Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Friday, 9 June 2023

EAC KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA VISIVYO VYA KIFORODHA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Katikati), akizungumza wakati wa Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta za Biashara, Viwanda Fedha na Uwekezaji (SCTIFI), wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo nchi hizo zimekubaliana kuondoa vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs), Mkutano huo umefanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha. Kushoto ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), na Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-maamry Mwamba.

Wataalamu wa Idara mbalimbali za Serikali wakifuatilia matukio ya Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta za Biashara, Viwanda Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo Nchi hizo zimekubaliana kuondoa vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs), wakati wa mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha.

Wajumbe kutoka Jamhuri ya Rwanda wakifuatilia kwa umakini Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta za Biashara, Viwanda Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo Nchi hizo zimekubaliana kuondoa vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha tarehe 3 Juni 2023.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akizungumza wakati wa mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta za Biashara, Viwanda Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo Nchi wanachama wa Jumuiya hiyo zimekubaliana kuondoa vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha, tarehe 3 Juni, 2023.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kushoto-mbele), na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa nne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Kisekta wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo, ambapo Nchi wanachama zimekubaliana kuondoa vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha, tarehe 3 Juni, 2023.


Na Suzan Mshakangoto, Benny Mwaipaja, Arusha


Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kuondoa vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs), huku vikwazo nane vikiendelea kushughulikiwa, na vikwazo vingine vipya vinne vimewasilishwa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara baina ya nchi hizo.

Vilevile, nchi hizo zimekubaliana kutoza kiwango cha dola 10 za kimarekani kwa kilomita 100 kwa ajili ya matumizi ya barabara (road user charge) kwa magari ya mizigo kutoka nchi moja kwenda nyingine katika Jumuiya hiyo badala ya kila nchi kuwa na viwango vyake vya tozo.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCTIFI) uliofanyika tarehe 03 Juni, 2023 katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha.

JOB VACANCY AT AfDB - CHIEF INVESTMENT OFFICER (INFRASTRUCTURE)


Full vacancy title: Chief Investment Officer (Infrastructure)
Location: Abidjan, Côte d'Ivoire
Position Grade: PL3
Position Number: 50052675
Posting Date: 05-Jun-2023
Closing Date: 18-Jun-2023

THE BANK:

Established in 1964, the African Development Bank (AfDB) is the premier Pan-African development institution, promoting economic growth and social progress across the continent. There are 81 member states, including 54 in Africa (Regional Member Countries). The Bank’s development agenda is delivering the financial and technical support for transformative projects that will significantly reduce poverty through inclusive and sustainable economic growth. In order to sharply focus the objectives of the Ten Year Strategy (2023 – 2032) and ensure greater developmental impact, five major areas (High 5s), all of which will accelerate our delivery for Africa, have been identified, namely: energy, agro-business, industrialization, regional integration and improving the quality of life for the people of Africa.

The Bank is seeking to recruit dynamic and highly skilled investment officers who will work on private sector infrastructure investment transactions within the Infrastructure and Urban Development Department (PICU) in the Infrastructure, Private Sector and Industrialization (PIVP) Vice Presidency.

THE POSITION

The core responsibilities of this position is to identify business opportunities and structure transactions related to private investments in transport and urban development infrastructures and services and originate projects for Bank financing.

THIS POSITION IS CLASSIFIED INTERNATIONAL STATUS AND ATTRACTS INTERNATIONAL TERMS AND CONDITIONS OF EMPLOYMENT.

UK EXPORT FINANCE (UKEF) KUSAIDIA UJENZI WA BARABARA NA UKARABATI WA UWANJA WA NDEGE PEMBA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa kikao na ujumbe kutoka Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw. Tim Reid, ambapo aliwashukuru kwa kukamilisha mchakato wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Treasury Square, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya UK Export Finance Bw. Tim Reid, akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambapo aliihakikishia Tanzania kupata fedha kwa ajili ya miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo, lakini pia kuendelea kufadhili miradi mingine ya kimkakati itakayowasilishwa na Serikali ikiwemo maji na nishati. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, (kushoto), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine (katikati) na Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade (kulia), wakisikiliza jambo wakati wa kikao na ujumbe kutoka Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw. Tim Reid, ambapo aliwashukuru kwa kukamilisha mchakato wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo. 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisikiliza jambo kutoka kwa ujumbe wa Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw. Tim Reid, ambapo aliwashukuru kwa kukamilisha mchakato wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo. 

Ujumbe kutoka Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya UK Export Finance Bw. Tim Reid (kulia), Mkuu wa Masuala ya Biashara Bw. Vomic Nur Shah (katikati) na Mkuu wa masuala ya Fedha ukanda wa Afrika Mashariki Bw. Isaac Kahara (kushoto), wakisikiliza jambo wakati wa kikao na ujumbe wa Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya UK Export Finance Bw. Tim Reid, baada ya kikao chao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw. Tim Reid (wa nne kushoto). Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, (wanne kulia), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine (wa tatu kulia) na Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade (wa pili kulia), Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa - Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Mursali Milanzi, Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Madeni - Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Tiba Kisonga (wa kwanza kushoto), Mkuu wa masuala ya Fedha ukanda wa Afrika Mashariki – UKEF Bw. Isaac Kahara (wa pili kushoto), na Mkuu wa Masuala ya Biashara - UKEF Bw. Vomic Nur Shah (wa tatu kushoto).

Na Benny Mwaipaja, Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishukuru Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), kwa kukamilisha mchakato wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo.

Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa UK Export Finance (UKEF), aliyepo nchini kwa ziara ya kikazi.

Alisema kuwa miradi hiyo, si tu kwamba itachokea shughuli za kiuchumi za visiwa hivyo ukiwemo utalii, bali pia itaboresha maisha ya wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

GEITA GOLD MINING YASIKIA KILIO CHA AKINA MAMA GEITA, YAGAWA VITANDA VYA KUJIFUNGULIA

Mkuu wa wilaya ya Geita, Kanali Boniphace Maghembe (wa nne katikati) akikata utepe kuashiria makabidhiano ya vitanda vya akina mama wajawazito kujifungulia kwa vituo vya afya vya Nyankumbu na Kasamwa. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji wa vituo hivyo, pamoja na Meneja Mwandamizi mahusiano GGML, Gilbert Mworia (wa pili kushoto).

Meneja Mwandamizi mahusiano GGML, Gilbert Mworia (wa pili kushoto) akizungumza katika hafla ya kukabidhi vitanda vilitotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya akina mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya vya Nyankumbu na Kasamwa.


Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), imetoa msaada wa vitanda vinne vya akina mama kujifungulia katika vituo vya afya vya Nyankumbu na Kasamwa vilivyopo kwenye Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita.

Msaada huo umekabidhiwa wiki iliyopita na Meneja Mwandamizi Mahusiano wa GGML, Gilbert Mworia kwa niaba ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo (GGGML) baada ya kupokea ombi la vituo hivyo vya afya kuhusu upungufu wa vitanda hivyo.

Alisema katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake iliyofanyika Machi mwaka huu, kampuni hiyo ilipokea ombi kuhusu uhaba wa vitanda vya kujifungulia kutoka kwa wanawake wa eneo hilo.

Aliongeza kuwa suala la afya na ustawi wa jamii ni jambo muhimu katika kila hatua ya maisha ya mtu yeyote anayekua, ndio maana kampuni ya GGML imeendelea kuboresha huduma za afya katika jamii inayozunguka mgodi huo na Tanzania kwa ujumla.

Thursday, 8 June 2023

BENKI YA CRDB KUWAZAWADIA SH. MILIONI 15.4 YA ADA YA SHULE WATEJA KUPITIA AKAUNTI YA JUNIOR JUMBO

Meneja Mwandamizi wa Mauzo Benki ya CRDB, Muhumuliza Buberwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Timiza Ndoto yake na Junior Jumbo” yenye lengo la kutoa elimu ya fedha kwa watoto na kuwahamasisha wazazi/ walezi juu ya umuhimu wa kuwawekea watoto wao akiba ambapo benki ya CRDB imetenga Shilingi milioni 15.4 kama zawadi ya ada kwa washindi wa kampeni hiyo inayotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Meneja Mauzo wa Benki ya CRDB, Amina Mawona (kushoto) na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Buza, Mary Joshua. Hafla hiyo imefanyika katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB.

Kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika mwaka huu, Benki ya CRDB imezindua promosheni ya “Timiza Ndoto yake na Junior Jumbo” ikiwa na lengo la kuwahamasisha wazazi/ walezi juu ya umuhimu wa kuwawekea watoto wao akiba.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Meneja Mwandamizi wa Mauzo, Muhumuliza Buberwa amesema kupitia kampeni hiyo Benki ya CRDB pia imejipanga kutoa elimu ya fedha kwa watoto ili kuanza kuwaandaa mapema kukabiliana na changamoto za kifedha. “Tumekuwa tukiwafundisha watoto juu ya mambo mbalimbali katika maisha, lakini watoto walio wengi wanakosa elimu juu ya fedha na kujiwekea akiba, elimu ambayo ni muhimu sana kwa watoto na vijana wetu.

Kampeni hii inakwenda kuhimiza juu ya ya umuhimu wa elimu, pamoja na kuwafundisha watoto kujenga utamaduni wa kuanza kujiwekea akiba,” amesema Buberwa.


Akielezea kuhusu muda wa kampeni hiyo Meneja Mauzo wa Benki ya CRDB, Amina Mawona amesema katika promosheni hiyo ya “Timiza Ndoto yake na Junior Jumbo” ambayo inatarajiwa kufikia kikomo Julai 5, 2023, Benki ya CRDB imetenga kiasi cha shilingi milioni 15.4 kama zawadi ya ada kwa ajili ya watoto 21 ambapo kila kanda ya benki hiyo kunatarajiwa kuwa na washindi watatu.

BENKI YA NBC YAZINDUA KOMBE JIPYA LA LIGI KUU TANZANIA BARA

Mkurugenzi wa fedha wa Bodi ya Ligi Ibrahim Mwayela (wa pili kushoto) akilifurahia kombe jipya la ligi kuu ya soka Tanzania bara lililoboreshwa baada ya kuzinduliwa rasmi na mdhamini mkuu benki ya NBC. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa NBC benki.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa Umma wa benki ya NBC Godwin Semunyu (kulia) akilifurahia kombe jipya la ligi kuu Tanzania bara na mkurugenzi wa fedha wa bodi ya ligi Ibrahim Mwayela (kushoto) wakati wa uzinduzi rasmi wa kombe hilo lililoboreshwa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wengine waalikwa wakati wa uzinduzi wa kombe jipya lililoboreshwa la ligi kuu ya NBC Tanzania bara.

Muonekano wa kombe jipya la ligi kuu ya NBC litakalokabidhiwa kwa bingwa wa msimu huu na misimu ijayo ya ligi.

Baadhi ya wafanyakazi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wengine waalikwa wakati wa uzinduzi wa kombe jipya lililoboreshwa la ligi kuu ya NBC lililozinduliwa jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam Juni 7, 2023: Mdhamini mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kombe jipya la ligi kuu ya soka ya Tanzania bara lililoboreshwa.

Kombe hilo ambalo lilizinduliwa mbele ya waandishi wa habari, litakabidhiwa kwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa msimu huu na misimu ijayo.

Akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa benki ya NBC, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa benki hiyo Godwin Semunyu alisema benki ya NBC ikiwa kama mdhamini mkuu wa ligi imeboresha kombe kutokana na maoni ya wadau mbali mbali wa soka.

“NBC ikiwa mdhamini mkuu wa ligi ya Tanzania bara inajivunia mafanikio makubwa ya ligi yetu. Kwa sasa ligi yetu ni ya tano kwa ubora Afrika na hii ni hatua kubwa na nzuri kwa soka letu. Leo tumezindua kombe lililoboreshwa ikiwa pia ni sehemu ya kuongeza thamani kwa ligi yetu,” alisema.

Godwin aliongeza kuwa, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya ligi, benki ya NBC inatoa bima kwa wachezaji wote wa ligi kuu pamoja na familia zao na pia mikopo ya mabasi kwa timu zinazoshiriki ligi.

