Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 30 September 2020

BENKI YA CRDB YABORESHA HUDUMA KWA WASTAAFU SASA KUHUDUMIWA KIDIJITALI

Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts (watatu kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji kwa wastaafu uliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam, leo. Wengine pichani ni kutoka kulia ni Mwenyekiti wa makatibu Wakuu Wastaafu, Michael Mwanda, Balozi Mstaafu Salome Sijaona, Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa, Mwenyekiti wa Umoja wa Polisi Wastaafu, Kamishna wa Polisi Mstaafu Suleiman Kova na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Adili Stephen.

Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts (watatu kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji kwa wastaafu uliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa na kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Polisi Wastaafu, Kamishna wa Polisi Mstaafu Suleiman Kova.

Benki ya CRDB imezindua mpango maalum wa uwezeshaji kwa wastaafu ambao unatoa fursa mbalimbali zinazolenga katika kuboresha maisha yao. Akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo wenye kauli mbiu ya “Ndoto zako hazistaafu”, Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts amesema mpango huo anajumuisha fursa za kujiwekea akiba, uwekezaji, pamoja na uwezeshaji wa kifedha kwa wastaafu.

Dkt. Witts alisema pamoja na uzinduzi wa mpango huo Benki ya CRDB pia imezindua huduma za akaunti maalum ya wastaafu “Pension Account” na huduma ya uwezeshaji kifedha kwa wastaafu kidijitali “Pension Advance” kupitia huduma ya SimBanking App.

Akielezea kuhusu akaunti ya wastaafu, Dkt. Witts alisema akaunti hiyo inawawezesha wastaafu kupokea pensheni zao kwa urahisi na usalama na kujiwekea akiba kutokana na vipato vinavyotokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi wanazozifanya. Dkt. Witts alisema ili kutoa nafuu kwa wastaafu akaunti hiyo hufunguliwa bure, haina makato yoyote yale na hutoa fursa kwa wastaafu kuunganishwa bure na mifumo ya utoaji huduma kidijitalli ikiwamo SimBanking na Internet Banking.

“Ninajivunia kuwajulisha kuwa hadi leo hii tukiwa tunazindua mpango huu wa uwezeshaji wastafu, tayari wastaafu zaidi ya 19,000 wameshafungua akaunti hii na wanafurahia huduma zetu,” alisema Dkt. Witts huku akibainisha kuwa kupitia akaunti hiyo wastaafu wanapewa TemboCard inayowawezesha kupata huduma kwa CRDB Wakala na ATM zote nchi nzima.

Kwa upande wa huduma ya uwezeshaji wa kifedha kupitia “Pension Advance”, Dkt. Witts alisema sasa hivi wastaafu wanaweza kupata uwezeshaji wa fedha za kujikimu na kuendesha maisha yao kuanzia shilingi 50,000 hadi shilingi milioni 1 popote pale walipo kidijitali kupitia SimBanking App, huku akibainisha kuwa mkopo huo wa Pension Advance unatolewa bila riba yoyote.

Akizungumzia kuhusu fursa za uwekezaji zinazotolewa na Benki ya CRDB kupitia mpango huo, Dkt. Witts alisema benki hiyo pia imeanzisha akaunti maalum ya uwekezaji ijulikanayo kama “Akaunti ya Thamani” ambayo inawawezesha wastaafu kujipatia kipato kila mwezi. “Akaunti hii ya Thamani inatoa fursa kwa wastaafu kuwekeza kwa kipindi cha miaka mitatu kwa riba ya hadi asilimia 8,” alisema Dkt. Witts.

Naye Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Rabala alisema kupitia mpango huo wa uwezeshaji kwa wastaafu benki hiyo pia imejipanga kuendelea kutoa mikopo kwa wastaafu ili kuwawezesha kuendeleza biashara na miradi yao ya maendeleo na hivyo kupunguza ukali wa maisha ya kila siku. Kupitia mkopo huo Wastaafu wanaweza kukopa kuanzia shilingi milioni 1 hadi shilingi milioni 100 kwa kipindi cha mwaka 1 hadi 7.

