Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 30 July 2015

TIGO YAZINDUA DUKA JIPYA IFAKARA

Katibu tawala wilaya ya Kilombero ndugu Yahya Naniya akikata utepe ikiwa ni ishara rasmi ya uzinduzi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini, kutoka kushoto ni meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya pwani, Isack Shoo, Inspekta Dotto Ngimbwa kutoka ofisi ya OCD Kilombero na mwisho kulia Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki Goodluck Charles.
Wafanyakazi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini wakipozi kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi aliyevaa tai nyekundu ndugu Yahya Naniya ambae ni Katibu tawala wa wilaya ya Kilombero, muda mfupi baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo.
Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya pwani, Isack Shoo akitoa maelekezo jinsi watakavyo hudumia wateja kwa mgeni rasmi Katibu tawala wa wilaya ya kilombero ndugu Yahya Naniya baada ya uzinduzi wa duka hilo lililopo Ifakara mjini.
Muonekano wa duka jipya kwa wateja wa Tigo lililopo Ifakara mjini.
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa duka la Tigo Ifakara mjini ndugu Yahya Naniya ambae ni Katibu tawala wa wilaya ya kilombero (wapili kutoka kulia) akiwa katika meza kuu na Goodluck Charles Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki (wa pili kushoto) Inspekta Dotto Ngimbwa kutoka ofisi ya OCD Kilombero (kushoto) na Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya pwani Isack Shoo (kulia).


No comments:

Post a Comment