Wednesday, 7 June 2023

GEITA GOLD MINING CELEBRATES WORLD ENVIRONMENT DAY BY EDUCATING AND EMPOWERING COMMUNITIES TO BEAT PLASTIC POLLUTION

GGML Senior Communications Officer, Laurian Pima speaks to residents of Uwanja Street in Geita District on the importance of separating plastic waste in continuation of the Company’s efforts to preserve the environment.


Geita Gold Mining Limited (GGML), one of AngloGold Ashanti's flagship mines in Tanzania, marked World Environment Day on 5 June with educational activities on the different types of plastics and the donation of containers that enable the public to properly separate plastic waste. The event took place in Geita town, where GGML staff and local authorities worked together to raise awareness about the importance of reducing, reusing and recycling plastics.

World Environment Day is an important global event organised by the United Nations Environment Programme, and this year the theme is 'Solutions to Plastic Pollution'. Plastic waste is a global problem that poses many threats to the environment, wildlife and human health..

GGML is aware that mining has a direct impact on the environment as land and water resources need to be developed. The company is committed to environmental stewardship and has taken various measures to minimise its environmental footprint and enhance its positive contribution to the communities around Geita.

BANK OF TANZANIA INSISTS FOREIGN EXCHANGE RESERVES SUFFICIENT


Bank of Tanzania (BoT) has said the country is experiencing shortages of US dollars, the dominant currency in international transactions but insisted that there was no cause for alarm, as the level of reserves was sufficient to cover four months of imports.

BoT Director of Economic Research and Policy, Dr Suleiman Missango told editors in Dar es Salaam yesterday that the stock of foreign exchange reserves declined to 4,881.2 million US dollars at the end of April 2023, from 5,461.4 million US dollars in the similar period in 2022.

Despite the decline, reserves remained adequate, covering 4.4 months of projected imports of goods and services, in line with the country benchmark of at least four months.

“There is a decline in foreign exchanges reserves in the country, however, that is not a crisis, as the level of reserves remains sufficient to cover four months of imports,” insisted Dr Missango.

Dr Missango said much as Tanzania’s external sector continued to be affected by cumulative effects of global shocks, particularly the war between Ukraine and Russia, Covid-19 and climate change, which largely impacted the global commodity prices, the country is grappling with the situation by instituting various measures.

He said that the available stock of foreign exchange which 4.9 billion US dollars is being used prudently to cope with the global dollar scarcity.

ECOBANK UNVEILS ITS SINGLE MARKET TRADE HUB, ONCE AGAIN PROMOTING INTRA-AFRICAN TRADE

Jeremy Awori, Chief Executive Officer, Ecobank Group.

Lomé, 1 June 2023 – Ecobank Group, the leading Pan-African banking Group, has unveiled its ‘Ecobank Single Market Trade Hub’ today as part of its commitment to promoting intra-African trade. The Ecobank Single Market Trade Hub (the “Trade Hub”) is live, with over 300 businesses from 22 countries having signed onto the digital platform so far. The Trade Hub connects traders across Africa, within the 1.4 billion people single market framework of the African Continental Free Trade Area (AfCFTA).

The Ecobank Single Market Trade Hub is a cutting-edge digital platform, which serves as an exchange and information repository, designed to respond to the evolving trading needs of SMEs and corporates within Africa's single market. The Trade Hub reduces the asymmetry in trade information and in this connection, leverages Ecobank’s wide client base and network advantage, through its presence in 35 African markets.

Jeremy Awori, Chief Executive Officer, Ecobank Group, said: “AfCFTA has created an immense opportunity for African businesses. As the pan-African bank with the most extensive coverage of Africa, Ecobank is perfectly placed to provide trade, information and payment solutions to support SMEs and corporates seeking to capitalize on the single market. The Ecobank Single Market Trade Hub is a new and remarkable addition to our portfolio of omni-channels, empowering businesses to thrive within Africa's single market.”

Monday, 5 June 2023

NMB YATOA GAWIO LA KIHISTORIA




Wanahisa wa Benki ya NMB wameidhinisha gawio la Shilingi Bilioni 143.1 kwa mwaka 2022, sawa na shilingi 286 kwa kila hisa moja katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 23 wa Wanahisa uliofanyika kwa njia ya mtandao leo. Hili ni ongezeko la 48% ukilinganisha na gawio la jumla la Shilingi Bilioni 96.7 lililolipwa mwaka 2021.


