September 3, 2020 - Katika kusaidia utimizaji wa azma ya kuleta maendeleo kwa watanzania na kuondoa umasikini, Benki ya Biashara ya DCB imeingia makubaliano na asasi isiyo ya kiserikali ya UYACODE inayotoa uangalizi na usimamizi wa VICOBA. Taasisi hii inatoa mafunzo,usimamizi na uratibu wa vikundi vya benki ndogo za kijamii (VICOBA) kwenye mikoa 21 Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa wadau wa UYACODE kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, Zacharia Kapama alisema ni matumaini wanachama wa UYACODE watanufaika na utaratibu huu ambapo benki itasaidia kujenga uwezo wa vikundi hivi huku vikinufaika biadhaa mbalimbali na huduma bora za kibenki zinazotolewa na benki hiyo, ikiwemo akaunti zisizo na makato , mikopo ya riba nafuu na msaada wa ushauri wa kitaalamu ikiwemo mfumo wa usimamizi wa kifedha.
“DCB kwa miaka kadhaa tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika huduma zinazowalenga wajasiriamali walio katika vikundi mbalimbali tukiwa na vikundi vya Vicoba zaidi ya 8,000 huduma ambazo zimeweza kubadilisha maisha na kukuza mitaji ya wengi ya wanavicoba hao.
Pamoja na hayo mkurugenzi huyo alisema ni imani ya DCB kuwa ushirikiano huo utakuwa chachu ya mafanikio ya kiuchumi kwa pande zote mbili ikiwa ni wanachama wa UYACODE kwa upande mmoja na DCB kwa upande mwingine kutokana na ukweli kuwa wa asasi hiyo inayoundwa na vikundi vya Vicoba zaidi ya 700.
“Natoa wito kwa wanachama wote na wasio wanachama kujiunga na UYACODE na pia kuchangamkia fursa hii kujiunga na akaunti ya vicoba ya DCB ili kusaidia serkali katika mpango wake wa kurasilimisha taasisi hizi .
“Natoa wito kwa watanzania kujiunga na Benki ya DCB ili kuweza kunufaika kiuchumi na kunufaika na huduma zetu kama DCB Sokoni, DCB Digital, Mikopo ya Ada kwa wanafunzi, DCB Lamba Kwanza, DCB Kibubu na nyinginezo”, aliongeza Bwana Kapama.
No comments:
Post a Comment