Wanahabari wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya 'Amsha Ndoto'. |
Kampeni itaendeshwa kwa miezi mitatu, kuanzia 27 Juni 2019 hadi 27 Septemba 2019 na itahusisha wateja wa zamani na wapya ikijikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti(kwa ajili ya kila mmoja) na Watoto Akaunti(kwa ajili ya watoto tu).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa ABL, Charles Itembe, Ili kustahili kupokea zawadi, wateja wanapaswa kuwa na akiba yenye thamani ya TZS 1,000,000 kwenye akaunti zao na kuendelea ili kuwawezesha kustahili kuingia kwenye fainali ya droo na hatimaye kuweza kushinda. Washindi wa 3 watapatikana kila mwezi. Kupitia kampeni hii wateja wataweza kujishindia mpaka mara mbili ya kiwango walichoweka kwenye akaunti, ambapo kiwango hiki cha zawadi huweza kufikia mpaka Shilingi milioni Tatu