Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Steven Gannon akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya kinywaji kipya cha pombe kali aina ya Jebel Coconut, mara baada ya uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Dar
es Salaam, Tanzania; KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) moja ya kampuni kubwa za
kutengeneza bia nchini na watengenezaji wa bia maarufu aina ya Serengeti
Premium Lager wametangaza rasmi kuzindua bidhaa yao mpya inayoitwa Jebel
Coconut.
Jebel ni kinywaji kipya aina ya pombe kali kilichobuniwa
Tanzania na kutengenezwa kwa ladha ya nazi, ambazo hupatikanan kwa kirahisi
hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi
wa kinywaji hicho jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
Mkuu wa SBL, Steve Gannon alisema, “Sisi tunayo furaha ya kuzindua bidhaa mpya
katika soko baada ya kufanya tafiti nyingi juu ya mahitaji ya wanywaji nchini
Tanzania na kubaini kuwa kuna pengo katika mahitaji yao.”
Jebel ilibuniwa hapa Dar es salaam kutokana na mandhari yake
ya ufukweni na ndio maana ya kuja na kauli mbiu ya “Full Kipupwe”. Kinywaji
hiki ni cha kwanza kubuniwa hapa nchini kati ya pombe kali zaidi ya 10 za
kimataifa zinazosambazwa na kampuni hiyo. Walengwa haswa wa kinywaji hiki ni watu
wazima wenye umri wa kati na SBL ina uhakika kwamba soko litaipokea vizuri
bidhaa hii kutokana na ladha, ubora na bei yake maradufu. Jebel ina ladha ya
kipekee na inaweza kunyweka kwa ilivyo au ikachanganywa na barafu na kwa
wengine soda ya tangawizi au ndimu.
Katika jitihada za kuhakikisha kuwa bidhaa inawafikia
wanywaji walengwa hivi karibuni, Mkurugenzi wa Masoko, Ephrahim Mafuru alisema,
"Hivi karibuni kutakuwa na shughuli nyingi ambazo zitampa nafasi mnywaji
wa kitanzania kupata ladha ya ukweli na uhakika kwa hiyo wanywaji wanaalikwa
kushiriki promosheni zitayofanyika katika baa mbalimbali na maduka ili kuwapa
nafasi wanywaji kujaribu ladha ya kipekee ya Jebel na
kupata zawadi kemkem.”
Kinywaji hiki kipya cha Jebel kitaletwa katika chupa yenye ujazo
wa 250ml na yenye rangi ya dhahabu, bluu na kijani kwa shilingi za kitanzania
3000 tu.
KUHUSU SERENGETI BREWERIES
LIMITED
Serengeti
Breweries Limited ni kampuni ya bia ambayo huandaa, kuzalisha na kuuza vinywaji
vilivyotengenezwa na shairi, ngano na mtama nchini Tanzania.
Kikiwa
na makao yake makuu jijini Dar es Salaam, SBL hutengeneza vinywaji vifuatavyo:-
Serengeti Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo
Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The Kick and Guinness®.
SBL pia
husambaza vinywaji mbalimbali vikali za kimataifa kama Smirnoff Vodka®, Johnnie
Walker®, Bailey’s Irish Cream ®, Richot®, Bond 7 Whiskey® and Gilbeys Gin®.
Serengeti
Breweries Limited ni kampuni mwenza ya East African Breweries Limited/ DIAGEO
PLC.
No comments:
Post a Comment