Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 22 January 2021

DStv YAZINDUA CHANELI MAALUM YA 007 JAMES BOND

Upele umepata mkunaji! Kama wewe ni shabiki wa filamu za nguli James Bond, sasa kaa mkao wa kula kwani M-Net Movies imetenga chaneli maalu kwa ajili ya filamu za James Bond.

Chanei hii maalum itakuwa kwamuda kuanzia Ijumaa Januari 22 hadi Jumapili Januari 31, 2021 na itakuwa DStv chaneli 111.

Chaneli hii maalum itakuwa katika vifurushi vya Compact, Compact plus na Premium. Kwa siku hizo kumi wapenzi wa filamu za James Bond watashuhudia filamu kali zilizotingisha ulimwengu wa filamu zilizoigizwa na waigizaji maarufu wakiwa kama James Bond wakiwemo Pierce Brosnan, Sean Connery, Roger Moore, bila kumsahau muigizaji wa sasa Daniel Craig.

Chaneli hii itazionyesha filamu za James Bond mfululizo kuanzia ile ya Dr. No (ya mwaka 1962), hadi ile ya Spectre (ya mwaka 2015).

Wateja wa DStv wa vifurushi vya Compact, Compact plus na Premium wataburudika na filamu hizo ambazo pia zitapatikana katika DStv Catch Up hadi Februari 28, 2021

Kwa wateja wa DStv vifurushi vya Bomba na Family wanaweza kupata chaneli hii kupitia chaneyi ya nyongeza ‘ad on’ ambayo ni M-Net Movies 1 (channel 104), M-Net Movies 2 (channel 106), na fliekNet (channel 149).

Kwa maelezo zaidi tembelea ukurasa wa M-Net Movies m-net.dstv.com.

No comments:

Post a Comment