Mwenyekiti wa Makatibu Wakuu Wastaafu, Michael Mwanda aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwakumbuka wastaafu kupitia huduma na bidhaa zinazotolewa na benki hiyo. Mwanda alitoa rai kwa wastaafu wote kuchangamkia fursa hizo kuboresha maisha yao huku akiitaka Benki ya CRDB kutoa semina juu ya huduma hizo kwa wastaafu wote nchi nzima.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Polisi Wastaafu, Kamishna wa Polisi Mstaafu, Suleiman Kova aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuja na mpango huo wa uwezeshaji kwa wastaafu huku akibainisha kuwa zitasaidia kuleta chachu ya maendeleo na kufanya kustaafu kusiogopwe. “Na sisi wastaafu sasa tunajidai tuna benki yetu ambayo sio tu inausikiliza bali pia inatambua mchango wa wastaafu katika taifa letu, Asanteni sana Benki ya CRDB,” alisema Kova huku akimuomba Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts kumsaidia kufungua akaunti ya Wastaafu ili aweze kufurahia huduma zote zinazotolewa katika mpango huo wa uwezeshaji wastaafu.






GEITA GOLD MINING LIMITED AND RAFIKI SURGICAL MISSION DONATE AN AMBULANCE TO BUKOLI HEALTH CENTRE IN GEITA DISTRICT

Executive Director for Geita District Council, Ali Kidwaka (left) receives the ambulance registration card from GGML’s Vice President, Simon Shayo.

GGML's Vice President for Sustainability, Simon Shayo (right) speaking to Bukoli Health Centre staf and residents during handover ceremony. Seated beside him is the Geita District Council Executive Director, Ali Kidwaka and the Geita District Medical Officer, Deo Kisaka.
Geita Gold Mining Limited (GGML) and Rafiki Surgical Mission from Australia have jointly donated an ambulance worth TZS 32 million to Bukoli Health Centre in Geita District. The ambulance will serve patients residing in close proximity to Bukoli Ward and the rest of Geita region.

Speaking during the handover ceremony at Bukoli village in Geita, the GGML Vice President – Sustainability, Simon Shayo highlighted that the ambulance donation was timely and would alleviate transportation challenges for critically ill patients.

“The Geita District Council requested an ambulance from GGML to help the Bukoli community who had limited means to transport patients with medical referrals to Geita Referral Hospital which is approximately 35 kilometres from Bukoli. Partnering with Rafiki Surgical Mission in response to that request came naturally as we have proved over the years our dual commitment to support health initiatives in Geita,” said Shayo.

IMPACT BUSINESS BREAKFAST; THEME - THE ROLE OF DIGITAL SOLUTIONS IN IMPROVING FINANCIAL INCLUSION

Today about six in 10 adults (56%) in Tanzania are financially included, almost all through mobile money accounts (55%). Tanzania has a predominantly rural population, which makes access to financial services a challenge and digital solutions ideal. 

Sixty-six percent of the population resides in rural areas, and FII data shows that less than one-third (29%) of the rural population have active accounts (used in the last 90 days), whereas urbanites are twice as likely to have active accounts (61%). Approximately 77% of Tanzania’s adults live on less than $2.50 per day, with three-quarters of Tanzanians employed in the agriculture sector, according to World Bank data.

There is an increasing need to implement strategic alliances between financial institutions, Fintechs, Telcos and government to facilitate a more deliberate collaboration that will enhance financial inclusion.

In the next Impact Business Breakfast, we will bring together key players within the financial sector; Banks, Mobile Network Operators, Financial services development organizations, Government and FinTech start-ups to discuss on best case partnership opportunities and policies that will allow multi-stakeholder collaborations that will facilitate a more inclusive financial services and create linkages /collaboration structures between key players in ensuring that unbanked adults in Tanzania are able to access financial services, contribute to national economy growth and increase job creation.

Tuesday, 29 September 2020

BENKI YA NMB YASHIRIKI MKUTANO WA VIJANA WA UMOJA WA MATAIFA JIJINI ARUSHA

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro (kulia) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Mwinyi Haji kuhusu programu za Benki hiyo za kuinua vijana nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, jijini Arusha leo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Mwinyi Haji alipokua akitoa salamu za pongezi kwa Benki hiyo kwa jitihada zao za kuinua vijana nchini. 
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro akizungumza wakati wa mkutano huo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro (kulia) akipokea Mkono wa pongezi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Mwinyi Haji baada ya kuitimisha hotuba yake kuelezea fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa vijana. Anaeshuhudia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Prof. Emmanuel Luoga.
Benki ya NMB imeeleza kuwa vijana ndio dira ya maendeleo ya sasa na baadaye kwa taifa lolote duniani na ni kundi muhimu la kuzalisha viongozi bora.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro amesema hayo leo katika ufunguzi wa mkutano wa vijana walio katika mtandao wa jumuiya za Umoja wa Mataifa nchini (YUNA) unaofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela jijini Arusha.

