Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Monday, 9 September 2024

VODACOM YATANGAZA WASHINDI WA DROO YA SITA YA KAMPENI YA NI BALAA!

Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania Plc, Joseph Sayi (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 20 kwa mshindi wa mwezi wa kampeni ya Ni Balaa! Amina Gwila mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Tawi la Dodoma mwishoni mwa wiki katika hafla iliyofanyika duka la Vodacom jijini Dodoma. Amina amepata nafasi ya kuchagua shule ambayo Vodacom watasaidia kukarabati maktaba yake ili kukamilisha adhma ya kusaidiana na Serikali katika kuboresha elimu nchini.
Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc Mkoa wa Dodoma, Balikulije Mchome (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/- mshindi wa droo ya sita wa kampeni ya Ni Balaa! Kila mtu ni mshindi, Bw. Peter Sheka katika duka la Vodacom lililopo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Endelea kufanya miamala kupitia M-pesa nawe uwe mshindi.
Afisa wa M-Pesa kutoka Vodacom Tanzania Plc, Mkoa wa Dodoma, Musa Kushoka (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/- kwa mshindi wa droo ya sita ya kampeni ya Ni Balaa! Kila mtu ni mshindi, Bw. Felician Mgimba (kulia) katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Endelea kufanya miamala na kununua vifurushi ili uweze kuibuka mshindi.
Afisa Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc mkoa wa Dodoma, Athumani Ngoma (kushoto) akimkabidhi mshindi wa wiki ya sita wa kampeni ya Ni Balaa! Kila mtu ni mshindi, Angel Bahingali (Kulia) mfano wa hundi ya shilingi 500,000/- katika duka la Vodacom lililopo jijini Dodoma mwishoni mwa mwiki Endelea kufanya miamala na kununua vifurushi kupitia M-pesa ili uweze kuibuka mshindi.

MSMEs PLAY CRUCIAL ROLE IN TRANSFORMING FOOD SYSTEMS IN AFRICA


MSMEs Highlighted as a Force in Building Africa’s Food Systems in the Latest Leading Agriculture Report 

Tuesday, 4th September 2024: AGRA has launched its 2024 Africa Agriculture Status Report, titled "Harnessing the Private Sector for Food Systems Transformation in Africa." The report provides an in-depth analysis of the significant role that micro, small, and medium-sized enterprises (MSMEs) play in transforming food systems across Africa. 

Developed through extensive collaboration with a diverse group of stakeholders, it explores the vital contributions of MSMEs to agricultural and economic transformation on the continent. Dr. Agnes Kalibata, President of AGRA, stated, “The Africa Agriculture Status Report 2024 highlights the transformative role of MSMEs in shaping Africa's agrifood landscape. By harnessing the power of the private sector, we can drive meaningful food systems transformation and achieve sustainable growth. 

This report provides actionable insights on supporting MSMEs to enhance their impact on food security and economic development.” Dr. Kalibata further emphasized, “This report marks a significant milestone in understanding the private sector’s influence on Africa’s agrifood systems. It showcases the crucial impact of MSMEs in driving agricultural productivity and economic development. 

Saturday, 7 September 2024

DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE CEO MEETS WITH MINISTER FOR WATER

Dar es Salaam Stock Exchange CEO, Peter Nalitolela (R), met with Hon. Jumaa Aweso (L), Minister for Water, for a strategic discussion on harnessing capital markets to accelerate the development of Tanzania’s water sector. Their dialogue focused on fostering innovative financing solutions for water infrastructure projects, with an emphasis on sustainability and long-term water security. Both leaders expressed a strong commitment to collaborating on initiatives that leverage public-private partnerships and capital market instruments to drive transformative progress in Tanzania’s water resources, ensuring resilience and accessibility for future generations.


Friday, 6 September 2024

USIKOSE AFRICA CUP OF NATIONS KWA NGUVU YA BUKU 1O TU NDANI YA DStv


BENKI YA NMB YASHIRIKI MKUTANO MKUBWA WA MADINI AUSTRALIA


Benki ya NMB inashiriki katika mkutano mkubwa wa madini duniani, Africa Down Under, Perth, Australia unaomalizika leo.


Mkutano huu wa siku tatu unawakutanisha wadau wa sekta ya madini kutoka sekta ya umma na binafsi ikiwemo viongozi wa serikali, makampuni ya uchimbaji, wawekezaji na wadau wengine kujadili fursa zilizopo, sera na hali ya jumla ya sekta hiyo barani Afrika.


