Meneja Miradi na Biashara DSE, Patrick Mususa
Kwa ufupi
Ripoti ya wiki ya soko hilo
inabainisha kushuka mauzo kwa asilimia 91, huku idadi ya hisa zilizouzwa
zikishuka kwa asilimia 94.
Dar es Salaam. Hali siyo nzuri katika Soko la Hisa la
Dar es Salaam (DSE) baada ya mauzo kuporomoka kwa kishindo huku idadi ya hisa
ikishuka.
Mauzo hayo yamepungua kutoka Sh32.5 bilioni wiki iliyopita
mpaka Sh3 bilioni kwa juma lililoishia Oktoba 13, baada ya hisa zilizouzwa
kushuka kutoka milioni tisa mpaka 500,000.
Meneja Miradi na Biashara wa DSE, Patrick Mususa alisema
hali hiyo ni ya kawaida na inadhihirisha uhuru wa soko kwa wawekezaji wa ndani
na nje na kwamba, hakuna kampuni au mtu anayeweza kupanga mwenendo wake.
No comments:
Post a Comment