Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (katikati) akiwa ameshikilia mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 6.7 bilioni ikiwa ni Gawio la Serikali kutoka Benki ya CRDB. Jumla ya Gawio ni TZS 9.9 bilioni kwa Serikali Kuu, Halmashauri, Taasisi na Mashirika ya Umma ambayo ni Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSF, NSSF, GEPF na ZSSF) - TZS 2.6 bilioni, TAMISEMI (Halmashauri za Mbinga, Lindi, Shinyanga) - TZS 133.7 milioni, Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) - TZS 243.5 milioni, Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Tabora - TZS 228 milioni. Wengine pichani kutoka kushoto ni Balozi wa Denmark nchini, Einar Jensen, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu. Hafla hiyo imefanyika Juni 15, 2019 katika ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma. |
No comments:
Post a Comment