Mwaka huu, ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ambaye aliwasilisha mada kwa washiriki kuhusu utayari wa Tanzania kushirikiana na wadau wa Australia na mataifa mengine ili kuendeleza sekta hii inayochangia zaidi ya 9% katika pato la Taifa.


Katika mkutano huu pia, Waziri Mavunde, alieambatana na Balozi wa Tanzania nchini Australia na Japan, Mhe. Baraka Luvanda, alitembelea banda letu na kupokelewa na Mhazini wa Benki ya NMB, Aziz Chacha, ambaye alimfahamisha Mheshimiwa Waziri kuhusu jitihada za benki katika kutoa masuluhisho mahsusi ya kifedha kwa wadau wa sekta ya madini ili kuongeza mchango wa sekta hii katika uchumi wa nchi.


Waziri Mavunde amepongeza juhudi za Benki ya NMB katika kuimarisha sekta ya madini na kuwainua wadau katika mnyororo mzima wa sekta hii, huku akihimiza kuendeleza juhudi hizo hasa kwa wachimbaji wadogo na wa kati.


“Napongeza ushiriki wa Benki ya NMB katika mkutano huu mkubwa wa madini kati ya Australia na Afrika. NMB imetoa mikopo kwenye utekelezaji wa miradi hii kwa baadhi ya kampuni za Australia. Hii ni hatua nzuri ya kukuza sekta ya madini kupitia mchango wa taasisi za fedha,” amesema Mhe. Mavunde.




NBC YAJIDHATITI KUCHOCHEA UKUAJI WA BIASHARA TANZANIA - AFRIKA KUSINI

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF), Manish Thakrar (kulia) akizungumza na wanachama wa jukwaa hilo wakati wa mkutano wa jikwaa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa kwa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Kimataifa wa Benki ya NBC, Wilson Nkuzi (kushoto) na Meneja Uendeshaji Biashara wa benki hiyo NBC, Ester Bgoya (Katikati). Benki ya NBC ilikuwa mdhamini wa mkutano huo.
Mkuu wa Miamala na Amana za Wateja Wakubwa wa NBC, Jimmy Myalize (aliesimama) akielezea huduma mbalimbali za benki hiyo kwa wanachama wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF) sambamba na mchango wa benki hiyo katika kusaidia jamii hususani kupitia udhamini wake kwenye sekta mbalimbali mbali ikiwemo michezo na sekta ya afya.
Mkuu wa kwa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Kimataifa wa Benki ya NBC, Wilson Nkuzi (katikati) akielezea huduma za benki hiyo kwa wananchama wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF) wakati wa mkutano wa jikwaa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Benki ya NBC ilikuwa mdhamini wa mkutano huo.
Meneja Mahusiano ya Umma na Mawasiliano wa benki ya NBC, Brendansia Kileo (alieshika mic) akielezea huduma za benki hiyo kwa wananchama wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF) wakati wa mkutano wa jikwaa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Mahusiano ya Umma na Mawasiliano wa benki ya NBC, Irene Peter (alieshika mic) akielezea huduma za benki hiyo kwa wananchama wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF) wakati wa mkutano wa jikwaa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF) wakijadili masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa jikwaa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam - Septemba 6, 2024: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa wito kwa wafanyabaishara wa kitanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara baina ya Tanzania na Afrika kusini huku ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuchochea na kuwezesha biashara baina ya mataifa hayo mawili kupitia ukuzaji wa mitaji na urahisishaji wa miamala.


Wito huo umetolewa na Mkuu wa kwa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Kimataifa wa NBC, Bw Wilson Nkuzi wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF) uliofanyika jijini Dar es Salaam jana jioni.


Mbali na wanachama ambao ni wafanyabiashara baina ya mataifa hayo mawili hapa nchini, mkutano huo pia ulihusisha wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali, maofisa wa ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania pamoja na maofisa kutoka benki ya NBC ambayo ndio ilikuwa mdhamini mkuu wa mkutano huo.


Kwa mujibu wa Bw Nkuzi, kupitia huduma zake mbalimbali za kifedha ikiwemo mikopo ya ukuzaji mitaji, dhamana, huduma ya fedha za kigeni sambamba na huduma ya malipo kwa njia ya mtandao inayofahamika kama ‘NBC Connect’ benki hiyo imedhamiria kurahisisha zaidi ufanisi wa biashara kwa wafanyabiashara hao ili waweze kushiriki kwa ushindani zaidi kwenye fursa hiyo ya kimataifa.