Benki hiyo ikiwa inaandika historia ya kutimiza miaka 25 ya kuwahudumia watanzania, hili ni gawio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na taasisi ya fedha nchini kwa wanahisa wake. Gawio hilo litalipwa kufikia tarehe 14 Juni 2023.


“Miaka minne iliyopita, tulilipa gawio la shilingi bilioni 33 kwa wanahisa wetu, lakini kwa mwaka 2022 gawio limeongezeka na kufikia Shilingi Bilioni 143.1. Ongezeko hili la gawio linaendana na ongezeko la mchango wetu katika uchumi wa taifa letu na maendeleo ya wananchi kupitia programu yetu ya uwajibikaji kwa jamii, ambapo kwa mwaka huu tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 6.2 zinazoelekezwa kwenye sekta ya afya, elimu, mazingira, elimu ya fedha na usaidizi wa majanga,” amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna.

VODACOM YAWAZAWADIA MAWAKALA WA USAJILI (FREELANCERS) KUPITIA KAMPENI YA 'LOYALTY PROGRAM' INAYOENDELEA NCHINI KOTE

Msimamizi wa Mauzo wa Vodacom Tanzania, Bw. Iddy Chitanda (kulia) akimkabidhi wakala wa usajili Bw. Goodluck Clement (kushoto) zawadi ya jiko la gesi na mtungi wake baada ya kujikusanyia pointi nyingi kwa kusajili wateja wapya wengi na wateja hao kununua salio na vifurushi kupitia M-Pesa. Kampuni hiyo inaendesha kampeni ya ‘Loyalty Program’ ikiwa imelenga kuboresha maslahi ya mawakala wake kupitia zawadi mbalimbali kama vile bima ya afya, pikipiki, luninga, simu za mkononi, magodoro, pesa taslimu na ikiwemo safari itakayogharamiwa kila kitu ya kwenda nchini Afrika ya Kusini mwezi Oktoba 2023.

Msimamizi wa Mauzo wa Vodacom Tanzania, Bw. Iddy Chitanda (kulia) akimkabidhi wakala wa usajili Bw. Mathias Lutumbi (kushoto) zawadi ya jiko la gesi na mtungi wake baada ya kujikusanyia pointi nyingi kwa kusajili wateja wapya wengi na wateja hao kununua salio na vifurushi kupitia M-Pesa. Kampuni hiyo inaendesha kampeni ya ‘Loyalty Program’ ikiwa imelenga kuboresha maslahi ya mawakala wake kupitia zawadi mbalimbali kama vile bima ya afya, pikipiki, luninga, simu za mkononi, magodoro, pesa taslimu na ikiwemo safari itakayogharamiwa kila kitu ya kwenda nchini Afrika ya Kusini mwezi Oktoba 2023.


Msimamizi wa Mauzo wa Vodacom Tanzania, Bw. Iddy Chitanda (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na mawakala wa usajili wa kampuni hiyo Bw. Mathias Lutumbi (kulia) na Bw. Goodluck Clement (kushoto) mara baada ya kuwakabidhi zawadi za majiko ya gesi na mitungi yake baada ya kujikusanyia pointi nyingi kila baada ya mteja mpya aliyemsajili akinunua salio na bando kwa M-Pesa. Kampuni hiyo inaendesha kampeni ya ‘Loyalty Program’ ikiwa imelenga kuboresha maslahi ya ‘mafrilansa’ wake kupitia zawadi mbalimbali kama vile bima ya afya, pikipiki, luninga, simu za mkononi, magodoro, pesa taslimu na ikiwemo safari itakayogharamiwa kila kitu ya kwenda nchini Afrika ya Kusini mwezi Oktoba 2023.

