Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Stanbic Bank Banner_201026

Absa Banner_170926_270926_101026_201026

Absa Banner_170926_270926_101026_201026

Tuesday, 20 October 2026

BENKI YA CRDB, GAVANA WA BOT WANG’ARA TUZO ZA GLOBAL FINANCE BANGKOK, THAILAND

Bangkok, Thailand - Tanzania imeendelea kupeperusha vyema bendera yake kimataifa baada ya Benki ya CRDB kutangazwa kuwa Benki Bora Tanzania kwa mwaka 2026 (Best Bank in Tanzania) na jarida maarufu la kimataifa la Global Finance, katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika jijini Bangkok, Thailand.

Katika hafla hiyo, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, naye ametambuliwa kimataifa kupitia tathmini ya Global Finance ya Central Banker Report Cards 2026, na kuongeza heshima kwa sekta ya fedha nchini Tanzania.

Utambuzi huo unaakisi maendeleo na mageuzi yanayoendelea katika sekta ya fedha nchini. Kwa upande wa Benki ya CRDB, tuzo hiyo inaonesha kutambuliwa kwa uimara wa benki hiyo, ubunifu katika huduma za kifedha, ukuaji wa biashara pamoja na mchango wake katika kukuza ujumuishaji wa kifedha na maendeleo ya uchumi.

Mafanikio hayo yanakuja katika wiki ambayo Benki ya CRDB pia iliandaa Kongamano la Uwekezaji Afrika (Africa Investor Forum) 2026 jijini Bangkok, Thailand, na kufanikisha makubaliano ya ufadhili yenye thamani ya dola za Marekani milioni 111 kutoka taasisi za fedha za kimataifa.

Ufadhili huo unalenga kuchochea biashara, uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania na barani Afrika, ukiimarisha nafasi ya Benki ya CRDB katika kuunganisha wawekezaji na fursa za uwekezaji katika ukanda huo.

Kutambuliwa kwa Benki ya CRDB na Gavana Tutuba katika jukwaa hilo la kimataifa ni hatua inayoongeza mwonekano wa Tanzania katika sekta ya fedha duniani na kuonesha umuhimu wa taasisi imara za kifedha katika kukuza uchumi.

Hongera Benki ya CRDB! Hongera Gavana Emmanuel Tutuba! Hongera Tanzania!


Fuata Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari, uchambuzi na taarifa za hivi punde kuhusu sekta ya benki, fedha, biashara na uwekezaji.

Mitandao yetu ya kijamii:



No comments:

Post a Comment