Peter Joseph meneja msaidizi idara ya rasilimali watu akitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake walioudhuria katika mafunzo hayo, Yombo jijini Dar es Salaam. |
Mmoja wa wanawake walioudhuria katika mafunzo hayo, Bi. Eva Tumaini akizungumza na waandishi kuipongeza benki ya I&M kwa kutoa elimu ya fedha na ujasiriamali kwa jamii. |
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya I&M wakishirikiana na mmoja wa wanawake katika kufundisha mbinu za biashara ili kujikwamua kiuchumi kupitia mapishi. |
Siku ya Ijumaa Novemba 6, wafanyakazi wa Benki ya I&M wakiongozwa na Meneja Masoko na Mawasiliano ya Benki, Bi. Anitha Pallangyo, Meneja Msaidizi wa idara ya Rasilimali watu, Elimu na Maendeleo Bw. Peter Joseph, Bi. Hellen Mbwana kutoka idara ya ukaguzi wa ndani na wafanyakazi wengine waliotoka katika matawi ya hapa Dar es Salaam na idara nyingine mbalimbali ndani ya benki hiyo, walitembelea vikundi vya kina mama wajasiriamali wadogowadogo waliopo maeneo ya Yombo vituka jijini Dar es salaam, na kutoa elimu ya kuhusu mambo ya fedha, uwekaji akiba na ujasiriamali kwa wakina mama hao waliokusanyika kujipatia elimu hiyo.
Akielezea lengo la kuanzisha mpango huu wa ‘IM FOR YOU’ unaomaanisha ‘I&M Kwaajili yako’, wa kutoa elimu bure kwa jamii na lengo la kutembelea vikundi hivyo vya wakina mama vilivyopo maeneo ya Yombo Vituka, Bi. Anitha Pallangyo alisema, “Tumeazisha mpango huu kama moja ya njia ya kurudisha kwa jamii kile ambacho timu yetu ya rasilimali watu imekipata kutoka kwenye kazi zetu za kila siku, na kama tunavyojua kuwa elimu ni ufunguo wa maisha, hivyo tumeona ni vyema kukutana na vikundi mbalimbali vya wakina mama na vijana hasa ambao wanajishughulisha na biashara ndogondogo kujikwamua kiuchumi, ili kuwaongezea ujuzi na mbinu za kuongeza kipato. Mpango huu utasaidia hata serikali kupunguza idadi ya watu ambao hawajaajiriwa kwani unalenga kumfungua kijana na watanzania kwa ujumla kubuni mbinu mbalimbali za kibiashara ili kuweza kujiajiri.
Bw. Peter Joseph, Meneja Msaidizi idara ya rasilimali watu akiongea na waandishi katika tukio hilo alisema Benki ya I&M inajitahidi kuajiri wafanyakazi wenye uwezo mkubwa na ufanisi wa kazi, pamoja na kuwawezesha kuongeza ujuzi kupitia mafunzo mbalimbali ndani na nje ya ofisi hivyo imezalisha vijana wanaoweza kutoa elimu bora kwa jamii hasa kwa mambo ya fedha, umuhimu wa kujiwekea akiba na ujasiriamali.
Pamoja na kutoa elimu kwa jamii, timu hiyo ya wafanyakazi wa benki ya I&M ambayo ilienda kuwakilisha wafanyakazi wote kutoka idara mbalimbali, ilipeleka vitu mbalimbali ambavyo wafanyakazi walijitolea kwaajili ya kina mama wanaoishi kwenye mazingira magumu kama vile wajane, wamama wanaolea watoto yatima, na walemavu kwenye jamii hiyo, vitu hivyo ni pamoja na nguo, viatu, vyakula, sabuni, dawa za mswaki nakadhalka.
Benki ya I&M imekua mstari wa mbele katika kujitolea kwa jamii kupitia mikakati mbalimbali ya elimu, afya na mazingira. Benki hiyo inatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wananchi wote kwa ujumla ikiwemo akaunti za akiba za watoto, wanafunzi, wafanyabiashara, wanawake, mikopo, huduma za kuhamisha fedha, huduma za kubadili fedha za kigeni nakadhalika. Benki hiyo inatarajia kuanzisha huduma za WAKALA hivi karibuni ambapo inategemea kuwa na mawakala walioenea Dar es salaam na mikoani, pia ina matawi yanaoendelea kutoa huduma bora ambayo ni;Tawi la maktaba, tawi kuu linalo patikana mtaa wa Indira Gandhi, Kariakoo, Nyerere, Oysterbay, Moshi, Arusha na Mwanza. Pia kupitia huduma zake za benki kwa njia ya simu (Mobile Banking) *150*32#, kwa njia ya mtandao (Internet Banking) na App, wateja wake wanaweza kupata huduma za kibenki saa 24 mahali popote wowote
No comments:
Post a Comment