguliwa na kushindwa kuanza masomo kutokana na upungufu wa vyumba kuanza masomo mwezi huu.
No comments:
Post a Comment