Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Friday, 16 October 2015
FASTJET, EMIRATES WAINGIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA
Dar es Salaam Oktoba 13, 2015 - Katika hatua ya kuhakikisha kuwa wateja wake wanaunganishwa na usafiri wa kimataifa, kampuni ya ndege ya kiafrika yenye gharama nafuu fastjet Tanzania imesaini makubaliano ya ushirikiano na shirika kubwa la ndege la Kimataifa Emirates.
Kupitia makubaliano hayo ambayo yanaanza rasmi Oktoba 15, 2015, Emirates kwa upande mwingine watanufaika kutokana na abiria wake kuweza kufikia mtandao wa njia wa fastjet ambao unakua ndani katika eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Akitangaza kusainiwa nkwa makubaliano hayo, meneja mkuu wa fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati alisema kuwa abiria wa Emirates hivi sasa wataweza kukata tiketi za fastjet kutoka kwenye mitandao yote ya Emirates kwa kutumia mtandao wa kompyuta uliounganishwa baina ya mashirika hayo mawili.
Kibati alisema, “Tunayo furaha kubwa kufanya kazi na shirika la ndege linaloheshimika na lenye mafanikio duniani. Sio tu kwamba hali hiyo itatuwezesha sisi kuwafikia mamilioni ya abiria ambao husafiri na Emirates bali pia ni uthibitisho mkubwa wa uendeshaji wetu makini, ubora wa huduma na bei zetu nafuu. Tunatarajia kusalimiana na abiria wa Emirates watakaokuwa wamepakia kwenye ndege zetu.”
Kibati aliongeza, “ubia wetu utaenda mbali kutunufaisha sote fastjet na Emirates na kutuhakikishia usafirishaji mkubwa wa abiria na utawapa wasafiri ndani ya Afrika fursa ya kuunganika na sehemu nyingine ulimwenguni kupitia kituo kikuu cha Emirates cha Dubai, ambapo Fastjet itaingiza abiria kituoni hapo kutoka miji na majiji ya Afrika.
Emirates ni shirika kubwa la ndege la kimataifa lenye makao yake makuu Dubai katika Himaya za Muungano wa Imarati. Hivi sasa Emirates linafanya safari hadi kwenye vituo 140 duniani vikiwemo 20 ndani ya Afrika, wakati Fastjet ni kampuni ya ndege inayoongoza ya kiafrika inayokuwa kwa kasi na yenye gharama nafuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment