Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 29 January 2021

BENKI YA ABSA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI KWA SHULE ZA DODOMA

Mwakilishi wa Benki ya Absa Tanzania, Elizabeth Kiwale akizungumza na walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji vifaa vya usafi kwa shule za msingi 54 vilivyotolewa kwa udhamini wa Absa, jana katika Shule Msingi Ipagala B jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Benki ya Absa tawi la Dodoma, Elizabeth Kiwale (wa pili kushoto), akimkabidhi vifaa vya usafi ndoo na sabuni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ipagala B, Plaxeda Fundisha, (wa tatu kulia) katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji vifaa vya usafi kwa shule za msingi 54 ulioratibiwa na Shirika la Pact Tanzania kupitia mradi wa WASH unaodhaminiwa na Absa. Uzinduzi huo ulifanyika jana shuleni hapo, jijiji Dodoma. Wa tatu kushoto ni mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Mazengo Eliasi na kushoto ni Beatrice Kamugisha kutoka Pact Tanzania.
Wawakilishi kutoka benki ya Absa Tanzania, Elizabeth Kiwale na Happy Alipipi pamoja na wahudhuriaji wengine wakinawa mikono kwa kutumia vifaa vilivyotolewa msaada na benki hiyo katika hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo kwa Shule ya Msingi Ipagala B, jijini Dodoma.
Mwanafunzi wa Shule ya Ipagala B, Jesca Saimon pamoja na mwenzake wakinawa mikono baada kukabidhiwa vifaa vya usafi kutoka Benki ya Absa shuleni kwao, Dodoma jana.

No comments:

Post a Comment