Amesema NMB ni benki inayothamini zaidi vijana na imejikita katika kutambua nafasi zao katika ujenzi wa taifa na ukuaji wa sekta ya fedha nchini.

Aikansia amesema benki hiyo inaendesha programu maalumu kwa vijana wanaotoka vyuoni –Graduate Trainee - kujifunza na baadae kupata kazi za kudumu, na kati ya mwaka 2019 na 2020 zaidi ya vijana 50 wameshanufaika na programu hiyo.

DStv INAKULETEA KIKOSI CHA JOSÉ MOURINHO DHIDI YA KIKOSI CHA MWANAFUNZI WAKE LAMPARD NDANI YA CARABAO CUP SAA 3:45 LEO USIKU

Kweli kabisa utu uzima ni dawa lakini hapa kila kitu kitawekwa kando tunachotafuta ni ushindi tu! Kikosi cha José Mourinho dhidi ya kikosi cha mwanafunzi wake Lampard, lazima kiwake ndani ya Carabao Cup...

Kunogesha mambo sasa DStv inakupa kutazama mechi hii kupitia kifurushi cha Bomba TShs. 19,900 tu. 


Piga sasa *150*53# kulipia kifurushi chako sasa au 0659 07 07 07 kujiunga na DStv.

#SokaLisiloPimika

#WorldBestFootball

Monday, 28 September 2020

MASHINDANO YA NCBA GOLF TOURNAMENT YAFANA ZANZIBAR

Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa Benki ya NCBA, Gift Shoko akipiga mpira kwenye mashindano ya gofu ya NCBA yaliyofanyika viwanja vya Sea cliff Zanzibar. Mashindano hayo yameenda sambamba na uzinduzi wa tawi la benki hiyo mtaa wa Mlandege mjini Zanzibar na kushirikisha zaidi ya wachezaji 70.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NCBA Tanzania Limited, Margaret Karume akipiga mpira kwenye mashindano ya gofu ya NCBA yaliyofanyika viwanja vya Sea cliff Zanzibar. Mashindano hayo yameenda sambamba na uzinduzi wa tawi la benki hiyo mtaa wa Mlandege mjini Zanzibar na kushirikisha zaidi ya wachezaji 70. 
Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Mhe. Balozi, Mohamed Ramia Abdiwawa (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa NCBA Bank, Margaret Karume (kulia), Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko wakimkabidhi zawadi mshindi wa jumla wa mashindano ya NCBA Golf Tournament Zanzibar, Ross Owen. Mashindano hayo yameenda sambamba na uzinduzi wa Tawi la Benki ya NCBA mtaa wa Mlandege, hafla ya sherehe ilifanyika Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar. 






BENKI YA NMB YAPONGEZWA KWA KUTOA AHUENI WAKATI WA COVID-19

Serikali na wadau mbalimbali wameipogeza Benki ya NMB kwa msaada wake mkubwa wakulisaidia Taifa na wateja wake kukabiliana na changamoto za janga la COVID-19 ambalo athari zake kiuchumi na kibiashara zinaendelea kuitikisa dunia.

Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha wakati wa hafla ya Mtandao wa Wateja Wakubwa wa Benki hiyo ‘NMB Executve Network’ uliyowaleta pamoja wateja zaidi ya 100 wa Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa mitatu ikiwemo Tanga na Kilimanjaro.
Wafanyabiashara wakubwa ambao ni wateja wa Benki ya NMB Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo kwenye hoteli ya Gran Melia jijini Arusha kujadili mikakati ya kuboresha ushirikiano.
NMB ilitangaza unafuu wa ulipaji mikopo kwa wateja wake mwezi Mei mwaka huu, kupitia likizo ya marejesho ya mikopo yao na wengine wakiongezewa muda wa kulipa mikopo hiyo ili kuwasaidia kukabiliana na madhara yaliyoletwa na COVID–19 katika biashara zao.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Longido - Frank Mwaisumbe alisema NMB iliwasaidia sana wateja wake na imeendelea kuwa nao karibu wakati wote wa kipindi cha COVID-19 na wao kama Serikali wanawapongeza kwa hilo. Ni jambo kubwa hasa kwa Sekta ya Utalii ambayo imeathiriwa sana na COVID-19. Siyo hivyo tu, Frank vilevile aliipongeza Benki hiyo kwa utaratibu wake wa kukutana na wateja jambo ambalo alisema linasaidia kuboresha mahusinao kati ya Benki na wateja wao.
Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo kwenye hoteli ya Gran Melia jijini Arusha.