“Kinachotupa msukumo zaidi katika jitihada hizi ni ongezeko kubwa la wafanyabiashara baina ya mataifa haya mawili ambao wamekuwa wakitumia fursa na huduma mbalimbali zinazotolewa na NBC mahususi kwao ikiwemo mikopo ya ukuzaji mitaji, dhamana, miamala ya kimataifa na zaidi huduma ya kubadilisha fedha za kigeni ambapo licha ya changamoto ya upatikanaji wa dola za Kimarekani nchini, NBC tunapambana kuhakikisha wafanyabaishara hawapitii changamoto hiyo,’’ alisema.

AGRICULTURAL FINANCING THROUGH CAPITAL MARKETS

Dar es Salaam Stock Exchange CEO, Peter Nalitolela (L), met with Hon. Hussein Bashe (R), Minister of Agriculture, to explore capital markets solutions that can fuel innovation, growth, and sustainability in Tanzania's agricultural sector. Together, we aim to empower farmers and agribusinesses through access to finance and investment opportunities.

Key takeaways from the meeting:

1) Agricultural Financing:

Exploring how the DSE can facilitate capital raising for the agriculture sector through debt or equity listings.

2) Empowering Farmers:

Ways to enhance access to financial markets for smallholder farmers and agribusinesses, promoting financial inclusion and sustainability.

3) Agri-Tech Innovation:

Collectively explore opportunities for funding agricultural technology (Agri-Tech) projects through the stock exchange to boost productivity and innovation.

4) Partnerships for Rural Development:

Collaborating on joint initiatives to increase rural participation in capital markets and improve economic outcomes for agricultural communities.

DAR ES SALAAM STOCK EXCFHANGE CEO MEETS HON. MOHAMED MCHENGERWA

Dar es Salaam Stock Exchange CEO, Peter Nalitolela (R), met with Hon. Mohamed Mchengerwa (L), Minister for President’s Office - Regional Administration and Local Governments, to discuss strategic partnerships aimed at enhancing financial inclusion and fostering economic development through Capital Markets.


Amongst other things, the discussed agenda included:

1) Financial Inclusion: Increasing participation in Capital Markets across the country, especially in underserved areas;

2) Collaborations with Local Governments: Leveraging Capital Markets to drive Alternative Financing initiatives for Regional and Local Government l-ed projects;

3) Capacity Building: Joint programs to improve financial literacy and investment knowledge at the local level;

4) Infrastructure Development: Making good use of Capital Markets, and the DSE in particular, to raise sustainable financing for medium to long-term projects.

Thursday, 5 September 2024

AFISA MTENDAJI MKUU WA SOKO LA HISA AJITAMBULISHA KWA WAZIRI WA FEDHA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salam (DSE) aliyefika kujitambulisha.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Dkt. Nchemba, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Peter Nalitolela, aliyefika kujitambulisha, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza kuhusu maendeleo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), alipokutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Peter Nalitolela, aliyefika kujitambulisha, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongoza mkutano kati yake na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Peter Nalitolela, aliyefika kujitambulisha, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Peter Nalitolela, (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka DSE baada ya Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE kujitambulisha kwa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

NBC YASAINI MoU KUTOA HUDUMA ZENYE UPENDELEO KWA WAFUGAJI

Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki ya NBC, Msafiri Shayo (kulia) na Katibu Mkuu wa CCWT, Mathayo Daniel (kushoto) wakionesha hati ya makubalino baina ya taasisi hizo mbili yanayolenga kufungua milango kwa benki ya NBC katika kutoa huduma za kifedha zenye upendeleo maalum kwa wafugaji pamoja na wadau wote waliopo kwenye mnyororo wa sekta hiyo nchini. Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam ikihusisha viongozi waandamizi kutoka pande zote mbili.
Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki ya NBC, Msafiri Shayo (kulia) na Katibu Mkuu wa CCWT, Mathayo Daniel (kushoto) wakisaini hati za makubalino baina ya taasisi hizo mbili yanayolenga kufungua milango kwa benki ya NBC katika kutoa huduma za kifedha zenye upendeleo maalum kwa wafugaji pamoja na wadau wote waliopo kwenye mnyororo wa sekta hiyo nchini. Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam ikihusisha viongozi waandamizi kutoka pande zote mbili. Wanaoshuhudia ni wanasheria kutoka pande zote mbili, Mathew Mtemi kutoka CCWT (kushoto) na Desmond Malyi kutoka NBC (kulia).
Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki ya NBC, Msafiri Shayo (wa tano kulia) na Katibu Mkuu wa CCWT, Mathayo Daniel (wa nne kushoto) wakionesha hati za makubalino baina ya taasisi hizo mbili yanayolenga kufungua milango kwa benki ya NBC katika kutoa huduma za kifedha zenye upendeleo maalum kwa wafugaji pamoja na wadau wote waliopo kwenye mnyororo wa sekta hiyo nchini.

