Akizungumza katika uzinduzi huo katika kata ya Idete, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo, Aloyce Kwezi, aliwakaribisha na kuwashukuru Tigo kwa kuongeza ufanisi wa mnara huo kutoka teknolojia ya 2G hadi 3G.
Serikali ya Tanzania imefanya suala la viwanda kuwa agenda yake kuu. Na sisi kama serikali tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika kufanikisha hii dira. Tunapenda kuwashukuru sana kwa kuifikiria Kilolo na wananchi wake, maana sekta hii ya mawasiliano ni chachu kubwa sana katika ukuaji na ubunifu wa viwanda mbalimbali,” alisema Kwezi.
Kwa upande wake, Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini, Abbas Abdurahamani, alisema kwamba kipaumbele ya Tigo ni kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma za kisasa za kiteknolojia za simu kama ya 3G.
Uzinduzi wa leo unaofanyika Kilolo ni mwanzo wa kampeni ya nchi nzima ambapo kutakuwa na uzinduzi wa minara 52 kutoka Tigo zitakazo zinduliwa kutoka kanda ya Ziwa, Kaskazini, Pwani na Kusini.
Uzinduzi wa minara uaenda sambamba na ofa maalum. Wateja ambao watahudumiwa na minara ambayo imeongezewa uwezo kutoka 2G hadi 3G. Wateja watazawadiwa kiasi cha MB 100 za data kila mara watakaponunua kifurushi chochote cha intaneti. Huku wateja katika maeneo ya minara ya 4G itakayozinduliwa, watazawadiwa GB 4 za data bure pale wanapobadilisha laini zao za simu kuingia 4G.
“Kuongeza ubora wa mnara huu kutoka 2G kwenda 3G ina maana kwamba wateja wetu wa Kilolo sasa wataweza kupata huduma rahisi na kasi zaidi. Kwa mfano, 3G itaweza kuwapatia huduma ya intaneti iliyo bora ambayo itafungua jamii zilizopo vijijini kuweza kupata huduma za kielektroniki katika nyanja za kibiashara, afya, elimu na serikali ambazo walishindwa kupata huko nyuma. Jambo hili litabadilisha namna watu watakavyojifunza na kufanya biashara,” alisema Abdurahamani.
Abdurahamani pia alisisitiza kuhusu kazi ambayo Tigo inafanya kuwezesha sera ya TEHAMA ya Taifa na kuunga jitihada ya serikali katika viwanda kwa kupanua na kuboresha wigo wa mtandao ili kuwezesha nchi kufaidika katika nyanja mbali mbali za kijamii kama uchumi na elimu kupitia mfumo wa kidijitali.
Minara mengine ambayo imeboreshwa na zitazinduliwa hivi karibuni katika Kanda ya Kusini ukiondoa Kilolo zinapatikana katika maeneo ya Sumbawanga, Katavi, Mufindi, Njombe, Songwe, Mbeya and Songea.
No comments:
Post a Comment