Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 24 September 2014

NBC WAKUTANA NA MAWAKILI WA MAKAMPUNI MBALIMBALI KWA LENGO LA KUFAHAMIANA

Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya NBC, Pius Tibazarwa, akizungumza katika hafla waliyowaandalia wanasheria kutoka makampuni mbalimbali ili kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kuwapa maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika kitengo hicho kilichopo ndani ya Jengo la Coco Plaza, Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya NBC, Pius Tibazarwa (katikati), akibadilishana mawazo na baadhi ya mawakili waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kukutana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.  Kushoto ni, Joseph Ngiloi na Protase Ishengoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia), akifurahi  na baadhi ya mawakili waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.  Kushoto ni, Joseph Ngiloi, Mkurugenzi Mtendaji wa muda wa NBC, Pius Tibazarwa na wakili Protase Ishengoma.

Meneja Mahusiano wa Wateja wa kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha Benki ya NBC, Subira Mwaya (kushoto) akiwa na Wakili wa Kampuni ya Summit Attorneys,  Bilal J. Bilal wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kufahamiana  na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (katikati), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla waliowaandalia wanasheria kutoka makampuni mbalimbali ili kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kuwapa maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. (Picha na Peter Mgongo).

No comments:

Post a Comment