Friday, 2 June 2023

TASAF KUNUFAIKA NA MSAADA WA SH. BIL 15 KUTOKA UINGEREZA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, wakipeana mikono baada ya kubadilishana Hati za makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, wakionesha Hati ya makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati za msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), iliyofanyika jijini Dodoma.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba (katikati), ukiwa katika hafla ya makabidhiano ya hati za msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), iliyofanyika jijini Dodoma, kushoto ni Kamishna wa Fedha za nje kutoka Wizara hiyo, Bw. Rished Bade na kulia ni msaidizi wake, Bw. Melckizedeck Mbise.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akizungumza kuhusu nchi yake kuendelea kuisaidia Tanzania katika kupunguza umasikini, wakati wa hafla ya kubadilishana hati ya makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya TASAF, iliyofanyika jijini Dodoma.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba (kulia) na Ujumbe wa Uingereza Ukiongozwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati ya makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Tanzania imepokea msaada wa paundi milioni tano sawa na takribani shilingi bilioni 15 kutoka Serikali ya Ungereza kwa ajili ya awamu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF).

Makabidhiano ya Hati za makubaliano ya msaada huo yamefanyika jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Dkt. Mwamba alisema kuwa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini Tanzania unaendelea vizuri jambo linalosababisha washirika wa maendeleo kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya mpango huo.

Alisema kuwa amekutana na Balozi huyo wakiangazia masuala ya kunusuru kaya maskini lakini pia kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizo mbili ambao umedumu kwa muda mrefu.

AFRICAN DEVELOPMENT BANK APPROVES $20 MILLION INVESTMENT IN PRIVATE EQUITY FUND TARGETING THE INFRASTRUCTURE SECTOR IN AFRICA

The Nairobi-Thika Highway, Kenya.

The Board of Directors of the African Development Bank Group has approved an equity investment of $20 million in the Africa50 Infrastructure Acceleration Fund I(link is external), in support of its target to mobilize private capital for infrastructure across the continent.

The Africa50 Infrastructure Acceleration Fund I is a pan-African infrastructure private equity fund that is mobilizing up to $500 million for investment and value creation in strategic infrastructure sectors. These include power, energy, digital and social infrastructure, transportation, logistics, and water and sanitation.

The fund is sponsored by Africa50,(link is external) an infrastructure investment platform established by governments and the African Development Bank. Africa50 brings infrastructure project development and financing under one umbrella. Africa50 has a strong track record of investments in the private sector and of projects undertaken under a Public Private-Partnership (PPP) framework.

The mobilization of private capital is critical to closing the infrastructure financing gap in Africa, especially given the limited fiscal space of African governments which currently provide the largest source of infrastructure funding on the continent.

The Africa50 Infrastructure Acceleration Fund I was established as a vehicle to help execute Africa50’s mandate of mobilizing private capital and accelerating further investment flows into African infrastructure by targeting private and institutional investors.

African Development Bank Director for the Industrial and Trade Development Department, Abdu Mukhtar said the Bank’s investment in the Fund underlined its strategic nature and the fact that the Bank prioritizes investing in strategic infrastructure sectors that contribute to closing Africa’s infrastructure financing gap (estimated at $68-108 billion annually).

BANK OF TANZANIA TAKES MEASURES TO TACKLE DOLLAR VOLATILITY


The Bank of Tanzania (BoT) has issued new directives aimed at controlling foreign exchange trading in the country a directive that comes at a time when several African countries are struggling with the dollar shortage including Kenya.

The directive was issued by BoT Governor Emmanuel Tutuba and takes effect from today, Thursday, June 1, 2023.

The new controls impact the retail market, stating that all foreign exchange transactions exceeding $1 million per transaction shall at all times be traded within the inter-bank foreign exchange market at prevailing quoted prices.

The directives have tightened the noose on unlicensed international foreign currency brokers operating in Tanzania, prohibiting them from purchasing or selling currency in the country.

UDHAMINI WA NMB MIKUTANO YA ALAT WAFIKIA 1.2BN/-

Afisa Mkuu Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB – Bw. Alfred Shao, akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango, kwa niaba ya Benki ya NMB kwa kudhamini Mkutano Mkuu wa 37 wa ALAT Taifa kwa Sh. Milioni 200. Wakishuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Mhe. Angella Kairuki pamoja na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa – Mhe. Constantine Sima (kati kati).

