Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 9 September 2020

TIGO YAUNGANA NA SAMSUNG KUZINDUA SAMSUNG NOTE 20 NA SAMSUNG NOTE 20 ULTRA TANZANIA

Meneja wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Simu janja aina ya Samsung Note 20 na Samsung Note 20 Ultra. Kushoto kwake ni Meneja Mkaazi wa Samsung electronics Tanzania, Suleiman Mohamed. Hafla ya uzinduzi imefanyika hivi karibuni  katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es Salaam.
Meneja Mkaazi wa Samsung electronics Tanzania, Suleiman Mohamed akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Simu janja aina ya Samsung Note 20 na Samsung Note 20 Ultra. Kulia kwake ni Meneja wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga.
Meneja wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga akieleza sifa za Simu janja aina ya Samsung Note 20 na Samsung Note 20 Ultra mara wakati wa uzinduzi wa simu hizo hifi karibuni jijinj Dar es salaam. Anayeshuhudia pembeni ni Meneja Mkaazi wa Samsung electronics Tanzania, Suleiman Mohamed .
  • Wateja watakaonunua simu hiyo watajipatia Gb78 za intaneti kwa mwaka mzima
Dar es Salaam. Septemba 4, 2020. Kampuni inayoongza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo kwa kushirikiana na Samsung Electronics wamezindua Simu janja aina ya Samsung Note 20 na Samsung Note 20 Ultra.

Ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kuongea matumizi ya mtandao wa 4G na kuchangia ukuaji wa teknolojia ya kidigitali nchini.

Meneja wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo alisema “Ni jambo la kubwa sana kwetu kuchaguliwa na Samsung kuwa wa kwanza kuzihifadhi na kuuza simu za Samsung Note 20 na Samsung Note 20 ultra kwenye soko la Tanzania. Hii inaonesha imani yao kwetu juu ya chaneli kubwa za usambazaji tulizonazo na pia kupitia timu yetu ya huduma kwa wateja inayotoa huduma zenye ubora wa hali ya juu,” alisema Myonga.


“Lengo letu ni kuchochea mageuzi ya kidigitali katika maisha ya watu hapa nchini na ndio maana tumeungana na Samsung ili kuongeza idadi ya umiliki wa simu janja pamoja na matumizi ya data ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanaifikiwa na teknolojia hii,” alisema Muyonga.

Muyonga aliongeza “Tunalenga kuongeza ueneaji wa simu janja nchini huku tukihakikisha wateja wetu wanafurahia huduma za kidigitali kupitia mtandao mkubwa wa 4G hapa nchini.Na ndio maana tunatoa 78 Gb za intaneti kwa mwaka mzima kwa wateja wote watakaonununa Samsung Note 20 na Samsung Note 20 Ultra,” alisema .

Akizungumza wakati wa uzindizu huo, Meneja Mkaazi wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohamed alisema Samsung imezindua simu ya Samsung Note 20 na Samsung Note 20 ultra toleo jipya ulimwenguni ambayo itabadilisha namna ambavyo watu wanavyoishi na kuufurahia ulimwengu.

“Tukiwa tunaingia kwenye muongo mwingine, kuna mabadiliko makubwa kwenye sekta ya mawasiliano na namna watu wanavyo ujua na kuufurahia ulimwengu.Samsung inahakikisha inatoa teknolojia na vifaa vya kisasa zaidi ili kuendana na mabadiliko hayo.Kwa kutumia camera yenye mfumo wa AI unaweza kupata kila tukio na kuungana na uwapendao bila mipaka,” alisema Mohamed.

Simu ya Samsung Note 20 itauzwa kwa Sh2,480,000, na Samsung Note 20 Ultra kwa sh 3,185,000.

No comments:

Post a Comment