Dar es Salaam - Septemba 5, 2024: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesaini makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji na Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) yanayolenga kufungua milango na fursa kwa wafugaji na wadau walioko kwenye mnyororo wa thamani wa sekta hiyo nchini ili kupata huduma za kifedha zilizo mahususi kulingana na mahitaji yao.

Hafla ya kusaini hati za makubaliano hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam ikihusisha viongozi waandamizi kutoka pande zote mbili ambapo ilishuhudiwa Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki ya NBC, Msafiri Shayo na Katibu Mkuu wa CCWT, Mathayo Daniel wakiwasilisha taasisi zao katika kusaini makubaliano hayo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Shayo alisema hatua hiyo ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo katika kukuza na kuboresha mnyororo wa thamani wa wakulima na wafugaji nchini kupitia uwezeshaji utakaowasaidia wadau hao kuendesha shughuli zao kisasa zaidi sambamba na kuongeza vipato na ajira, lengo likiwa ni kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla.

TAFINA BEGINS COUNTDOWN FOR EAST AFRICAN FINTECH INVESTMENT FORUM

The Vice Chairman of the Network of Financial Service Providers via Technology (TAFINA), Reuben Mwatosya (center), speaks to the press (not in the picture) about preparations for the upcoming East Africa Investment Forum (EAIF) 2024, scheduled to take place on September 12 and 13, 2024, at Serena Hotel in Dar es Salaam. On the right is Shadrack Kamenya, Secretary General of TAFINA, and on the left is Juliet Kiluwa.

Dar es Salaam, September 4, 2024 – The East African Fintech Investment Forum (EAIF) is set to ignite the fintech landscape across East Africa, with just 10 days remaining until the event. This collaborative initiative, spearheaded by the Tanzania Fintech Association (TAFINA) in partnership with fintech communities from Kenya (AFIK, FINTAK), Uganda (FITSPA) and Democratic Republic of Congo (DFA), aims to spotlight innovation, investment prospects, and collaborative opportunities within the region.

Event Details

The forum will take place on September 12-13, 2024, at the Serena Hotel in Dar es Salaam, Tanzania. The theme for this year’s event, 'Invest & Partner: Leave No One Behind,' encapsulates the forum's mission to drive inclusive growth and foster meaningful partnerships within East Africa’s rapidly evolving fintech sector. The forum will be inaugurated by the Central Bank of Tanzania on Day 1 and by the Embassy of the Netherlands on Day 2 .

New Updates on Panelists

We are excited to announce the latest additions to our panel of distinguished speakers who will share their insights and expertise. The panel will be represented by experts from Tigo, Stanbic, Vodacom, and CreditInfo, just to name a few.

These esteemed panelists will join other leading voices in fintech, policy, and investment, ensuring a robust and insightful dialogue throughout the forum.

Sponsors and Partners Onboard

The forum is backed by key industry players who have come on board as sponsors, including:
  • TALA, a leader in digital lending, supporting the forum’s mission to drive financial inclusion and innovation across East Africa.
  • Selcom Tanzania, a trailblazer in digital payment solutions, supporting the forum’s vision of a connected and thriving fintech ecosystem.
  • Serena Hotel, our esteemed venue and hotel partner, provides a world-class setting for the forum in the heart of Dar es Salaam.
These partnerships reflect the growing interest and commitment to the fintech sector's development across East Africa.

CONTINENTAL CORRUPTION BIGGEST ISSUE FOR AFRICAN YOUTH


  • Two thirds of African youth want to emigrate with North America and Western Europe as top destinations
JOHANNESBURG: Thursday, 5 September 2024 – Almost 60% of African youth are looking to emigrate in the next five years, with North America being the top destination of choice followed by Western Europe, where France, UK, Germany and Spain are the top destinations.

These findings are based off the 2024 edition of the African Youth Survey, which indicated that despite Africa’s youth having bounced back from the ravages of COVID 19, they aren’t happy with the direction their governments are taking. They are unafraid to speak out and they are unequivocal about what the greatest threat to their futures is – corruption.

