Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday, 24 May 2015

SAGCOT YAWATAKA WANAOMALIZA VYUO VIKUU KUCHANGAMKIA AJIRA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Dk. Rehema Nchimbi akifungua kikao kazi cha biashara ya kilimo kwa kongani ya Ihemi iliyoandaliwa na SAGCOT (Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania) kwa ushirikiano na UONGOZI Institute (Taasisi ya Uongozi Afrika kwa Maendeleo Endelevu) mapema jana Iringa mjini. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kilimo wa TCCIA Bi. Magadalena Mkocha, Mwenyikiti wa Bodi ya Agricultural Council of Tanzania Dk. Sinare Y. Sinare, DC wa Iringa Mh. Angeline Mabula, DC wa Mufindi Mh. Mboni Mhita na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Philemon Luhanjo.
Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Bw. Geoffrey Kirenga akitoa utangulizi wa mada ya biashara ya kilimo kwa nyanda za juu kusini. Mkutano huo wa siku mbili ulikutanisha viongozi wa serikali, sekta binafsi, mashirika ya kimataifa pamoja na wakulima kwa ajili ya kujadili kuhusu kuboresha biashara ya kilimo nchini kwa nyanda za juu kusini hususan kongani mwa Ihemi Iringa na Njombe.

No comments:

Post a Comment