Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday, 24 January 2021

JOHNNIE WALKER WAITARA TROPHY YAWALETA PAMOJA WACHEZAJI 180 KUTOKA NJE NA NDANI YA NCHI

Veterani wa mchezo wa Gofu Dkt. Edmund Mndolwa (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 1,500,000 mshindi wa kwanza ambaye ni mchezaji wa kulipwa kutoka Klabu ya Gofu ya Lugalo Bryson Nyenza baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Kupitia kinywaji chake cha Johnnie Walker.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kulia) akimkabidhi zawadi ya kinywaji cha Johnnie Walker Mkuu wa Majeshi ya Ulinzia na Usalama mstaafu Generali George Waitara ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika mchezo wa Gofu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana wakati wa kuhitimisha mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy 2020.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) na Mkuu wa Majesi wa Malawi Generali Vincent Nundwe wakiingia uwanjani tayari kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy 2020. Mashindano hayo ya siku moja yalifanyika jijini Dar es Salaam jana na yalidhaminiwa na Kumpuni ya Serengeti Breweries kupitia kinywaji cha Johnnie Walker.

Baadhi ya washiriki wa mashindano wa Johnnie Walker Waitara Trophy 2020, wakijiandaa kwa ajili ya mashindano hayo makubwa yaliyofanyika katika viwanja vya Gofu vya kijeshi vilivyopo Lugalo jijini Dar es Salaam na kushirikisha zaidi ya wachezaji 180 kutoka nje na ndani ya nchi.

No comments:

Post a Comment