Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 25 June 2019

PROF. PALAMAGAMBA KABUDI AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na ujumbe wake akiwa kwenye mkutano pamoja na mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa mambo ya nje wa China na Mjumbe wa Baraza la Taifa, Mhe. Wang Yi na ujumbe wake. Mkutano huo umefanyika Beijing, China tarehe June 24, 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiteta na mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa mambo ya nje wa China na Mjumbe wa Baraza la Taifa, Mhe. Wang Yi mara baada ya kumaliza mkutano baina yao. Mkutano huo umefanyika Beijing, China tarehe June 24, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini mkataba wa msaada wa shilingi bilioni sitini bila ya masharti yeyote. Pembeni yake ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la China, Bw. Zhou Liujun, akisaini kwa niaba ya serikali ya China. Zoezi hilo limefanyika Beijing, China tarehe June 24, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akibadilishana nyaraka na Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la China, Bw. Zhou Liujun, mara baada ya kusaini nyaraka hizo. Zoezi hilo limefanyika Beijing, China tarehe June 24, 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi 53 za Afrika na Taasisi za Fedha za China.
Sehemu ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Wajumbe wao waliohudhuria katika mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi 53 za Afrika na Taasisi za Fedha za China.

No comments:

Post a Comment