Kupitia Chama Cha Wamachinga Mkoa wa Arusha, tarehe 26/06/2019 kampuni ya Tigo kupiti kitengo chake cha Tigo Business imetoa simu 247 pamoja wa miavuli 100 kwa wateja wake ambao ni wanachama wa umoja huo wa wafanya biashara wadogo wadogo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwakabidi vifaa hivyo kwa wateja hao 247, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo alisema, zawadi hizo ni utaratibu wa kawaida wa kampuni hiyo kuwazawadia na kuwashukuru wateja wake waliopo kwenye vikundi na unalenga kuboresha biashara zao pamoja na mazingira wanayofanyia kazi.
“Leo kampuni ya Tigo inayofuraha kukabidhi vifaa hivi kwa wateja wetu ambao ni wanachama wa Umoja wa Wamachinga hapa mkoani Arusha. Ni utaratibu wetu wa kawaida kuwapa zawadi wateja waaminifu kama hawa na tunaamini vifaa hivi vitawasadia kuboresha biashara zao huku wakifurahia huduma bora kutoka Tigo,” alisema
Lilian alifafanua kuwa, kampuni ya Tigo hutoa zawadi mbali mbali ikiwamo simu za mkononi kwa wateja wa malipo ya baada waliopo kwenye vikundi na ambao hutumia huduma za Tigo wakiwa na mkataba wa miezi 12 au 24.
Ili mteja aweze kunufaika na zawadi hizi anatakiwa kujiandikisha kama mteja wa walipo ya baada (postpaid) na ni lazima awe katika kikundi au kampuni kubwa AU ndogo. Hivyo basi, tunakaribisha vikundi, makampuni pamoja na taasisi kwa ajili ya kupata huduma zetu nzuri na za uhakika za mawasiliano.
Meneja huyo pia aliwataka wanafuaika wa zawadi hizo kuendelea kutumia mtandao wa Tigo na kuongeza kuwa Tigo inajali na kuwekeza kwa wateja na wabia wake wa biashara ili kuhakikisha kuwa watanzania wote wawanufaika na huduma bora za mawasiliano.
No comments:
Post a Comment