Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 18 February 2015

AFISA MTENDAJI MKUU WA TTCL, AFANYA ZIARA MIKOA YA KUSINI NA NYANDA ZA JUU KUSINI

Afisa Mtendaji Mkuu Dr Kamugisha Kazaura atembelea mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Mbeya ikiwa na lengo la kukagua miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TTCL wa mikoa hiyo.

Dr Kazaura ailijionea juhudi mbalimbali zinazofanywa na wafanyakazi wa TTCL katika kuhakikisha miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inakuwa salama muda.

Hivi sasa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imekuwa kampuni pekee ya mawasiliano ambayo imefanikiwa kuunganisha wateja mbalimbali kupitia mtandao wake.

Wateja hao ni pamoja na TAMISEMI, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mabenki, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG), Wizara ya Fedha, watoa huduma za mtandao/intaneti (ISPs) pamoja Makampuni ya Simu

Pia TTCL imefanikiwa kuunganisha nchi jirani katika ukanda huu wa afrika Mashariki (Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda) pamoja na nchi za kusini wa Jangwa la Sahara (SADC) ambazo ni Malawi na Zambia.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua mitambo ya TTCL mkoani Lindi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akipokea maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa TTCL Mtwara kuhusu juhudi zinazofanyika kulinda na kusimamia mitambo yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua Mtambo wa Mkongo wa Taifa, pembeni yake ni Mkuu wa Idara ya Ufundi wa TTCL,Senzige Kisenge.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na mafundi ambao wanajenga Barabara katika mkoa wa Ruvuma, akiwasisitiza walinde Mkongo wa Taifa.
Meneja wa TTCL mkoa wa Lindi, John Nindwa akimuonesha Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura eneo ambalo Mkongo wa Taifa ulikatwa na wezi katika hifadhi za Taifa ya Selous na juhudi zilizofanyika katika kurejesha mawasiliano Ruvuma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na wafanyakazi wa TTCL mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Ufundi Senzige Kisenge na Kushoto Mkuu wa Biashara Nyanda za juu Kusini, Juvenal Utafu.

No comments:

Post a Comment