Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 6 July 2015

BENKI YA NBC YANDAA FUTARI KWA WATEJA WAKE JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Edward Marks (katikati, mwenye suti nyeusi) akishiriki mlo wa futari waliyowaandalia wateja wao na wageni wengine waalikwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Kaimu Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Bin Zubeir Bin Ali, Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein na kushoto kwa mkurugenzi ni Ofisa Fedha Mkuu wa benki hiyo, Jaffari Matundu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC Tanzania, Dk. Kassim Hussein (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Bin Zubeir Bin Ali (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Edward Marks (katikati, mwenye suti nyeusi) na Ofisa Fedha Mkuu wa NBC, Jaffari Matundu (kulia) katika hafla ya futari waliyowaandalia wateja wao na waalikwa wengine jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Edward Marks (wa pili kushoto), akimkaribisha Kaimu Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Bin Zubeir Bin Ali katika hafla ya futari waliyowaandalia wateja wao na wageni wengine waalikwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rejareja wa Benki ya NBCTanzania, Isidory Shirima (wa pili kushoto) akishiriki kuchukua mlo wa futari katika hafla waliyowaandalia wateja wao na wageni wengine waalikwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC, Eddy Mhina (katikati) akifanya mahojiano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari akizungumzia maendeleo ya huduma za kibenki za NBC zinazofuata kanuni na misingi ya Kiislamu (Islamic Banking). Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein.
Baadhi ya wateja wa NBC na wageni waalikwa wakichukua futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC.
Baadhi ya wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na waalikwa wengine wakijumuika kushiriki mlo wa futari ukiuoandaliwa na Benki ya NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment