Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 20 June 2017

HUU NI ZAIDI YA UKARIMU KUTOKA KWA VODACOM TANZANIA FOUNDATION

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Marwa iliyoko Mikindani Mtwara wakijiandaa kupata futari mwishoni mwa juma. Vodacom pia wamekuwa wakitangaza maeneo ambayo yatafuatia kuturishwa katika muendelezo wa kampeni ya Ukarimu.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea yatima cha Mwinyi Baraka cha Misugusugu Kibaha mkoani Pwani, wakimsikiliza Glori Mtui ambaye ni mfanya kazi wa Vodacom Tanzania PLC wakati wakati wa futari iliyoandalia na Vodacom Tanzania Foundation kwa watoto hao kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kampeni ya Ukarimu wa Vodacom imendeelea kuwafikia watanzania maeneo mbalimbali nchini Tanzania na kuwafuturisha katika mfungo huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo kampeni hiyo ina lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku.

Huduma hii pia ina lengo la kuendeleza mshikamano inawawezesha Waislamu na Watanzania kwa ujumla kujiunga na kifurushi kinachowapatia muda wa maongezi, SMS na kuwawezesha kupiga simu BURE wakati wakisubiri muda wa kula daku, kugawa tende pamoja na maji. Pia huduma hiyo inawakumbusha muda wa kuswali na kuwapatia Mawaidha na Hadith. Ili kujiunga na huduma hii mteja anapiga *149*01# kisha anachagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha, kuna bando linalodumu kwa saa 24 na lingine linadumu kwa siku 7.

No comments:

Post a Comment