Dar es Salaam. Mei 20, 2015 - Benki ya NMB imezindua rasmi tawi jipya kwaajili ya wateja maalum wa NMB kwa jiji la Dar es Salaam. Tawi hilo ni maalum kwa wateja wakubwa na wa kati wenye kadi maalum. Tawi jipya la NMB Oyster Plaza lipo kwenye jengo la Oyster Plaza, Oysterbay, barabara ya Haile Selassie.
Tawi hili ni maalum kwa wateja na wafanyabiashara wakubwa na litatoa huduma kwa mteja kwa njia ya mtu mmoja mmoja kupitia Mameneja na Maofisa Mahusiano wa kibiashara ambao wataweza kuwasiliana moja kwa moja na mteja na kumpa msaada wa huduma anayoitaka.
|
No comments:
Post a Comment