Benki ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi ya Tawala za Mitaa (ALAT Taifa), ikiwemo kudhamini Mikutano yake Mikuu ya Mwaka kwa takribani miaka 7 mfululizo na hadi sasa jumla ya Shilingi bilioni 1.2 zimeshatumika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango akielezewa mafanikio na mipango iliyopo kati ya Benki ya NMB na ALAT Taifa katika ngazi zote, Afisa Mkuu Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB – Bw. Alfred Shao, alipotembelea banda la NMB katika viwanja vya AICC Arusha, ulipokua unafanyika Mkutano Mkuu wa 37 wa ALAT Taifa.

Haya yamesemwa na Afisa Mkuu Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB – Bw. Alfred Shao wakati akiwasilisha mada katika Mkutano wa 37 wa ALAT uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa AICC- Arusha ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango alikuwa Mgeni rasmi.

Afisa Mkuu Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB – Bw. Alfred Shao, (kushoto) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa – Mhe. Sima Constantine Sima mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 200 ikiwa ni udhamini wa NMB kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika jijini Arusha. Akishuhudia ni Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali Benki wa NMB - Vicky Bishubo.

Mkutano huu wenye Kauli Mbiu “Miundombinu iliyoboreshwa ni chachu ya utoaji wa huduma bora katika Mamlaka za Serikali za Mitaa” uliwakutanisha zaidi ya watumishi 500 kutoka Halmashauri zote 184 za Majiji, Manispaa, Wilaya na Miji kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Aidha, Bw. Shao alielezea kuwa, Benki ya NMB kama mdau wa maendeleo kupitia Halmashauri zote chini, imekuwa mshirika mkubwa sana kuboresha miundombinu ya elimu, afya, usafirishaji na mazingira na inaendelea kushiriki kikamilifu katika kutoa dhamana kwa Makandarasi zaidi ya 580 zenye thamani ya bilioni 49 katika hatua zote kuanzia hatua ya kuomba na kutekeleza miundombinu chini ya TARURA. Kupitia mifumo na mtandao mpana wa NMB umesaidia Serikali katika makusanyo ya mapato ya zaidi ya shilingi Trilioni 9.8 kuanzia mwaka 2018.

Thursday, 1 June 2023

UBER AND TIGO ANNOUNCE PARTNERSHIP TO ROLL OUT CASHBACK INITIATIVES FOR DRIVERS AND RIDERS

The CEO of Uber East Africa, Mr Imran Manji (second left) shakes hands with Tigo Pesa’s Chief Officer, Angelica Pesha (second right) after announcing a partnership to roll out cashback initiatives for drivers and riders. Standing with the CEO of Uber East Africa is Monica Mziray, Operations Manager (left) of Uber Tanzania and a fellow Manager from Tigo Tanzania (right).

Monica Mziray, Operations Manager of Uber Tanzania speaks to the media and stakeholders from Tigo and Uber (not in the picture) during a press briefing in Dar es Salaam.

The CEO of Uber East Africa, Mr Imran Manji (left) speaks with Tigopesa Chief Offer, Angelina Pesha (second left) during a press briefing that was held in Dar es Salaam.

Wednesday 31 May 2023, Dar es Salaam, Tanzania: Uber and Tigo have announced a one-year partnership to roll out a series of cashback initiatives for drivers and riders who use the Uber app.

Effective immediately, drivers on the Uber platform have the option of being registered by Tigo Pesa as Lipa Kwa Simu merchants to enable them to collect funds from riders that use other telecommunication networks. Drivers will be able to cash out from their Lipa Kwa Simu merchant accounts with zero charges through diverse Tigo Pesa agents for any amount below Tshs. 500,000 per day.

Riders who pay for their trips using Tigo Pesa Lipa Kwa Simu will receive 10% cashback in their Tigo Pesa wallets, in addition to other periodic promotions that Uber may run through the app. Drivers who collect funds using their Lipa Kwa Simu merchant accounts will get a commission of 20% of the transactional fees for fares paid by riders.

Uber’s Head of East Africa, Imran Manji says, “We are excited to announce this partnership with Tigo to roll out diverse savings benefits for drivers and riders on the Uber platform. Riders will be able to save on costs and drivers will have the opportunity to increase their earnings. In addition, this is an important collaboration as it provides a seamless and convenient payment avenue on our platform, including those who may be unbanked or underserved by formal financial systems, and typically depend on cash.”