Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 4 May 2016

TIGO 4G LTE YAINGIA KWENYE MIJI 5 KANDA YA ZIWA

Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa Tigo kusambaza mtandao wa 4G lte nchi nzima. Pembeni yake ni Afisa Mkuu wa Ufundi wa teknolojia ya mawasiliano wa Tigo Jerome Albou katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama Jijini Dar es salaam.

Waandishi wa habari wakichukua taaarifa
Dar es Salaam, Mei 4, 2016 - Kampuni ya simu ya Tigo ambayo inaendesha maisha ya kidijitali Tanzania imetangaza kuzinduliwa kwa huduma ya 4G LTE katika miji mingine mitano ya kanda ya ambayo ni Tabora, Musoma, Bukoba, Kigoma na Shinyanga.

Kampuni hiyo awali ilizindua huduma hiyo jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa mwaka jana na baadaye kuisambaza katika miji ya Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na Mwanza na hivyo kuifanya kuwa kampuni ya simu yenye mtandao mpana na wa kasi wa 4G LTE nchini Tanzania.

Ikiwa inachukuliwa kuwa ni teknolojia nzuri na ya uhakika katika sekta ya mawasiliano ya simu duniani ya kupata intaneti, kasi ya teknolojia ya 4G LTE ni takribani mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G na Tigo inaifanyia kazi kwa kina ili kuongeza ubora wa huduma hiyo na mtandao wa 4G kutokana na matumizi ya wateja kuwa nayo yanaongezeka kwa kasi kubwa.

Hivi sasa Tigo ina timu inayofanya kazi saa zote kuimarisha na kukuza ubora wa teknolojia ya 4G. Matokeo yake ni kwamba mtandao wa 4G umekuwa unategemewa kwenye miji ambamo upo (Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na Mwanza).

Mtandao wa 4G LTE unatoa intaneti ya kasi ya kurambaza (surf) na kupakua vitu, kufanya miito ya simu ya kuonana (Skype) isiyo na kikomo. Kutokana na uzinduzi wa hivi karibuni wa video za bure kupitia YouTube nyakati za usiku, mtandao wa 4G LTE unawawezesha wateja kwa kiwango kikubwa kupata uzoefu wa kutiririsha video zilizo na uangavu mkubwa. Aidha kutokana na ushirikiano na Facebook mteja wetu wa 4G pia anaweza kufurahia kutiririsha video zilizomo kwenye mitandao maarufu ya kijamii duniani.

Pia, mteja akiwa na 4G LTE anaweza kupakua mafaili makubwa (sinema, mafaili yanayohusiana na kazi) au vifaa na hali kadhalika kucheza michezo kwa njia ya mtandao.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez, alisema mpango wa kupanua teknolojia ya 4G hadi kwenye maeneo yote ya nchi upo mbioni ambapo kampuni hiyo imejikita kwenye kuwapa wateja wake huduma zenye ubora duniani ambazo zitawawezesha kufurahia mtindo wa maisha ya kidijitali.

“Kupanua mtandao wa 4G LTE nchi nnzima kwa mara nyingine kunaonesha sio tu Tigo kuongoza kwenye kutoa teknolojia na ubunifu wa kisasa ndani ya soko bali pia kusisitizia kujituma kwetu katika kuongeza fursa ya kufikia intaneti kwa Watanzania walio wengi kwa kadri iwezekanavyo,’ alisema Gutierrez.

Kwa mwaka huu 2016, Tigo itawekeza zaidi ya dola milioni 75 kwenye upanuzi wa mtandao na kuimarisha ubora wake kwa kukuza maeneo ya teknolojia ya 4G na 3G, mkongo wa mawasiliano na hali kadhalika kuongeza idadi ya sehemu za kutolea huduma kwa wateja nchi nzima.

“Tukiwa kama kampuni tunatambua umuhimu wa wa ubora na ukaribu kwa wateja wetu na tunafanya kazi ili kufikia malengo hayo katika siku za karibuni,” alisema Gutierrez.

“Hivi sasa pia tuna programu ya kufanya mtandao kuwa wa kisasa ambao unajumuisha kuongeza uwezo wa 4G kwenye miji yote 12 ambako tuna mtandao wa 4G pamoja na kuongeza mtandao wa 3G kufika maeneo yote nchini,” alisema Gutierrez na kuongeza kuwa wateja wa Tigo katika miji ya Mbeya, Mtwara na Lindi wajitayarishe kufurahia huduma ya Tigo 4G LTE itakayoanza kutolewa siku za hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment