Afisa mdhibiti wa Rasilimali watu wa kampuni ya Zantel -Zanzibar
Said Habibu akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa
kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi
hilo limefanyika jana mjini Unguja. (Kushoto) ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu
kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Mohammed Ali
akijiandaa kuchangia damu katika zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa
kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya
watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana mjini
Unguja. (Kushoto) ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu
Salama-Zanzibar.
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel-Zanzibar Isaka Ali
akichangia damu katika zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa
upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji
mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo
limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar
Gabriel Laurent.
Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kampuni ya Zantel-Zanzibar, Mohammed
Musa Baucha akijiandaa kuchangia damu wakati wa zoezi hilo la hiari lililoandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ni njia ya
kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo, limefanyika jana mjini
Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar Gabriel
Laurent.
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Kassim Bakari
Zuberi akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni
hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye
uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo
limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar
Gabriel Laurent.
Katika kuisaidia benki ya damu hapa nchini,
wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar wamejitokeza kwa wingi na kujitolea kuchangia damu
katika kuendeleza mwitikio huo kwa jamii ulioanzishwa na Kampuni hiyo wiki
iliyopiata katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam.
Zoezi hili ambalo linaratibiwa na Kitengo
cha uwajibikaji kwa jamii (CSR) cha Kampuni hiyo, limelenga kusambaza upendo kupitia
shughuli hii ya uchangiaji damu ili kuiwezesha benki ya damu sambamba na kuokoa
maisha ya Watanzania wenzetu.
Shughuli hiyo ya uchangiaji
iliyofanyika katika makao makuu ya Ofisi za Zantel-Zanzibar, ilishuhudia
mwitikio mkubwa kutokana na wingi wa wafanyakazi wa Zantel kujitokeza, pamoja
na baadhi ya wananchi wakishiriki kuchangia damu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la
uchangiaji damu, Mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Musa
Baucha aliwashukuru watu wote walioshiriki na kutoa rai kwa makampuni
mbalimbali pamoja na wananchi kuwa tayari kujitolea kwenye shughuli kama hizo
wanapotakiwa kufanya hivyo.
“Tunayo furaha kwa mwitikio huu wa
kukubali kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu kwa kuonyesha upendo hususan wafanyakazi
wa Zantel Zanzibar. Niwaombe muendelee na moyo huu huu wa kujitolea pindi mnapohitajika
kushiriki kwenye shughuli nyingine kama hizi,”alisema.
Kwa upande wake, Afisa Uhamasihaji wa
Mpango wa damu salama Zanzibar Bw. Omar Said Omar alisema kwamba zoezi la
uchangiaji damu limefanyika kwa mafanikio makubwa na amefurahishwa na moyo wa
kujitolea ulioonyeshwa na wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar.
Hata hivyo aliongeza
kuwa, bado mahitaji ya damu ni makubwa ikilinganishwa na kiwango kilichokusanywa
ambapo kwa mwaka huu wa 2017 walijiwekea lengo la kukusanya chupa 12,000.
Alisema kwamba shughuli ya kukusanya damu
ni zoezi endelevu la kujitolea, benki ya damu imekuwa ikiomba makampuni na
jamii kwa jumla kutambua umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya
wananchi.
“Ni watu wachache sana ambao wamekuwa
wakijitokeza kuchangia damu, hivyo tunaamini kuwa zoezi hili litaendelea kuwahamasisha
watu wengi kujitokeza kushiriki,” alisema.
Kuhusu Zantel
Mtandao
wa Mawasiliano wa Zanzibar (Zantel) ni miongoni mwa wawekezaji na wagunduzi
kwenye sekta ya mawasilino wakiongoza kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Lakini zaidi ya yote, ni miongoni mwa kampuni ya mawasilino inayokuwa kwa kasi
kubwa na inayotengeneza faida kubwa katika Sekta ya mawasiliano Tanzania.
Mtandao huu wa Mawasiliano Zanzibar ndiyo mtandao pekee wa huduma za mawasilino
unaotoa huduma ya simu za nje kwa bei nafuu, simu nab ado kupitia mfumo bora wa
CDMA, GSM, 3G networks.
Huduma
za Zantel zimekuwa zikikua kutokana na kuongezeka watumiaji wake huku ikizidi
kuonyesha ubora katika huduma zake ambazo kila mtu anaweza kuzimudu pamoja na
kutoa huduma ya haraka ya mtandao wa wireles kwa haraka na ubora.
Zantel
imepokea tuzo mbalimbali kutokana na kutambuliwa kutoa huduma bora na ufumbuzi
kwenye sekta ya mawasilino. Baadhi yake ni pamoja na Tuzo ya GSMA M – Health.
Zantel imedhamiria kuwaunganisha watu ulimwenguni ili wawe mstari wa mbele
kupata tarifa kwa haraka.
Kwa
maelezo zaidi tafadhali, tembelea mtandao wetu…www.zantel.com
No comments:
Post a Comment