Corruption is now front and centre in the minds of youth in the rest of the continent. They believe that corruption in their countries is robbing them of their birth right; the single greatest hurdle they face to achieve their own potential and achieve the better life that was denied their parents and their grandparents. Most of all, they don’t believe their governments are doing enough to address this scourge.

The 2024 edition of the African Youth Survey is the third edition of the unique biennial survey of African youths aged between 18 and 24. For this edition, 5,604 youths were interviewed in 16 countries. Since its inception in 2020, researchers have gauged the sentiments of more than 14,000 respondents across Africa, collectively representing 84% of the continent - on a variety of a different issues from their hopes and aspirations to their most pressing concerns.

DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE CEO PAYS COURTESY CALL ON HON. RIDHIWANI KIKWETE

Dar es Salaam Stock Exchange Chief Executive Officer, Peter Nalitolela (L) pays a courtesy call on Hon. Ridhiwani Kikwete (R) - Minister of State, Prime Minister’s Office (Labour, Youth, Employment & Persons with Disability). During the meeting, they discussed potential collaboration on enhancing youth employment opportunities through capital markets, promoting inclusive economic growth, and developing financial literacy programs tailored for persons with disabilities.

Wednesday, 4 September 2024

NBC, ZSSF WASAINI MoU YA MAUZO YA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU ZANZIBAR

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (kushoto) na Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Bw. Saleh Daudi Makame (kulia) wakisaini makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji (MoU) baina ya taasisi hizo mbili yanayotoa fursa kwa wadau hao kuuza nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na mfuko huo katika eneo la makazi ya kisasa yanayofahamika kama Dkt. Hussein Mwinyi yaliyopo eneo la Mombasa kwa Mchina Mwanzo, visiwani Zanzibar. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika Zanzibar.
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (kushoto) na Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Bw. Saleh Daudi Makame (kulia) wakionesha hati zilizosainiwa za makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji (MoU) baina ya taasisi hizo mbili.
Mkurugenzi Rasilimali Watu wa ZSSF, Bw. Saleh Daudi Makame (kulia) na Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Binafsi wa NBC, Bw. Elibariki Masuke (wa pili kulia) wakiziungumza wakati wa hafla hiyo. Makubaliano hayo yanatajwa kuwa yatafungua fursa mpya kwa wananchi wa Zanzibar, Tanzania Bara, na raia waliopo nje ya nchi ‘Diaspora’ kumiliki nyumba kwa gharama nafuu na kwa urahisi zaidi.
Mkurugenzi Rasilimali Watu wa ZSSF, Bw. Saleh Daudi Makame (kulia alieketi) na Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Binafsi wa NBC, Bw. Elibariki Masuke (kushoto alieketi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya maofisa waandamizi wa taasisi hizo wadau wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC akiwemo Meneja wa benki hiyo tawi la Zanzibar, Bw. Abdul Karim Mkila (wa tatu kulia) wakifuatilia hafla hiyo.

Zanzibar, Septemba 3, 2024: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesaini makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji (MoU) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) yanayotoa fursa kwa taasisi hizo mbili kuuza nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na mfuko huo katika makazi ya kisasa yanayofahamika kama Dkt. Hussein Mwinyi yaliyopo eneo la Mombasa kwa Mchina Mwanzo, visiwani Zanzibar.

Makubaliano hayo yaliyosainiwa leo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya ZSSF Zanzibar yanatajwa kuwa yatafungua fursa mpya kwa wananchi wa Zanzibar, Tanzania Bara, na raia waliopo nje ya nchi ‘Diaspora’ kuweza kumiliki nyumba kwa gharama nafuu na kwa urahisi zaidi.

Katika hafla ya kusaini makubaliano hayo ilishuhudiwa Mkurugenzi Rasilimali Watu wa ZSSF, Bw. Saleh Daudi Makame na Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Binafsi wa NBC, Bw. Elibariki Masuke wakiziwakilisha taasisi zao kwa kusaini makubaliano hayo, zoezi ambalo pia lilishuhudiwa na maofisa wengine waandamizi kutoka taasisi hizo.

Akizingumzia hatua hiyo, Bw. Masuke, alisema kuwa makubaliano hayo ni sehemu ya jitihada za benki hiyo kuboresha upatikanaji wa makazi bora nchini kupitia huduma zake.