Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mh. Dk. Perseko Vincent Kone akipata maelezo kuhusu huduma na bidhaa zinazo tolewa katika tawi hilo kutoka kwa Meneja wa NMB tawi la Singida, Bi. Christine Mwangoma. |
Kufunguliwa kwa tawi la Singida sasa kutaharakisha maendeleo ya wakazi wa Mkoa wa Singida na pia kurahisisha biashara kati ya wananchi wa mji huo na wa maeneo ya jirani.
Hii ni kwa sababu NMB sasa inawezesha wateja wake kuuza, kununua, kutuma na kupokea fedha za kigeni popote ulimwenguni tena kwa gharama nafuu. Kwa hili biashara itaimarika na ubadilishaji wa fedha za kigeni utakuwa rahisi kupita hapo awali, hasa tukifahamu kua Singida ni sehemu ya biashara na wafanyabiashara mbali mbali hutembelea mkoa huo.
Kwa kutambua pia nia ya kuendelea kuchangia huduma mbali mbali za kijamii, benki ya NMB imetoa shilingi Milioni 25 kwa ajili ya hospitali na shule kama shukrani za Benki kwa wananchi wa Singida kwa kuendelea kwao kuunga mkono maendeleo ya benki.
NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 160, ATM zaidi ya 600 nchi nzima pamoja na idadi kubwa ya wateja.
No comments:
Post a Comment