Naye Afisa Mkuu wa Huduma Jumuishi wa NMB - Nenyuata Mejooli alisema, Benki ya NMB ilitoa ahuweni kwa wateja wake ili kuhakikisha shughuli zao zinastahimili misukosuko ya COVID-19 ikiwemo kubadilisha mfumo wa urudishaji mikopo kulingana na ukubwa wa athari.

Wakati huohuo, Nenyuata, aliwapongeza wateja wao kwa ukakamavu waliouonyesha kipindi cha COVID-19 na kuahidi kuendelea kuwa nao bega kwa bega. “Tunaelewa katika kipindi hiki,biashara kama utalii na sekta ya hoteli zilipata changamoto. Sisi kama NMB tumehakikisha tupo karibu zaidi nanyi wateja wetu ili kuhimili changamoto hizo zilizojitokeza,” aliongeza.

Wiki hiyohiyo, NMB pia iliweza kuwakutanisha wateja wadogo na wa kati walioujiunga na mtandao maalumu wa ‘NMB Business Club’ na kuwapa elimu ya masuala ya kibenki ikiwemo mifumo mipya ya malipo kupitia NMB Mkononi, Mastarcard QR pamoja na huduma zingine za Benki kama Bima (NMB Bancassuarance).

Washiriki wa kongamano la wafanyabiasha Wadogo na wa Kati waliojiunga na Mtandao wa NMB Business Club kutoka Arusha, Moshi na Tanga wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
Mwakilishi wa kiwanda cha ngozi cha Tanneries kutoka Himo Wilaya ya Moshi - France Sawerio kulia,akitoa maelezeo kwenye maonesho ya bidhaa anazo zitengeneza,wakati Viongozi wa Benki ya NMB walipo tembelea banda lake wakati wa Kongamano la wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (NMB Business Club), lililofanyika katika ukumbi wa Kuringe - mjini Moshi.
Tangu kuanzishwa kwa NMB Business Club miaka sita iliyopita, mtandao huo upo kwenye Mikoa ya; Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Mtwara, Mbeya na Dodoma huku washirika wake wakiwa zaidi ya 600.

DStv INAKULETEA LIVERPOOL DHIDI YA ARSENAL LEO USIKU NDANI YA ULIMWENGU WA MICHEZO SUPERSPORT

Tunaifungua wiki vyema na kivumbi cha EPL kinatimka kikiwakutanisha Liverpool dhidi ya Arsenal, na kama kawaida sehemu pekee yenye #SokaLisilopimika ni DStv ndani ya ulimwengu wa michezo SuperSport.

Hakikisha unalipia mapema kifurushi cha Compact TShs. 49,000 tu ili uweze kutazama mechi zote za EPL Live.

Piga 0659 07 07 07 kujiunga na DStv kwa gharama nafuu zaidi.

#WorldsBestFootball.

#SokaLisiloPimika

Sunday, 27 September 2020

BENKI YA NCBA YAENDELEA KUPANUA WIGO WAKE, YAFUNGUA TAWI JIPYA ZANZIBAR

Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Mhe. Balozi, Mohamed Ramia Abdiwawa (wa pili kulia) akizindua nembo ya benki ya NCBA kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo lililopo jengo la Muzamil mtaa wa Mlandege mjini Zanzibar. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Mhe. Hassan Khatib, Mkurugenzi Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Limited, Margaret Karume, Mshauri wa Raisi wa Zanzibar, Mhe. Abdulrahman Mwinyimbegu, Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Mhe. Hassan Hafidh na mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank, Gift Shoko. 
Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Mhe. Balozi, Mohamed Ramia Abdiwawa akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya NCBA lililopo jengo la Muzamil mtaa wa Mlandege mjini Zanzibar. 

Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Mhe. Balozi, Mohamed Ramia Abdiwawa akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NCBA nchini, Margaret Karume kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la Benki hiyo lililopo jengo la Muzamil mtaa wa Mlandege mjini Zanzibar.
Benki ya NCBA imedhamiria kuchangia juhudi za maendeleo za dira mpya ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2020-2050
Zanzibar. NCBA Bank Tanzania Limited (NCBA) ilisherehekea hatua nyingine ya kihistoria ya ujio wake nchini kwa kuzindua tawi jingine jipya visiwani Zanzibar jumamosi ya tarehe 26 Septemba. Tawi hili linapatikana Mtaa wa Mlandege, Kituo cha Muzzamil.

Hafla hii ni kati ya sherehe zinazoendelea za ujio wa Benki ya NCBA ambayo ni muunganiko wa hiari kati ya NIC Bank (T) Limited na CBA Bank (T) Limited ambapo huduma rasmi za taasisi hii mpya zilianza tarehe 8 Julai 2020 baada ya idhini ya Benki Kuu ya Tanzania.

Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Mhe Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa alikua mgeni rasmi kwenye hafla hiyo aliipongeza Benki ya NCBA kwa juhudi zao za kuungana.

Waziri aligusia maeneo muhimu ambayo serikali ya Mapinduzi imefanikiwa katika maono yao ya maendeleo ya 2020, na alitoa wito kwa Benki ya NCBA kusaidia inapobidi kutokana na nguvu zake za kifedha na uimara kama taasisi ya fedha kwenye Dira mpya ya maendeleo ya Zanzibar ya 2050; alinukuliwa, ‘‘Katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita, uchumi wetu umekuwa ukikua kwa kiwango cha kila mwaka kwa zaidi ya asilimia 4. Haya yamefanikiwa pamoja na kukuza kilimo, ushupavu na ushindani katika tasnia ya utalii, huduma na sekta zingine za uzalishaji wa uchumi. Tumeweka pia mifumo na sera ngumu ili kukabiliana na changamoto za soko linalobadilika na hali ya kiteknolojia ulimwenguni’’.

BENKI YA NCBA YAZIDI KUPANUA MTANDAO WAKE WA HUDUMA KWA WATEJA, YAZINDUA TAWI JIPYA ZANZIBAR

Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Balozi, Mohamed Ramia Abdiwawa (katikati) akikata utepe kuzindua tawi jipya la benki ya NCBA lililopo mtaa wa Mlandege, Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Ltd, Margaret Karume na Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa benki hiyo, Gift Shoko. 

Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Balozi, Mohamed Ramia Abdiwawa akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa tawi jipya la benki ya NCBA lililopo jengo la Muzamil mtaa wa Mlandege, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko (wa pili kushoto) akiongoza matembezi ya uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo lililopo jengo la Muzamil, mtaa wa Mlandege, Zanzibar. 


Mkurugenzi Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Ltd, Margaret Karume akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa tawi jipya la benki ya NCBA lililopo jengo la Muzamil mtaa wa Mlandege, Zanzibar.

Friday, 25 September 2020

CRDB BANK SLASHES AGRICULTURAL LOAN INTEREST RATES

The Minister for Agriculture, Japhet Hasunga (fourth right), cuts a ribbon to launch the agri-equipment loan that is jointly implemented by CRDB Bank, the lender in collaboration with ETC Agro, LoanAgro and Agricom, the suppliers of farm machines in Dar es Salaam recently, an initiative poised to benefit farmers by enabling them to get affordable loans for agricultural equipment including tractors, power tillers and harvesting machines. Fourth left is CRDB Bank Managing Director, Abdulmajid Nsekela, and third left is Agricom Managing Director, Angelina Ngalula. Extreme right is the Bank's Director of Retail Banking, Boma Raballa.
CRDB Bank has slashed agricultural loan interest rates and removed collateral for farming machines.

The Lender said that the rate dropped from 20 per cent to 18 per cent in a move aimed at empowering farmers to increase their capital base and expand their businesses.

Continue Reading >>>

AUGUST 2020 PROGRESS VIDEO - STANDARD GAUGE RAILWAY LINE FROM DAR ES SALAAM TO MOROGORO

BENKI YA NCBA BANK TANZANIA LIMITED YAKABIDHI MALIWATO YA KISASA KWA KLABU YA GOFU LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko akikata utepe kuzindua rasmi Maliwato (Changing room) ya kike kwenye viwanja vya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam. Benki ya NBCA ilidhamini ukarabati wa Maliwato hayo ya kisasa ili kuwezesha wachezaji Gofu wa kike kupata sehemu nzuri ya kubadilishia mavazi yao. Wengine pichani kulia ni Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwoga, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Resolution Insurance, Maryanne Mugo na Meneja Mkazi nchini wa GardaWorld, Patrick Karimi.

Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwoga akifungua pazia la uzinduzi Maliwato ya kike kwa wachezaji Gofu wa klabu ya Lugalo jijini Dar es Salaaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko.
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Maliwato ya kike iliyofanyika klabu ya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwoga (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko (katikati) wakimkabidhi zawadi mchezaji wa Gofu wa klabu hiyo, Chiku Elias aliyejishindia kwa kuwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Chairman Trophy yaliyowashindanisha wachezaji wanawake wa klabu ya Lugalo.
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko (kulia) akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwoga kwenye hafla ya uzinduzi wa Maliwato ya kike kwenye klabu ya Gofu Lugalo.