Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 17 August 2018

MAKAMU WA RAIS, MHE SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIIKALI WA SADC WANAOUNDA UTATU WA ASASI YA USHIRIKIANO WA SIASA, ULINZI NA USALAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wanaounda Utatu wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama uliofanyika mjini Windhoek, Namibia tarehe 16 Agosti 2018. Kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda wakifuatilia mkutano.
Wajumbe wa Serikali ya Tanzania na Zambia wakifuatitilia hafla ya ufunguzi wa mkutano. Kulia kwa Makamu wa Rais ni Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Edgar Chagwa Lungu. 
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, Dkt. Stergomena L.Tax (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano. Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Namibia na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama.
Mhe. Makamu wa Rais akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Joseph Kabila kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huu pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018.

Mkutano huu umehusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wanaounda Utatu huo ambao ni Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço, Rais wa Angola na Mwenyekiti wa sasa wa SADC organ; Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu, Rais wa Jamhuri ya Zambia na Makamu Mwenyekiti wa SADC Organ na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa SADC Organ aliyemaliza muda wake.

Mkutano huu umejadili taarifa ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita wa Agosti 2017 hadi Agosti 2018.

Continue Reading

No comments:

Post a Comment